Kwanini Serikali ilimpuuza Zitto Kabwe wakati hoja zake zina mashiko?

Adrian Stepp

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
2,764
2,581
Huenda serikali ingelichukulia kwa makini hoja za ZZK pengine tusingefika tulipofika juu ya sakata la Korosho.

Tatizo ni ZZK, Chama Anachotoka ama Hoja zake? Maslahi ya taifa yanapewa kipaumbele kwa kiasi gani? Uzalendo tunaoimba ni kweli unatoka rohoni?

Bandiko hili niliandika February 14, Mwaka huu!

February 10,2018 Mh.Zitto kupitia ukurasa wake wa kijamii wa facebook alikuja kutoa mrejesho wa kilichokua kinajadiliwa bungeni (Feb,9) ambapo bunge lilikua likijadili taarifa ya mwaka ya kamati ya Bunge ya Ulinzi , Usalama na mambo ya nje!
Hoja yake kuu akipendekeza kufumuliwa kwa sheria ilioanzisha Taasisi yetu ya ujasusi (Rejea kurasa yake).

Hoja yake huenda ikawa imechelewa lakini ni nyeti na binafsi niliwahi kutafakari kama huenda baadhi ya viongozi wanaihujumu serikali nakumbuka ilikua September mwaka uliokwisha na nilisita kuileta humu jamvini.
Historia inaonesha kwamba kampuni ya German East Africa (GEAC) mwishoni mwa karne ya 19 ilileta katani nchini kutoka Mexico, Mpaka kufikia mwaka 1961 (Wakati Wa Uhuru) Tanganyika ilikua ya Kwanza duniani kwa uzalishaji na uuzaji Wa katani mikoa Kinara wakati huo ikiwa Kilimanjaro na Tanga.

Mwaka 2012 Tanzania ilitangazwa kua nchi ya 8 duniani na ya 4 Afrika kwa uzalishaji Wa Korosho.
Tanzania ndiyo brand ya pili kwa ukubwa baada ya Brazil katika zao LA Kahawa.

Duniani kote kahawa kutoka Tanzania imepewa jina la Kilimanjaro coffee na kimsingi inakubalika.
Korosho inasafirishwa toka Tanzania Ili kwenda kukobolewa na kua packed nchini India na kwahilo tu India imetengeneza wastani Wa ajira 50,000 kwa mwaka huku ikitajwa kuingiza Fedha nyingi za kigeni (kwa processing & packaging tu)
Kwa maana nyingine ni kwamba Kilimanjaro na Tanga pekee inauwezo Wa kulifanya taifa kua Kinara (Namba 1) duniani kwa kilimo cha katani huku Lindi na Mtwara zikiwa na uwezo Wa kulifanya taifa kua juu ya nafasi ya 8 kwa soko LA korosho pekee ( Ukiachilia mbali hujuma za hivi karibuni kwamba mawe yamegundulika kwenye korosho zetu Vietnam)
Maana yake ni kwamba wenye ufahamu Wa brand ndio kusema korosho ni "Apple company " ya Tanzania duniani.

Inakadiriwa kwamba Tanzania INA hekari Mil.44 zenye ubora Wa kilimo na kati ya hizo ni hekarI 14.5 tu ndio zinatumika sasa hatujafika hata nusu ya matumizi ya ardhi ya kilimo.
Kwa mujibu Wa Zitto kufumuliwa kwa sheria inayounda Tiss kutatoa mwanya Wa kuundwa ama kufanyika kwa mapana zaidi shughuli za ujasusi Wa kiuchumi.

Matatizo kama haya ya kubainika kwa mawe kwenye korosho zetu ya ngeweza kuchambuliwa na ikibainika kwamba hujuma za maadui wetu au matatizo ya wakulima wetu na pengine Mh.Rais angeshauriwa namna bora zaidi ya kuchukua hatua.

Majibu ya Mh Mkuchika hayaridhishi..serikali isimpuuze zitto hata hizi kelele za ukosefu wa ajira zisingesikika endapo tukijipanga na kutumia fursa zilizopo effectively.
Hata hivyo wakuu Wa mikoa na viongozi wenye dhamana waache kufanya kazi kwa mazoea na wabuni njia mpya za kutafuta masoko na kuboresha kilimo..
Sitaki kuwaza ama kusema kwamba kuna baadhi ya waliopewa dhamana wana ihujumu serikali LA hasha!

Nini kifanyike? Kujua tatizo ni mwanzo wa jawabu-Jakaya Kikwete!

Wasalaam!
Adrian H.S.Mahundi
 
Unajua siyo fair kama mnatubombard na habari positive za Zito Kabwe lkn mnablock habari zozote zinazojadili upande wa pili, mnafikiri mnamsaidia Zito Kabwe kwa kumlinda lkn ni kinyume chake, acheni watu wajadili kwa uwazi na siyo kufuta Habari ambazo zinaonyesha upande wa pili na kuruhusu zile ambazo zinamuimbia mapambio, watu ni wajinga lkn siyo kwa kiasi hicho, mtaback fire tu!
 
Nchi hii ina viongozi wajinga mno kuliko kawaida, mawazo yote yakitolewa na mpingaji wa Sera za serikali bila kujali ametoa mawazo mbadala mazuri kiasi gani hawatamuelewa kamwe, na hili ndio tatizo litakaloendelea kututafuna huko mbeleni kama mentality za kijinga zisizo na afya kwa nchi zitaendelea kuwapo kwa hawa watawala waliopewa dhamani ya kutawala
 
Hakuna kiumbe anaekubali hadharani kuwa mpinzani wake amemzidi akili na uwezo, hata kama unajua anajua, utamkosoa wakati unajua unakosea.
 
Back
Top Bottom