Kwanini serikali isiwatumie wataalamu wa ndani kufanya ukaguzi wa BoT?

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Naomba kutoa wazo kwa waziri serikali kwanini wanaendelea kutoa mabilioni ya fedha kuwapa kampuni za ukaguzi kama KPMG. E&Y, PWC kufanya ukaguzi kwa taasisi za umma kama BOT na sehemu zingine . ninachokiona ni kwamba taifa kwa mfano linatumia zaidi ya bilion 30 kufanya ukaguzi kwenye bank kuu (BOT) pekee lakini kumbuka kazi hizi zingeweza kufanya na National Audit chini ya CAG na kama tunahitaji kwenda mbele basi ni wakati taasisi hii kuongezewa nguvu na washirikiane na TRA kubana makampuni ya madini, mashirika ya simu yani VODACOM ,TIGO NA AIRTEL kwenye ukwepaji wa kodi .

kwa mfano leo ukiangalia ukwepaji wa kodi kwenye sekta ya simu

kuna namba za simu milioni 17 na wastani wa matumizi ta vocha ni kama sh 600 kwa kila mtu hivyo ukitazama pato lao ni

17,000,000 X 600 = bilion 10.2 kwa siku

10.2 x365 = bilion 3723 kwa mwaka

3723 bilion X 18%( VAT) =bilioni 670 hii ni kodi ambayo TRA walistahili kupata yani ni VAT pekee lakini kuna kodi zingine ambazo ni corporate tax ambayo ni 30% ya faida lakini sijaongelea hapo je tuagalie kama tungedhibiti kodi kwenye makampuni ya simu kwenye vitengo vyote

Kwenye sekta ya mawasiliano
1. vat ni 670 bilioni

2.internet service kwenye taasisi za umma ?

3.M-PESA charge za kutuma fedha ?

4. Corparate tax 30% ?

kwenye sekta ya madini

1. VAT ?

2.corparate ?

3.royalty ?



kwanini tuendelee kupoteza fedha nyingi na tusianza kutumia shirika letu la ukaguzi washirikiane na TRA kudhibiti tatizo ili na kulinda rasilimali za taifa badala ya kuendelea kutumia kampuni za kigeni ? je tumeshindwa kuajiri vijana wetu wa NAO na TRA kudhibiti tatizo hili
 
Mkuu sehemu nyeti zenye ulaji CAG haitwi,wanaitwa wale wenye kunegotiate deal na hawa unaswa tu pale ktk kunegotiate Audit fee. Pia aya makampuni yako kiaina kama ya kigeni yakianika uozo yatapewa nauli,mwisho wa siku CAG ataambiwa akakimbizane na maDT,DC DAS na wenyeviti wa kata. Huku nssf,bot,n.k kuna wenyewe! Ktk ku audit utaambia kazi watapewa among the big 4 audit firm,sijui wanadhani ukisema 'the big 4'ndo umetaja,economy,efficiency and effectiveness kama ilivo ktk auditing profession!! Ukiwaambia wawaajiri vijana wazarendo pale National audit utaambiwa bajeti hamna,kama mwaka huu eti wanataka vijana mia tu kuja kufuatilia malipo ya trioni13.5 ya bajeti pamoja na miaka iliyopita. Wahasibu wa wilaya ni std8 wa zamani,na wengine ni mababu wakati vijana wako kijiweni wamesubiri ujuzi ukomae maana inahitajika 3 to 10years,au wasubiri wazee wafe. TRA imeanza kukengeuka na kujihusisha na siasa,ajira zinaenda kwa kupangana,vyote ivi vinakwamisha juhudi za kukuza uchumi.
 
wanaogopa siri zitafumuka, wazungu ni wazuri katika kuficha siri mpaka washitukiwe ndio wanasema
 
