Kwanini Serikali iliamua kuwadhalilisha na kuwavua nguo uchi wa mnyama viongozi wa CHADEMA walipokuwa Magereza? Wahusika wachukuliwe hatua

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
Kwa kweli nimeshtuka na kusikitika kumsikia Mchungaji Msigwa akidai kwamba yeye na viongozi wenzake waliohukumiwa walivuliwa nguo na kubakishwa uchi wa mnyama walipofikishwa gereza la segerea.

..kama Raisi Magufuli hakubaliani na vitendo hivyo vya udhalilishaji basi anapaswa kuwachukulia hatua wote waliohusika na tukio hilo.
 
..kwa kweli nimeshtuka na kusikitika kumsikia Mchungaji Msigwa akidai kwamba yeye na viongozi wenzake waliohukumiwa walivuliwa nguo na kubakishwa uchi wa mnyama walipofikishwa gereza la segerea.

Usitegemee kuona rais akichukua hatua yoyote pindi ukatili anapofanyiwa mpinzani hasa wa cdm. Hayuko tayari kuona wapinzani wakitendewa haki, inakuwa kama hayo mambo yana baraka zake.
 
..kwa kweli nimeshtuka na kusikitika kumsikia Mchungaji Msigwa akidai kwamba yeye na viongozi wenzake waliohukumiwa walivuliwa nguo na kubakishwa uchi wa mnyama walipofikishwa gereza la segerea.

..kama Raisi Magufuli hakubaliani na vitendo hivyo vya udhalilishaji basi anapaswa kuwachukulia hatua wote waliohusika na tukio hilo.
Nanyie mnakuripukaga sana kwani kila linalozungumzwa linakuwa na ukweli? Nani alivovuliwa akafanywaje? Alivuliwa tu basi akachunguliwa kengele zake nanvigoda akaachwa? Malalamiko mengine ni uongo mtupu.
 
..sina sababu ya kutoamini alichosema Mchungaji Msigwa.

..Msihalalishe haya mambo kwasababu nyinyi ni CCM na wanaodhalilishwa ni CDM.
 
Kuvuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama Ni kawaida na ndio utaratibu uliopo Magereza yote Tanzania uwe kila unapoingia Gerezani uwe mfungwa/mahabusu Ukitoka tu unaporudi/ingia Gerezani lazima uvue nguo zote na ufungue kitabu wapongo waangalie ndio taratibu zingine zifuatwe!!

Hii ni kwa usalama zaidi na mbaya Zaid Magereza yetu hayana vifaa vya kisasa kufanya ukaguzi kwa wafungwa/mahabusu bado wanatumia utaratibu wa mkoloni kabisa!!!

Typed Using KIDOLE
 
Nanyie mnakuripukaga sana kwani kila linalozungumzwa linakuwa na ukweli? Nani alivovuliwa akafanywaje? Alivuliwa tu basi akachunguliwa kengele zake nanvigoda akaachwa? Malalamiko mengine ni uongo mtupu.

tumia vizuri simu yako mkuu
hivi unajua hili sio lalamiko la kwanza ? about two weeks ago kuna vijana wamelalamika pia walivuliwa nguo wakaambiwa wafanye mapenzi kwa lazima

wewe hupati taarifa za mambo yanayoendelea nchini alafu bado unabisha

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
..kwa kweli nimeshtuka na kusikitika kumsikia Mchungaji Msigwa akidai kwamba yeye na viongozi wenzake waliohukumiwa walivuliwa nguo na kubakishwa uchi wa mnyama walipofikishwa gereza la segerea.

..kama Raisi Magufuli hakubaliani na vitendo hivyo vya udhalilishaji basi anapaswa kuwachukulia hatua wote waliohusika na tukio hilo.
Jera siyo paradise braza ukiingia kule treatment ni ileile tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..hakuna aliyesema ni paradiso.

..kinachosikitisha ni ccm na serikali kuungana kuwadhalilisha ndugu zao wa cdm.

..wanajua kabisa mashtaka yale ni ya kubambikia, na kifungo siyo halali. Na juu ya hayo wanawadhalilisha wenzao.
 
Back
Top Bottom