Kwanini serikali inawavumilia wenye kuhubiri "umwagikaji damu" au inawaogopa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini serikali inawavumilia wenye kuhubiri "umwagikaji damu" au inawaogopa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 10, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  • Asema wanajaribu kutumia ngazi ya maiti za watu kuingia Ikulu
  • Asisitiza kuwa damu ikianza kumwagika wao watakimbilia Ulaya
  • Awashutumu ‘wanaochonga' kuwa Tanzania haijapata maendeleo tangu uhuru

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amewaonya Watanzania kuwakataa wanasiasa wanaohubiri umwagaji damu nchini kwa nia ya kutumia maiti za watu kama ngazi ya kwenda Ikulu.

  Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa umwagaji damu ni jambo lenye maslahi tu kwa wanasiasa ambao damu itakapoanza kumwagika watapanda ndege kukimbilia zao Ulaya.


  Vile vile, Rais Kikwete amewashutumu wanasiasa wanaotumia uongo katika kampeni za sasa za Uchaguzi Mkuu katika kupindisha mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa CCM akiwaita wanasiasa hao "watu wazima ovyo".


  Akihutubia mkutano mkubwa na uliochangamka wa kampeni kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea jioni ya leo, Jumapili, Oktoba 10, 2010, Rais Kikwete amewasuta ipasavyo wanasiasa ambao wamekuwa wanatishia umwagaji wa damu nchi kama hawakufanikiwa kushika nafasi za uongozi wanazozitaka.


  "Sisi ni CCM. Sisi ni chama kisichohubiri umwagaji damu. Sisi ni chama cha amani. Umwagaji damu hauna maslahi yoyote na wala tija kwa yoyote isipokuwa kwa wanasiasa wanaotaka kutumia maiti za watu kama ngazi ya kuingilia Ikulu," amesema Rais Kikwete na kuongeza:


  "Hawa siyo watu. Hawana maana yoyote. Achaneni nao watu wa namna hii wanaotaka kupata madaraka kwa ngazi ya maiti za wananchi wasiokuwa na hatia."


  Amesisitiza Rais Kikwete: "Wanachochea watu wamwage damu na wao wapande ndege kwenda zao Ulaya na kuwaachia nyie mkitoana damu."


  Viongozi wa Chama cha CHADEMA, na hasa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamekuwa wakihubiri umwagaji damu nchini endapo chama hicho kitashindwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.


  Kuhusu madai ya uongo ambayo yamekuwa yanasambazwa na wanasiasa kuwa hakuna maendeleo yoyote ya maana yaliyopatikana Tanzania tokea uhuru mwaka 1961, Rais Kikwete amewaambia maelfu ya wananchi hao kwenye Uwanja wa Majimaji:


  "Wanapitapita.. wakichonga sana kuwa hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana tokea uhuru wetu. Kwa nini watu wanakuwa waongo kiasi hiki…watu wazima ovyo"


  Amesema kuwa ukweli utabakia pale pale hata kama wengine hawataki kuukubali kuwa CCM imeongoza Tanzania vizuri na chama hicho kimekuwa mbegu iliyozaa vyama vingine vyote vya siasa nchini. "Hiki ni chama imara, chama dume, dume la mbegu. Mbegu yetu ndiyo imezaa CHADEMA, ndiyo iliyozaa CUF na vingine vyote."


  Rais Kikwete amewaelezea wana-Songea mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka mitano iliyopita ya uongozi wake.


  Aidha, Rais Kikwete ametangaza kuwa Serikali itajenga Chuo Kikuu cha Madaktari mjini Songea kwa kushirikiana na Serikali ya Cuba.  --
  Campaign Communications Team
  Kikwete 2010


  My Take:
  Hivi ni kweli wapo wanaohubiri umwagikaji damu nchini na watu hao wanataka kuingia Ikulu. Kwanza mimi binafsi:

  a. Siamini kwamba wapo watu wanaotaka kuingia Ikulu kwa kumwaga damu; ila wapo ambao wanaweza kutaka kubakia Ikulu kwa kumwaga damu

  b. Kama wapo watu wanaohubiri umwagikaji damu na wanataka kuingia Ikulu na Rais wa sasa anajua wapo, usalama wa taifa wanajua wapo ni kutokuwajibika kutowazuia watu hao mara moja.

  c. Wanaopanga umwagikaji damu ndio hao hao ambapo peke yao wana uwezo wa kuuzuia kwa hiyo isije kuwa wanahubiri kile ambacho kinawahusu wenyewe ili watakapomwaga damu ya Watanzania waruke na kusema "siyo sisi ni wao, si tuliwaambia".
   
