Kwanini Serikali ina kigugumizi kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Nimebaini kwamba hakuna Serikali, chama au kiongozi anayeweza kuijenga nchi, kuleta maendeleo ya nchi au kufanya mambo makubwa ya wananchi akiwa peke yake. Dhana ya ushirikishwaji wananchi ni dhana ambayo ina mifano mingi na watu wengi ikiwemo nchi na vyama vimenufaika sana.

1. Sera ya Elimu bure yaweza kukwamisha serikali maana haijaeleweka ipasavyo na hakuna mipaka iliyowekwa wazi na serikali kuhusu ushiriki wa wananchi katika dhana ya Elimu bure. Kuhamasishwa ujenzi wa madarasa kunaweza kufanya wengine wajitokeze na kusema Elimu bure ni pamoja na serikali au chama kuwatafutia wananchi madarasa ya kusomea.

2. Ushiriki wa chama kimoja katika siasa na kiuongozi kwaweza kwamisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa. Ni dhahiri kuwa viongozi wa vyama mbali mbali na wengine hujitokeza na kuwaomba wananchi washiriki tukizingatia wengi wako upande upi na wachache wapo upande upi.

Kuna haja ya serikali kujifunza kwa awamu hii na kurekebisha makosa yote yaliyojitokeza kuwa hayatajirudia tena, nafahamu chama tawala na kiongozi wa nchi atakuwa na muda mgumu sana sana kuiongoza nchi.
 
Elimu bure means elimu bure 100%, Nothing less nothing more. Serikali ijenge madarasa. Iache visingizio
 
Elimu bure ni bure tu
Hayo ndio madhara ya kukaa madarakani bila ridhaa ya wananchi. Ccm wanajua fika matokeo ya uchaguzi, hayakuwa upande wao, hata kama walioongoza kwa ushindi, ila sio kwa idadi waliyotangazwa. Hivyo hawathubutu kuhamasisha wananchi kushiriki ujenzi wa madarasa, maana wanajua hisia za watu zitaonekana dhidi yao.
 
Back
Top Bottom