Kwanini Serikali isiboreshe Magereza kama ya Hong Kong?

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
WAPO WALIOFUNGWA HONG KONG NA HAWATAKI WARUDISHWE KWENYE NCHI ZAO.

Father John ametusogezea siri kuwa kuna baadhi ya wafungwa ambao wapo kwenye magereza ya Hong Kong na hawataki kurudi nchini kwao kutokana na Magereza ya kule yalivyo.

“Magereza ya Hong Kong yapo vizuri yaani kwenye Chakula, makazi na mavazi vinatolewa bure lakini ukienda kwenye nchi nyingine kidogo ni shida familia ndiyo inabidi kulipia.

Hong Kong kuna wafungwa ambao wanafanya shughuli mbalimbali wakiwa gerezani na wanajipatia kipato cha kutuma kwa familia zao na wengine wanaingiza dolla 80 kwa mwezi na zaidi na wanasema kipato wanachokipata ni kikubwa kuliko wanachokipata wakiwa nchini kwao” - Father John, PowerBreakFast

Sent from toyota Allex
 
Tuna methali ya Kiswahili isemayo "Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu"

Magereza yetu yamejaribu kuuvua utu wa mwanadamu na kumvalisha vazi la mateso kwa wakati ambao anakuwa gerezani na huo ndio ulimwengu ambao unazungumziwa katika ile methali.

Pili, Kuna nchi ambazo hatupaswi hata kujifananisha nao katika sekta yoyote ila hata kiakili sijui huyo msela kapata wapi ujasiri wa kutaka tuwe kama hao.
 
Siyo Hong Kong tu hata Brazil na Argentina. Ukifungwa unaweza ukaafanya Kazi na ukapata posho Wenzetu walishauweka Mfumo huo kitambo.

Mbona Tanzania wafungwa wanafanya useremala, wanatengeneza viatu, wanafanya ufugaji, wanalima na wanazalisha lakini Kazi yote hiyo hapewi hata senti. Ukiuliza sababu Wanakwambia ndy malipo ya makosa yake aliyo fanya uraiani
Jela za wenzetu ni correction facility.

Wao hawamkomoi mfungwa wa najaribu kumbadilisha. Ila kwa case ya tz kuhusu wafungwa walipwe, wangelipwa wale tu wanaofanya Kazi za kuzalisha bidhaaa za magereza

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa naangalia documentary moja ya magereza huko Brazil Wanwake wana hadi mashindano Ya umiss Na ukiwa fresh ukimaliza Muda wako Unaendelea na kazi kama Miss Au model

Wanakula vizuri
wanajiremba and so on
 
5174AC8D-7EAC-40AA-94CE-14B20FEBB1EC.jpeg
rio de jeneiro maximam Security prison Beauty contenstants
 
Nilikuwa naangalia documentary moja ya magereza huko Brazil Wanwake wana hadi mashindano Ya umiss Na ukiwa fresh ukimaliza Muda wako Unaendelea na kazi kama Miss Au model

Wanakula vizuri
wanajiremba and so on
Mimi Kuna mtu namjua alifungwa Sao brazil
Na kila mwezi alikuwa anawatumia ndg zke vijisenti.... Maana yeye alikuwa anapiga Kazi jela

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magereza hutofautiana kulingana na uchumi wa nchi. Sasa kama kibarua wa kiwandani tanzania anapokea buku tano kwa kutwa sawa na usd 2 ambayo sawa na usd60 kwa mwezi kwa nini asifungwe tu akapokekea usd80 na msosi bule kama magereza yataboreshwa kama hongkong

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli bwan afadhari uende ukajifungie huko hong Kong kwenye maandamano yasiyo na kikomo
 
Tukifanya gerezani kama Brazil vijana watafanya uhalifu kupelekwa huko.
Ajira mtaani hakuna, alafu mtu aambiwe aende gerezani na atafanya kazi na kulipwa.

Si balaa hiii
 
WAPO WALIOFUNGWA HONG KONG NA HAWATAKI WARUDISHWE KWENYE NCHI ZAO.

Father John ametusogezea siri kuwa kuna baadhi ya wafungwa ambao wapo kwenye magereza ya Hong Kong na hawataki kurudi nchini kwao kutokana na Magereza ya kule yalivyo.

“Magereza ya Hong Kong yapo vizuri yaani kwenye Chakula, makazi na mavazi vinatolewa bure lakini ukienda kwenye nchi nyingine kidogo ni shida familia ndiyo inabidi kulipia.

Hong Kong kuna wafungwa ambao wanafanya shughuli mbalimbali wakiwa gerezani na wanajipatia kipato cha kutuma kwa familia zao na wengine wanaingiza dolla 80 kwa mwezi na zaidi na wanasema kipato wanachokipata ni kikubwa kuliko wanachokipata wakiwa nchini kwao” - Father John, PowerBreakFast

Sent from toyota Allex
hiyo device balaaa-toyota Allex
 
Magereza hutofautiana kulingana na uchumi wa nchi. Sasa kama kibarua wa kiwandani tanzania anapokea buku tano kwa kutwa sawa na usd 2 ambayo sawa na usd60 kwa mwezi kwa nini asifungwe tu akapokekea usd80 na msosi bule kama magereza yataboreshwa kama hongkong

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata sisi tungeweza kuleta mapinduzi ya Magereza jambo kubwa ambalo tunatakiwa kuwa nalo ni mind set yetu ibadilike kwanza, wafungwa wafanye kazi ya kuzalisha mali halafu wapewe posho kutoka kwenye mazao ya kazi zao
 
Back
Top Bottom