Kwanini Serikali inaleta siasa kwenye hela za mafao?

Sababu kuu ni kwamba mifuko hiyo iko hoi.

Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu.

Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara. Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake.

Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo.

Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. "You can rest assured" haitarudi hata senti moja.

Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika.

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja. Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani.

Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao. Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa.

Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.

By Tundu Lissu
Wamepeleka hela ktk kampeni
 
Wafanyakazi wanaofukuzwa kazi au mikataba kuisha.. hawalipwi Pesa zao.

NSSF wamepeleka wapi akiba zao?

Ndio hizo CCM wamejaza Mabango barabarani?
 
TUCTA Ni wachumia tumbo

Nssf hawana Pesa... Magufuli amefilisi hii mifuko

Rudisha Fao la kujitoa

CCM mnaonea Watanzania

CCM sio ya kuchagua....
 
*VIUMBE KARIBA YA MAGUFULI WANAKUJA KWA NADRA SANA, WAKIONDOKA MNASUGUA SANA KUWAPATA TENA.*

Na Bwanku M Bwanku

Mwanamama Mchumi wa Zambia Dambisa Moyo aliyepata kufanya kazi Benki ya Dunia (WB) na kupata tuzo mbalimbali za uandishi wa masuala ya kiuchumi na anayeheshimika kote duniani, ameeleza kwenye kitabu chake alichokiita Dead Aid kwamba matatizo makubwa ya kiuchumi yanayolikumba bara la Afrika ni matokeo ya tatizo la kiuongozi ambao umekuwa ukigharimu bara la Afrika miaka kwa miaka.

Mwanamama Dambisa anasema Afrika licha ya kuathirika na mifumo ya ulimwengu ya kibepari na ubeberu uliojaa unyonyaji ambayo inailazimisha Afrika kukopa sana mikopo ya nje inayowaingiza kwenye mizigo ya madeni (Debt burden) lakini suala la uongozi makini na madhubuti unaopambana na ufisadi, wenye maono ya mbali na wenye misimamo thabiti ni stori isiyoisha kwa Afrika.

Dambisa anasema ili Afrika ijiondoe kwenye minyonyoro hii ipo haja ya Afrika yenyewe kuimarisha mifumo yake ya kiuongozi hasa kuwa na kariba ya viongozi mashujaa, wenye misimamo isiyoyumba na kutetereka, makini, wanaopinga rushwa na watakaotengeneza mifumo ya Afrika kujitegemea hasa kwa kupiga vita ufisadi, rushwa na kuimarisha aina ya uongozi wake utakaowekeza na kuwezesha Afrika kukwepa mnyonyoro wa utegemezi wa mikopo ya nje ambayo kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu imekuwa ikiigharimu Afrika kwa kuiingiza kwenye misaada na mikopo inayoiumiza Afrika aliyoiita 'Dead Aid.'

Mawazo yale aliyoyaota na kuyaeleza Mchumi huyu wa dunia na anayehishimika kote duniani, kwa miaka mitano tu ya uongozi wa Dkt John Pombe Magufuli kuliongoza Taifa la Tanzania inashuhudia mapinduzi makubwa ya kiuongozi na mifumo iliyoshindikana miaka kwa miaka ili kuleta ukombozi wa kiuchumi.

Toka kuingia madarakani kwa Rais Magufuli kumeitoa kimasomaso Afrika na dunia nzima kwa ujumla kwa kushuhudia na kupata mtoto wa kweli wa Afrika aliyekubali kujitoa sadaka na kafara, aliyekubali kufa, aliyekubali kubaki pekee yake na mengine mengi ili kupigania maslahi ya ndugu zake weusi wa Afrika.

Baada ya kuwasoma mashujaa wengi waliolipigania bara la Afrika akina Mwalimu Nyerere, Kwame Nkrumah, Mandela na wengine wengi, Rais Magufuli anaibuka katikati na kuwa moja ya mashujaa wakubwa wa kizazi hiki cha kisasa cha Afrika hasa kwa misimamo yake linapokuja suala la maslahi ya nchi na kupambana na makampuni makubwa na nchi korofi za nje zilizozoea kunyonya mataifa ya Afrika.