 2. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka hata Mkombozi Slaa alipoanza kutamka kuhusu ufisadi wa EPA, Kikwete alikataa kata kata kwamba alichokuwa anaongea ni uogo mtupu ila nia yake ni kuanzisha machafuko ili umwagaji wa damu utokee nchini. Sasa kwa kuwa hana hoja ya nguvu anataka kuonyesha Watanzania kwamba Dr Slaa na CHADEMA ni wavunja amani na wanataka kusababisha umwagaji wa damu nchini.

  Itakuwa vizuri kama Watanzania walio wengi wakamshtukia mapema na kutomsikiliza wala kumpa kura zao.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Huyu Mzee hizo ahadi kweli atazitimiza zote? Mbona zinazidi kuwa nyingi kuliko maji ya bahari!
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani nilipata taarifa kutoka kwa rafiki yake na mtoto wa kikwete(miraji) the only option iliyobaki kwa CCM nikutumia propaganda ya umwagaji damu ambayo wameifanyia utafiti na kuona kuwa inaweza kuwanusuru kubakia madarakani. Kijana huyo alinidokeza kuwa mpango huo utakuwa na faida kubwa mbili kwao.

  • Utarahisisha au kuharalisha wizi wa kura, kwa maana kwamba hata wapinzani wakigundua na kugoma, vyombo vya usalama vitatumia kigezo cha wanaotaka kumwaga damu hivyo wananchi wataamini kweli wapinzani walikusudia kumwaga damu.

  • Wananchi wengi wataogopa kupiga kura na watakaopiga watapigia CCM kwa maana ni chama kisichotaka kumwaga Damu.
  Mpango huu huko well coordinated.
  My take
  Tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu walioko hasa vijijini na kuwaeleza mpango huu mbaya wa CCM.
  Naamini CHADEMA mnamashushu wenu tafadhari watumieni ili kuzima mpango huu mbaya kabisa wa CCM
   
 5. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa ameagiza jeshi kukamata wote wanaotaka damu imwagwe. Mbona hawajawakamata? Maana yake ni kuwa hawapo!! CHADEMA inahubili amani na utulivu unaotokana na uwepon wa huduma bora za kijamii kama afya, elimu na uwezeshaji wa kiuchumi.

  Jk atajiju na damu anayotaka kumwaga kwa kungangania kubaki madarakani!!
   
 6. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengi mmesema. WANAOTAKA KUMWAGA DAMU NI WAO na wanajua kuwa wataiba kura.
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu Kikwete ina maana hawezi kufanya chochote zaidi ya kuwachafua wenzake. Nafikiri kuna haja ya CHADEMA kuendelea kupeleka mashitaka kwenye mashirika mbalimbali ya kimataifa. Ikiwezekana, kwa hapa tulipofikia kuna haja ya uchaguzi kusimamishwa. Hao waangalizi wanaona hizo message zinazosambazwa kummaliza Slaa? Je wanazisikia kauli hizi zinazotolewa na hawa wehu?

  Kwanini yasifanyike maamuzi magumu? Tuugomee uchaguzi kama vipi!!
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa anawaza zile damu za watu wa THAILAND waliomkataa Mkuu wa nchi labda.....style yao ni UNIQUE...anahisi CHADEMA wata adapt
   
 9. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280


  • Mwanakijiji,
   Hizi zote ni kampeni. Na wala husidanganyike kwamba kampeni au siasa ni mchezo msafi hata siku moja. Vitisho, majigambo, uongo, kuchafuana ndio kampeni. Wakati wa kampeni Obama aliitwa Osama, jina lake la katikati likahusishwa na marehemu Saddam, akaambiwa ni mvuta sigara mkubwa. Bush mtoto akahusishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya.

   Leo hii, Dr Slaa anashutumiwa kuiba mke, Kikwete mgonjwa kifafa, nk. Kadhalika kama CCM wanajuwa mtaji wao ni amani lazima kwenye kampeni watatoa vitisho vya kuvunjika kwa amani endapo hawatapigiwa kura. AS SIMPLE AS SUCH. Ukidhani siasa ni mchezo msafi basi wewe sio mwanasiasa, bora tu uwe paroko au shekhe!
   
