Kwanini Serikali na CCM hawakumpokea Kibanda?

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Sote tunajua Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alirudi jana akitokea Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa. Lakini jambo la kushangaza kwa serikali yetu na hasa chama tawala CCM kutojitokeza kumpokea kama wafanyavyo kwa watu wengine wakiwemo wasanii pindi warudipo. Kitendo kama hiki kimeniacha na sintofahamu hadi pale Kibanda mwenyewe atapotoa yaliyo moyoni kama alivyoahidi.
 
Hebu nipe flashback kidogo.Nani (private citizen)alirudi nchini kutoka nje ya nchi akapokelewa na serikali na ccm?
 
Jamani siyo mtumishi wao. Hapo mnawaonea.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
4.0. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.
4.1. Uchunguzi ulifuatilia masuala mbalimbali ikiwamo miendendo ya watu waliotajwa kwa njia moja au nyingine kuhusinaa na tukio hili. Hata hivyo, karibu watu wote waliohojiwa, akiwamo Kibanda mwenyewe aliyeumizwa walimtaja kwa kutilia shaka mwenendo wa kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandano ya kijamii siku ya Machi 6, 2013.
4.2. Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick katika naye alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo. Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili, fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.
4.3. Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu wengi hasa baada ya kuleeza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kiwaida mwendo wake hauwezi kuzidi dakika 10.
 
Sote tunajua Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alirudi jana akitokea Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa. Lakini jambo la kushangaza kwa serikali yetu na hasa chama tawala CCM kutojitokeza kumpokea kama wafanyavyo kwa watu wengine wakiwemo wasanii pindi warudipo. Kitendo kama hiki kimeniacha na sintofahamu hadi pale Kibanda mwenyewe atapotoa yaliyo moyoni kama alivyoahidi.

Acha mambo yako wewe, wagonjwa wote wanaotoka kutibiwa nje wanapata mapokezi ya serikali?
 
Wanasikitika ni kwa nini hawakummaliza kabisa!!!
3.4. Kibanda hakuhama Free Media kwa amani. Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda. Kwa maneno yake, anasema:"Nilihofu kuwa Mbowe anaweza kutugombanisha. Nikaona ni bora niondoke nisije nikagombana na Mbowe au Ngurumo."Anasema alianza kupoteza mamlaka yake na kutoaminika kwa mwajiri wake baada ya kuandika makala kuhusu Abdulrahman Kinana ambayo kabla ya kuiandika hakuwa na wazo la kuondoka. Yaliyofuata baada ya makala hiyo, yalimshukuma aondoke
 
4.0. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.
4.1. Uchunguzi ulifuatilia masuala mbalimbali ikiwamo miendendo ya watu waliotajwa kwa njia moja au nyingine kuhusinaa na tukio hili. Hata hivyo, karibu watu wote waliohojiwa, akiwamo Kibanda mwenyewe aliyeumizwa walimtaja kwa kutilia shaka mwenendo wa kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandano ya kijamii siku ya Machi 6, 2013.
4.2. Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick katika naye alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo. Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili, fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.
4.3. Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu wengi hasa baada ya kuleeza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kiwaida mwendo wake hauwezi kuzidi dakika 10.

Na huyu huyu LUDOVICK alikuwa best wa karibu sana na gaidi LWAKATARE, na KIBANDA aliondoka Tanzania Daima siyo kawa jema bali kwa ugomvi, hivi hapa bado tunatafuta mchawi.
 
Sote tunajua Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alirudi jana akitokea Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa. Lakini jambo la kushangaza kwa serikali yetu na hasa chama tawala CCM kutojitokeza kumpokea kama wafanyavyo kwa watu wengine wakiwemo wasanii pindi warudipo. Kitendo kama hiki kimeniacha na sintofahamu hadi pale Kibanda mwenyewe atapotoa yaliyo moyoni kama alivyoahidi.

kwani kibanda ana nafasi gani katika taifa kiasi cha kupokelewa na viongozi wa chama na serikali?
 
3.4.Kibanda hakuhama Free Media kwa amani. Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda. Kwa maneno yake, anasema:"Nilihofu kuwa Mbowe anaweza kutugombanisha. Nikaona ni bora niondoke nisije nikagombana na Mbowe au Ngurumo."Anasema alianza kupoteza mamlaka yake na kutoaminika kwa mwajiri wake baada ya kuandika makala kuhusu Abdulrahman Kinana ambayo kabla ya kuiandika hakuwa na wazo la kuondoka. Yaliyofuata baada ya makala hiyo, yalimshukuma aondoke

Kazi kweli kweli. Mbona alipokwenda kutibiwa nje CHADEMA hawakumsindikiza kwa mabango kama ilivyokuwa kwa ULIMBOKA? KIBANDA anaajua watesaji wake asije na suaga za ajabu hapa kutaka kuwafurahisha watu, aseme tu kuwa CHADEMA wanahusika mambo yaishe.
 
Kwa kibanda ni mtumishi wa ccm au serikali mpaka apokelewe kiserikali.
 
Walewale waliomtesa wanafiki wakubwa eti wanajifanya kwenda kumpokea na ile hali wao ndo waliomtesa,kazi kweli.
 
Kwenye sheria kuna kitu kinaitwa suspicious character.

Kwa matukio mawili ya utekwaji ya Dr Ulimboka na Absolom Kibanda,mwenendo wa jeshi letu la polisi,kushughulikia matukio hayo,unazua maswali mengi,yanayokosa majibu.

Katika tukio la kwanza la kutekwa kwa Dr Ulimboka,inafahamika wazi kuwa ni jeshi la polisi lenyewe ambalo linasisitiza dhana ya polisijamii,ambayo dhana yake kuu ni kuwa raia walisaidie jeshi hilo katika kuwabaini wahalifu.

Sasa swali kubwa linaloulizwa na wananchi ni kuwa iweje dhana hiyo imepuuzwa kabisa na jeshi hilo,baada ya mtekwaji mwenyewe Dr Ulimboka,kujitokeza hadharani na kumtaja kwa jina mtu anayeitwa Ramadhan Ighondo,kuwa ndiye alikuwa kinara wa utekaji huo,iweje basi jeshi la polisi,pamoja na kurahisisiwa kazi ya kuwapata wahalifu,waliomdhuru Ulimboka,jeshi hilo lishindwe hata kumtia mbaroni,angalau tu hata kwa mahojiano,ili tu kubaini,kama kinachosemwa na Dr Ulimboka,kina ukweli au hakina ukweli?!!

Kuhusu suala la Kibanda,iweje jeshi la polisi pamoja na tambo zao za mara kwa mara,kuwa jeshi hilo lina intelejensia ya hali ya juu kwa kuweza kubaini wahalifu,katika kipindi kifupi sana,iweje sasa ni miezi mitatu kamili,liwe halijamtia nguvuni hata mtuhumiwa mmoja,angalau tu kwa mahojiano??!!
 
Kitu kingine kinachoonyesha dhahiri suspicious character,katika sakata hili la Ulimboka na Kibanda,ni kitendo cha JK,kumpandisha cheo afande Kova,badala ya kumfukuza kazi.

Kwa maana hiyo haihitaji mtu kuwa na degree ya sheria,kubaini kuwa kwa kuunganisha hizo dots,unapata ushahidi usio na mashaka yeyote kuwa,serikali ya CCM,ni watuhumiwa wakuu,wa masakata hayo mawili,ya Ulimboka na Kibanda!!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom