Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 20,517
- 30,576
Inashangaza sanaKama sikosei, mpaka sasa Rais Samia keshaongea na waandishi wa habari kama mara mbili hivi.
Ni zaidi ya mwezi sasa tokea alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari/ waandishi wa habari toka ikulu ya Dar es Salaam.
Wiki moja au mbili zilizopita, akafanya mahojiano na Salim Kikeke wa BBC.
Katika nyakati zote hizo mbili, sikusikia kabisa akiulizwa ni kwa nini serikali yake ilituficha kuhusu kuugua kwa Rais Magufuli.
Wananchi hatukupata taarifa zozote zile zilizo rasmi hadi tukaishia kutegemea habari umbea na zisizo rasmi kupitia mitandao ya kijamii.
Kimya kilipozidi kutanda, tukaanza kudokezwa dokezwa kuwa hali si nzuri, mara sijui yupo anachapa kazi, mara sijui anafanywa nini…
Haikupendeza hata kidogo. Na hata vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti kuhusu tetesi za kutoonekana kwa Magufuli.
Kwangu hili halikubaliki kabisa!
Wananchi kama waajiri wa hawa viongozi wetu, tuna haki ya kujua kuhusu afya za viongozi wetu.
Hapa simaanishi kila kitu kuhusu afya. Namaanisha tu ile kwa ujumla wake.
Kama mtu anaumwa, kalazwa, tuna haki ya kujua.
Mambo ya kuficha/ kufichwa halafu mnakuja tu kuambiwa mtu kaaga dunia, hayafai.
Hivyo, ningependa sana kujua kwa nini wananchi hatukupewa taarifa.
Na itokeapo fursa ingine ya Rais Samia au hata waziri mkuu Majaliwa kuongea na waandishi wa habari, ningependa kuona na kusikia wakiulizwa ni kwa nini hawakutufahamisha kilichokuwa kinaendelea.
Pascal Mayalla take note and spread the word.