Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
KWANINI SERIKALI INAOGOPA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA?
By Malisa GJ,
Jumamosi April 15 mwaka huu umoja wa kizazi cha kuhoji nchini (UTG) ulifanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea juu ya matukio mbalimbali ya watu kupotea, kutekwa na wengine kuuawa. Katika mkutano huo tulieleza baadhi ya hatua tulizochukua kuhusu hali hii ya kuogofya inayoendelea nchini kwa sasa.
Moja ya hatua hizo ni uongozi wa UTG kukaa mezani na uongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC) kuomba kituo hicho kupeleka malalamiko rasmi Umoja wa mataifa (UN) juu ya matukio ya watanzania kupotea, kutekwa na kuuawa.
Tuliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa kituo hicho Dr.Hellen Kijo Bisimba ambaye alishiriki mkutano wa umoja wa mataifa wa taasisi za kiraia zinazoshughulika na masuala haki za binadamu ambapo aliweza kupenyeza hoja kuhusu watanzania kupotea katika mazingira ya kutatanisha akihusisha suala la Ben Saanane ambaye ni Katibu Mkuu wa UTG Tanzania.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo Umoja wa mataifa ulimtaka Dr.Kijo kuwasilisha kwa maandishi malalamimo hayo ili waweze kutuma wataalamu wake kuja kuchunguza. Ieleweke kwamba Umoja wa mataifa una chombo huru cha uchunguzi kiitwacho "The Observer" na kina uwezo wa kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi yoyote mwanachama (Tanzania ikiwemo).
Hivyo basi UTG tulishirikiana na LHRC kuhakikisha kuwa barua hiyo inaandikwa na kufika katika utaratibu rasmi ili waweze kutuma wataalamu hao kuja kuchunguza. Tayari barua hiyo imeshaandikwa na tunasubiri majibu.
Dhumuni la kufanya hivyo ni kwa sababu hatujaridhishwa na utendaji wa vyombo vyetu vya ndani. Tunaamini vyombo vya kimataifa vinaweza kuwa huru zaidi kuchunguza mambo haya ya watanzania kupotea, kutekwa na kuuawa bila hatia.
Leo kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe.Freeman Mbowe ameonesha dhamira ileile iliyooneshwa juzi na UTG ya kukosa imani na vyombo vyetu vya ndani. Mhe.Mbowe ameomba serikali iruhusu makachero wa Uingereza maarufu kama "Scottland Yard" waje nchini kufanya upelelezi kuhusiana na matukio ya watanzania kupotea, na Mbowe amekua specific kwa Ben Saanane.
Lakini katika hali ya kushangaza Waziri Mkuu amejibu swali la Mbowe kwa majibu mepesi mno. Amesema vyombo vyetu vya usalama vinaendelea na uchunguzi. Katika kuonesha hakubaliani na kuja kwa vyombo vya kimataifa Waziri Mkuu amesema kwa sasa tuviachie vyombo vyetu vya ndani na serikali ikiona kuna haja ya kuita vyombo vya nje basi itafanya hivyo.
Maana yake ni Kwamba Waziri mkuu hadi sasa haoni haja ya kuita vyombo vya nje. Bado anaamini vyombo vyetu vya ndani vinaweza kuchunguza. Mi nadhani Mheshimiwa Waziri Mkuu anapaswa kutafakari upya. Huu sasa ni mwezi wa 6 tangu Ben apotee serikali inasema bado inaendelea na uchunguzi. Kweli?
Hivi waziri mkuu anajua kwamba katika miezi yote 6 hivyo vyombo anavyovitaja vimeshindwa kukamata hata mshukiwa wa suala la Ben, Vimeshindwa kutrace hata simu moja kati ya simu zilizompigia Ben mwishoni, Vimeshindwa kumhoji hata mwandishi aliyesema Ben anaonekana mtaani, vimeshindwa kufuatilia hata mtu aliyefuta baadhi ya post za Ben kwenye ukurasa wake wa facebook (zilizokua zikihoji PhD ya JPM). Hivi ndio vyombo ambavyo Waziri mkuu anasema tuendelee kuviamini.
Hivi Wairi Mkuu najua kwamba yombo hivyo anavyosema tuviamini vimetuhumiwa hadi bungeni kuhusika na njama za utekaji na utesaji? Waziri Mkuu anajua kamba Wabunge wake wa CCM akiwemo Mhe.Bashe wamevituhumu vyombo hivyo waziwazi kuwa vinahusika na kuteka raia wasio na hatia na kuwatesa hata kuwapoteza?
Sasa ikiwa tuhuma za kina Bashe ni za kweli, Waziri mkuu anapata wapi moral authority ya kutuambia tuendelee kuviamini vyombo hivyo? Kama vyombo hivyo vinatuhumiwa kuteka raia, vinawezaje kujichunguza vyenyewe na vikaleta ripoti ambayo tutaiamini?
Kanuni za msingi za sheria zinazuia mtu/taasisi/chombo kuwa hakimu wa kesi yake yenyewe (Nemo judex in causa sua). Sasa kwanini Waziri mkuu anatushinikiza tuviamini vyombo hivyohivyo vinavyotuhumiwa? Yani chombo kinatuhumiwa kuteka watu, halafu chombo hichohicho kinapewa kazi ya kuchunguza watekaji. What do u expect??
Hata kama tuhuma hizo si za kweli lakini kitendo cha kutuhumiwa tu kinavindolea vyombo hivyo sifa ya kuendelea na uchunguzi.
Kwanini Waziri Mkuu asiruhusu vyombo vya kimataifa vije kuchumguza ambavyo tunaamini vitakua fair and objective zaidi kuliko hivi vya ndani vyenye tuhuma lukuki?
Maazimio ya UTG ni uchunguzi wa madai ya watu kutekwa/kupotea/kuuawa yafanywe na vyombo vya kimataifa. Na tayari UTG kwa kushirikisna na LHRC wameshaandika barua Umoja wa mataifa kuomba wachunguzi hao. Leo mheshimiwa Mbowe naye kaomba makachero wa Uingereza waje kuchunguza. Lakini majibu ya Waziri mkuu yanaonesha serikali haipo tayari kwa wachunguzi hao. Swali la msingi ni kwanini serikali inaogopa wachunguzi wa kimataifa?
Malisa GJ