msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Kuna kitu hakipo sawa kwenye ajira za walimu.
Kwenye kila kibali cha ajira kinachotoka idadi ya walimu wenye shahada wapatao fursa ya kuajiriwa serikalini huwa ni ndogo sana kulinganisha na walimu wa ngazi zingine za kielimu kama vile cheti na diploma.
Kielelezo kizuri ni ajira zilizotoka juzi ukizichunguza kwa makini utakubaliana na hiki ninachokisema.
Kwani katika hizo ajira, wenye shahada walioajiriwa hawafiki hata robo ya waajiriwa wote(wapo chini ya 1500 kati ya 8000).
Tukumbuke asilimia kubwa ya walimu hawa wamesomeshwa na serikali hivyo wanadaiwa na bodi ya mikopo(HESLB). Lakini cha kushangaza serikali ni kama inatoa kipaumbele kidogo kwa wao kuajiriwa.
Je, ni kipi hasa kinafanya walimu hao waajiriwe kwa uchache kuliko walimu wengine?
Je, watalipaje madeni yao ya mikopo kama serikali itaendelea kuwaacha mitaani?