Kwanini serikali inatoa pesa kwa ATC!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini serikali inatoa pesa kwa ATC!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamundu, May 31, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Je ni kwa nini serikali inatoa pesa kwa ATC? Kazi ya serikali haitakiwi kuwa kuendesha kampuni ya ndege badala yake serikali ingetakiwa kuzitumia pesa kwa mambo mengine ya manufaa ya nchi. ATC ni hasara kubwa na inatakiwa kuachiwa kufa inawafanyakazi wengi sana na ndege mbili tu za kukodi!! na ndiyo maana haiwezi kufanikiwa hata kidogo.
  Serikali kama inataka kukuza na kuhimarisha usafirishaji wa anga basi iachie kampuni za binafsi na kuruhusu kampuni ndogo kuja kuwekeza kwenye hii secta. Kuna kampuni ndogo nyingi sana duniani zingependa kuwekeza kwenye secta ya anga lakini inatakiwa kuwe na mazingira mazuri ya uwekezaji. Sio lazima tatizo la usafiri wa anga kutatuliwa na serikali kwani mabasi ni mfano mzuri sana kuna watu binafsi wengi wenye mabasi na ndiyo yanayofanya ushindani uwepo na bei kupungua.

  Angalia hii kali kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya bunge.

  “Shirika la Ndege lenyewe linahitaji sh bilioni 23 ambazo ni lazima serikali iziweke. Pia Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo anatakiwa kutoa sh bilioni moja kwa ajili ya kulipia deni la ndege iliyo nchini Afrika Kusini,” alisema Serukamba.
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa nini watu wanapendekeza kutupa fedha zaidi? ATC kama shirika la uma tayari limekufa. Lizikwe kwa amani!
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ilikuwaje iingie ubia na South African 2002 badala ya ile kampuni ya Republic ya Ireland? ok waliamini makaburu watatubeba zaidi? ndege ndogo zina bei ya gari tena wanashindwa kununua? hata za kukodi ni mbovu, kampuni ya nini? nakubali hoja
   
Loading...