Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Ni wazi kuwa katika mchakato wa kupanda madaraja watumishi ajira mpya 2012, walipanda lakini wakanyang'anywa mwaka 2016.
Wengine (wa 2012) wakapanda mwaka 2017 na wengine 2018 na wameendelea na mishahara mipya mpaka leo. Kwanini walipandisha baadhi ya halmashauri?
Waraka mpya wa kupandisha madaraja kuanzia mei mos 2019 naona unatekelezwa tofauti katika halmashauri tofauti. Wengine wanapandisha wa 2012 tu, wengine 2012 na 2013, wengine 2012, 2013 na 2014. Katika ufatiliaji wanadai kuwa walipokea maagizo ya kufanya wanayoyafanya. Kwanini watoe waraka baadae watoe maagizo kimyakimya?
HOJA:
-Je, hayo maagizo wamepewa baahi ya halmashauri tu?
-Kwanini wanapandisha tofauti tofauti kama maagizo yapo sawa?
-Ni uzembe wa maafisa utumishi?
-Kama mishahara inalipwa na hazina, bajeti za halmashauri zinahusikaje?
NB: Uchunguzi unaendelea mpaka mishahara itoke tuone kama wanapanda kwa maneno au matendo.