 10. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama Slaa alishapita Songea basi kuna haja ya kurudi huko na kuwatoa wasiwasi wananchi hawa waliolishwa sumu hii kali na Kikwete. Na ikibidi sasa ratiba ya Kampeni ya Slaa ibadilishwe awe anapita huko alikopita Kikwete ili kuondoa hiyo sumu.

  CCM wanatakiwa kujuwa kuwa amani na utulivu tulionao Tanzania ni neema ya MUNGU kwa watu wa Tanzania. Ametupa mioyo ya utulivu na uvumilivu na si wao (CCM) kama wanavyodai. Maana kama watanzania wasingekuwa wavumilivu haya maovu wanaotutendea CCM mfano kuwachekea mafisadi na kuwatetea hadharani na kuuza maliasili za nchi zetu kwa wageni basi wangeweza kubeba mapanga na kusema hatuwataki hawa wawekezaji wanyonyaji.
   
 11. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Luteni Kanali mshindwa Jakaya Halfani Mrisho Kikwete hafai kuwa Rais wa nchi yeyote duniani. Hana uwezo huo,hana sera, hana kichwa cha uongozi, hana uwezo wa kuongoza, ni mbabaishaji, mshirikina, mwingi wa habari, mnafki, muongo, katili, mlipiza visasi, mahututi, fisadi na mfuasi wa ibilisi.
   
 12. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni mbele kwa mbele mpaka kieleweke..JK anatumia mbinu dhaifu mnoo..yaani CHADEMA tumiene huu udhaifu wao kuwamaliza kabisaaaa..
   
 13. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hizi zooooooote ni sifa zake JK. Haiingii akilini kumchagua mtu anayesema eti EL ni msafi, Mramba ni msafi, RA ni msafi. Huyu hana maadili ya uongozi hata kidogo. Mnakumbuka alisema tena kwa kuonyesha seriouness kabisa kuwa hakuna mkataba wa madini utakaosainiwa kabla ya marekebisho ya sheria ya madini, lakini baada ya siku chache tu swahiba wake Karamagi akasaini mkataba wa Buzwagi gizani huko UK na hakumfanya kitu. Huyu Kikwete ameuza madini yetu kwa rafiki yake Sinclair (spelling sijui kama ni sahihi) and the co., RA mwizi wa uchumi wetu na rafiki zake akina Somaia ndo maana anasema elimu bure haiwekani kwani anajua kuwa uchumi uko mikononi mwa mafisadi asioweza kufanya kitu.
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  hii kauli ysake ya umwagaji damu na ile msg inayomzungumzia dr Slaa kuwa anataka kumwaga damu zina uhusiano sana, nadhani hawa ndio walioziandika
   
 15. Y

  YgJunior Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mbona malaria sugu hachangii kwenye mada kama hizi
   
 16. M

  Mundu JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  CCM wana uhakika kuwa, katika njia zote za kawaida watashindwa katika uchaguzi huu. Na njia pekee waliyonayo ni kuwatisha watanzania kwamba Dr. Slaa anataka kumwaga damu.

  Watanzania wengi hata wa vijijini wameshagundua kuwa hiyo ni danganya toto; na wengi watapigia vyama vya upinzani October 31. Na tushishangae, TV zetu zikaanza kuonyesha mauaji yaliyotokea katika nchi jirani, ili kuzidi kutisha watanzania kuwa, nchi hii ikichukuliwa na Chadema au CUF, damu itamwagika. Wapii, Wapiii, Wapiiii. Na hata CCM wakiamua kumwaga damu hata hao wanaijiita kuwa ni wana CCM hawatapona! Kwakuwa CCM ya sasa haina mwenyewe.

  Watanzania, wakiamua kuikataa CCM wanaweza!!
   
 17. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Zile message za vitisho kutoka Finland zina ujumbe kama alioutoa JK Songea, ina maana anazisambaza yeye nini?? Wadau hebu fungueni macho...
   
 18. M

  Masauni JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi propaganda ni za kikwete, na kama nilivyosema hapo juu that is only option kwa CCM kujaribu kubaki madarakani.
   
 19. K

  Kaka Joe Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamani jamani tusiseme sana na kuumiza vichwa bureeeee,wait and see the game as who win and who lose the tutakuja jionea Yale yoooote yaliyokuwa yanasemwa semwa ili tuje prove Kama ni kweli au yalikuwa ni ya uongo na uzushi fo several dirt reasons.
   
 20. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  anasambaza mwanae anaeitwa Miraji Kikwete kwa kushirikiana na wataalam fulani wa IT.
   
Loading...