COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,600
- 3,648
Serikali na jeshi lake la polisi wamekuwa wakitumia kigezo cha kuzuia wananchi wenye hasira kujichukulia sheria mkononi. Hoja hii imekuwa ikiwapa jeuri vibaka na wahalifu mbalimbali nchini kufanya wizi wa mali za wananchi wanaohangaika kujikwamua kiuchumi.
Utakuta mtaani vibaka wanawaibia watu, mkimkamata na kumpeleka polisi baada ya wiki mbili au mwezi wanamuachia anarudi tena mtaani na kutamba kuwa hakuna wa kumkomesha. Anarudia tena kuiba, kujeruhi wananchi; mkimkamata tena na kumpeleka polisi wembe ni uleule, huyo kibaka/ mhalifu ataachiwa tu.
Sasa wananchi wanapokuwa wamechoka, wanakuwa wapole, huyo kibaka akirudi mtaani na kuendelea kuiba siku atakapokamatwa na wananchi kinachofuatia ni kibaka huyo kupokea mkong'oto wa nguvu na hata kuchomwa moto. Hapo ndiyo kihoja kinapokuja; utakuta jeshi la polisi wanawasaka wananchi walioshiriki kutoa huo mkong'oto na kumtia kiberiti huyo kibaka kisa eti " wananchi wamejichukulia sheria mkononi".
Hapo hadi mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa utamsikia akikemea tabia ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Swali: hao viongozi na jeshi la polisi wao wapo kutetea wahalifu? Mbona hatusikii wakikemea tabia mbaya wanayofanya hao vibaka/wahalifu?
My take: serikali na jeshi la polisi acheni kutetea vibaka na wahalifu, wanaturudisha nyuma kimaendeleo.