Naomba kutoa wazo kwa waziri serikali kwanini wanaendelea kutoa mabilioni ya fedha kuwapa kampuni za ukaguzi kama KPMG. E&Y, PWC kufanya ukaguzi kwa taasisi za umma kama BOT na sehemu zingine . ninachokiona ni kwamba taifa kwa mfano linatumia zaidi ya bilion 30 kufanya ukaguzi kwenye bank kuu (BOT) pekee lakini kumbuka kazi hizi zingeweza kufanya na National Audit chini ya CAG na kama tunahitaji kwenda mbele basi ni wakati taasisi hii kuongezewa nguvu na washirikiane na TRA kubana makampuni ya madini, mashirika ya simu yani VODACOM ,TIGO NA AIRTEL kwenye ukwepaji wa kodi .kwa mfano leo ukiangalia ukwepaji wa kodi kwenye sekta ya simukuna namba za simu milioni 17 na wastani wa matumizi ta vocha ni kama sh 600 kwa kila mtu hivyo ukitazama pato lao ni17,000,000 X 600 = bilion 10.2 kwa siku10.2 x365 = bilion 3723 kwa mwaka 3723 bilion X 18%( VAT) =bilioni 670 hii ni kodi ambayo TRA walistahili kupata yani ni VAT pekee lakini kuna kodi zingine ambazo ni corporate tax ambayo ni 30% ya faida lakini sijaongelea hapo je tuagalie kama tungedhibiti kodi kwenye makampuni ya simu kwenye vitengo vyoteKwenye sekta ya mawasiliano1. vat ni 670 bilioni2.internet service kwenye taasisi za umma ?3.M-PESA charge za kutuma fedha ?4. Corparate tax 30% ?kwenye sekta ya madini1. VAT ?2.corparate ?3.royalty ?kwanini tuendelee kupoteza fedha nyingi na tusianza kutumia shirika letu la ukaguzi washirikiane na TRA kudhibiti tatizo ili na kulinda rasilimali za taifa badala ya kuendelea kutumia kampuni za kigeni ? je tumeshindwa kuajiri vijana wetu wa NAO na TRA kudhibiti tatizo hili
Mkuu kweli taasisi nyeti kama BOT ni muhimu ikaguliwe na CAG mwenyewe.zinatumika pesa nyingi sana ingawa nakubali hizi international firm zinafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu.ila pamoja na ubora wao lakini ni vizuri kumtumia CAG kuepusha uwezekano wa ukaguzi ku influence mengine.Bot ndio wanaoratibu uchumi na pengine strategy yao isiwapendeze wafadhili ambao hizi firm ndio zinatokea.ingawa CAG mwenyewe ndio anateua lakini hata mm sijui kwanini mara nyingi tunatumia hawa jamaa ingawa wazawa walishapewa pia( TAC) na wakafanya vizuri tu.nafikiri tuwape nafasi wazawa ktk kazi nyeti ili mzunguko wa pesa uwe humu humu.road construction sawa pengine zinataka substantial capital,hata ukaguzi jamani unaotegemea largely intellectual capacity?
 
hapa tuwekane sawa,CAG ndio mwenye mamlaka ya kukagua au kuteua wa kufanya kwa niaba yake hivyo hii inagusa kitengo cha CAG directly.
 
yapo maeneo mengi CAG anaweza ku outsource ukaguzi lakini sio BOT inayopanga mwelekeo wa uchumi wa nchi yetu.
 
makampuni ya audit makubwa ndio yanachangia kampeni za chama cha mapinduzi nyinyi pigeni kelele mpaka mfe lakini kazi za maana zote zitachukuliwa na wajanja
 
makampuni ya audit makubwa ndio yanachangia kampeni za chama cha mapinduzi nyinyi pigeni kelele mpaka mfe lakini kazi za maana zote zitachukuliwa na wajanja
kuchangia kampeni si sababu ya msingi ya kufanya mambo yasiyo na faida kwa jamii husika. lazima tufike wakati tuwe na udhibiti mahususi kwenye rasilimali zetu
 
tatizo ni serikali sio makampuni ya kigeni
makampuni haya nayo yanamatatizo kwani ni makampuni ya kijambazi na mafisadi kwani yanachota fedha nyingi kwa kazi ndogo wanayofanya kwenye ukaguzi lakini kikubwa ninachokiona ni kutumia ushawishi wa viongozi wa kisiasa kupata fedha . ni wakati wa taifa na CAG mwenyewe kuweka wazi nini cha kufanyika katika sekta ya usimamizi wa fedha za umma
 
Back
Top Bottom