Kwanini Serikali Tanzania inawachukulia poa diaspora

mbwewe

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
3,262
3,392
Naandika hili bandiko nikiwa nimetoka kuangalia video ya traveling sister huko YouTube.

Kwa msio mjua traveling sister, huyu dada ni Mmarekani mweusi ambayo ameolewa na Mtanzania na wanaishi Arusha.

Sasa kwenye hiyo video wamekutana na diaspora wengine wanaoishi hpo Arusha wakiwemo Wajamaika, kikubwa wanacholalamika ni mazingira magumu ya kufanya biashara nchini Tanzania kutokana na sheria ambazo zimeweka mazingira magumu kwa mtu asiye raia wa Tanzania kufanya biashara.

Kwa mfano issue km residential permit imekuwa ni ngumu kuipata na ina gharama sana, sasa ili kulinda status zao za ukazi inabidi hawa diaspora kila baada ya miezi mitatu waende kenya bila kupenda ili wagongewe viza mpakani.

Sasa najiuliza kwanini serikali isiwawekee mazingira bora hawa watu kwa sababu hawa wana mitaji na mawazo ya kutuwezesha kupiga hatua km nchi .

Na isitoshe hawa watu ni Waafrika wenzetu ambao mababu zao walichukuliwa utumwani bila kupenda. Sasa Leo wanarudi nyumbani mnawalipisha permit $ 3000 kweli?

Kwa mujibu wa Traveling Sister kuna Wamarekani weusi wengi sana wana interest ya kuja Tanzania kuishi na kuwekeza Ila wanakwamisha na sheria zisizo rafiki na badala yake wengi wanachagua Ghana ambapo wana initiative maalum kwa ajili yao.

Ushauri wangu kwa serikali kuanza kuwachukulia serious diaspora wote kwa ujumla, kwani kwa trend ninayoiona inayoendelea sasa ivi kwenye hili bara letu la Afrika nchi ambayo itafungua milango kwa diaspora ndyo itakayopata maendeleo kwa haraka zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuki kwa Nguruwe! Hao diaspora huko makwao wamekuwa na sheria kali sana pale vijana wetu wa kiafrica wanapokuwa na uhitaji wa kwenda kusaka fursa makwao huko, issues kama visa, working permit na mengineyo havipatikani kirahisi, ni lazima na sisi tuweke sheria Kali kulinda vya kwetu. Maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe si wageni!
 
Tatizo travel sister nae mjanja mjanja na sijui aliingiiaje pale ni hivyo kihuni huni tu,diaspora hapo bongo hutambuliki utaulizwa maswali ya ajabu na ukiuliza ww utaambiwa umetoka somalia etc wakati we kwenu huko Turiani ni mlunguluka tu,huyo yuko hapo siku nyingi sema sasa wameshindwana ndo analalamika.
anyway next destination Jamaica man then Cuba.
 
Mkuki kwa Nguruwe! Hao diaspora huko makwao wamekuwa na sheria kali sana pale vijana wetu wa kiafrica wanapokuwa na uhitaji wa kwenda kusaka fursa makwao huko, issues kama visa, working permit na mengineyo havipatikani kirahisi, ni lazima na sisi tuweke sheria Kali kulinda vya kwetu. Maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe si wageni!
utamuitaje mtu mweusi km wewe mgeni au hujasoma Uzi vizuri? halafu huko marekani hizo sheria Kali zimewekwa na watu weusi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo travl sister nae mjanja mjanja na sijui aliingiiaje pale ni hivyo kihunu huni tu,diaspora hapo bongo hutambuliki utaulizwa maswali y jbu n ukiuliza ww utaambiwa umetoka somalia etc ni mlunguluka tu,huyo yuko hapo siku nyingi sema sasa wameshindwana ndo analalamika.
anyway next destination Jamaica man then Cuba.
out of the topic

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mpaka leo sijaelewa ni kwa nini serikali ya Ccm haitaki kusikia kitu kinachoitwa URAIA PACHA. Kwa nini tusijifunze faida na changamoto za aina hii ya Uraia kwa maendeleo ya nchi yetu?
 
Mimi mpaka leo sijaelewa ni kwa nini serikali ya Ccm haitaki kusikia kitu kinachoitwa URAIA PACHA. Kwa nini tusijifunze faida na changamoto za aina hii ya Uraia kwa maendeleo ya nchi yetu?
 
Tatizo hawajawahi piga hesabu ni kiasi hawa diaspora wanachangia na wakitengeneza mazingira mazuri kwa diaspora watapata kiasi gani Kama hapo Uganda raia wao wanapeta sana kwa kufanya uwekezaji nyumbani wakiwa nje au wanaporudi, Botswana na Zimbabwe pia ingawaje Uchumi wao umedorola bongo unakuja na pick up za utali mfano tano ukalipia tatu ukaacha mbili ili uje umalizie unaambiwa zishai gia kwenye mnada huko unaanza kupigana ili zitoke huko uzilipie hawapo kwa ajili ya kuwasaidia ni kuwanyonya tuu...
 
Naandika hili bandiko nikiwa nimetoka kuangalia video ya traveling sister huko youtube.

kwa msio mjua traveling sister hyu dada ni mmarekani mweusi ambayo ameolewa na mtanzania na wanaishi arusha.

sasa kwenye hyo video wamekutana na diaspora wengine wanaoishi hpo arusha wakiwemo wajamaika, kikubwa wanacholalamika ni mazingira magumu ya kufanya biashara nchini tanzania kutokana na sheria ambazo zimeweka mazingira magumu kwa mtu asiye raia wa tanzania kufanya biashara

kwa mfano issue km residential permit imekuwa ni ngumu kuipata na ina gharama sana, sasa ili kulinda status zao za ukazi inabidi hawa diaspora kila baada ya miezi mitatu waende kenya bila kupenda ili wagongewe viza mpakani.

sasa najiuliza kwanini serikali isiwawekee mazingira bora hawa watu kwa sababu hawa wana mitaji na mawazo ya kutuwezesha kupiga hatua km nchi .

na isitoshe hawa watu ni waafrika wenzetu ambao mababu zao walichukuliwa utumwani bila kupenda. sasa Leo wanarudi nyumbani mnawalipisha permit $ 3000 kweli?

kwa mujibu wa traveling sister kuna wamarekani weusi wengi sana wana interest ya kuja tanzania kuishi na kuwekeza Ila wanakwamisha na sheria zisizo rafiki na badala yake wengi wanachagua Ghana ambapo wana initiative maalum kwa ajili yao.

ushauri wangu kwa serikali kuanza kuwachukulia serious diaspora wote kwa ujumla, kwani kwa trend ninayoiona inayoendelea sasa ivi kwenye hili bara letu la afrika nchi ambayo itafungua milango kwa diaspora ndyo itakayopata maendeleo kwa haraka zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kila mmarekani mweusi ni diaspora
 
Back
Top Bottom