Rais aliyejitoa muhanga kupambana na makampuni makubwa na mapapa kwenye sekta ya madini kama Barrick, waliokuwa wanaiba madini pale Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara miaka kwa miaka, yeye akasema hapana ni lazima madini yafaidishe Watanzania wa kawaida kwa umiliki na kuruhusu na kutenga maeneo ya wachimbaji wadogo.

Ni rahisi aliyeonyesha misimamo ya kutisha kwenye kupambana na mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi ambao wana mikono mirefu na mtandao mkubwa, mrefu na mpana sana. Leo husikii tena habari za ufisadi Tanzania. Rais aliyechomoa maelfu kwa maelfu ya watumishi hewa na feki waliokuwa wanaliingiza Taifa kwenye hasara ya mabilioni kwa mabilioni kila sekunde.

Nenda kwenye nidhamu ya watumishi wa umma. Hakuna anayeenda kunywa chai masaa 8 sasahivi. Hakuna lugha za hovyo na kuudhi zilizokuwa zinatoka kwenye vinywa vya manesi, madaktari na watumishi wengi sana kwenye ofisi za umma pindi mama zetu na Watanzania mbalimbali walipoenda kupata huduma. Amenyoosha na kukomesha kila aina ya mifumo mibovu, ya hovyo na iliyokuwa inawaamuza mno wananchi wa kawaida wa chini wasio na sauti. Ni Rais halisi wa wanyonge aliyejitoa kwa maneno na vitendo vyake kulinda maslahi ya watu wa chini. Akina kapuku walionyanyasika sana.

Rais aina ya Magufuli wanakuja mara chache sana kwenye uso wa dunia. Mataifa ya wenzetu watu kama Magufuli huachwa watawale mpaka wachoke na mataifa hayo hukataa kuingia mkenge wa demokrasia laana. Urusi na Vladimir Putin wao wamefanya hivyo, China pia wamempa Xi Jinping kutawala mpaka afe na majirani zetu Rwanda wamefanya hivyo.

Yako mataifa yanamlilia Rais Magufuli, wanatamani angekuwa wa kwao asimamie na kuonyesha njia. Rais mwenye maono, asiyeyumba na aliye tayali kusimama kidete kwa maslahi ya wengi. Fikiria Afrika ingekuwa na Marais kariba ya Magufuli, wenye misimamo, vitendo, maono, wachamungu, wazalendo na wa wote, Afrika ingekuwa wapi? Haya mataifa ya nje na makampuni yao yanayoibagaza Afrika na kulifanya shamba la bibi kwa kuvuna kila wanachokitaka wangepata upenyo huo?

Tumtunze, tumlinde na tuzidi kumpa moyo na kumuombea sana Rais Magufuli, huu ni mpango wa Mungu Tanzania. Mungu ana makusudio na Tanzania. Narudia viongozi aina ya Magufuli wanakuja kwa nadra sana na wakipotea mnaweza kusugua sana kuja kuwapata tena.
 
Kwa Nini CCM wanaleta ulaghai kwenye maisha ya watu?

FAO la kujitoa Ni lazima lirudishwe...Pesa sio za Rais, au Ndugai...Ni fedha za wananchi
 
Hakuna kitu kizuri kama kuongea kitu kwa Mfano halisi.

Watanzania ifike mahala tujifunze kuappreciate vitu vyenye manufaa kwetu.

Hakuna haja yakubeza vitu wakati ukweli unaujua na unaujua vina manufaa kwetu
 
Una maana FAO la kujitoa Ni Haki ya wafanyakazi?

Sasa kwa Nini Magufuli aliondoa FAO la kujitoa kwa kutunga Sheria na kusaini Sheria ya kufuta FAO la kujitoa?

Pesa za mafao Ni za wafanyakazi au Ni pesa za Serikali?
 
Hii story yako ina uhusiano gani na hela za mafao ya kustaafu ya wafanyakazi?

Jipige dole ukimaliza nusa then jipige kifuani mara 3 ukisema kwa sauti mimi ni takataka.
 
Back
Top Bottom