Kwanini serikali hutoa pesa ya kujikimu kwa siku saba tu kwa waajiriwa wapya?

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
494
Mwajiriwa mpya hupewa pesa ya kujikimu kwa siku saba tu! Hivi ni kwa nini? Baada ya siku saba kuisha aishi vipi maana mshahara wa kwanza huchukua hadi wiki tatu baada ya kumalizika kwa siku saba hizo!
 
Magufuli ndoo amepunguza pesa zamani tulikuwa tunalipwa pesa za siku 14 kwanini ulichagua ccm ?
 
Posho za kujikimu zinatolewa kwa majibu wa waraka wa utumishi wa umma siyo maamuzi ya MTU.
 
Sheria na kanuni haki na stahiki za mwajiriwa mpya zilirekeishwa awamu ya 2 ya Jakaya ila kuna baadhi ya taasisi mpaka leo huishi kwa utaratibu wa zamani kwa kulipa posho shku 14, mimi niliajiriwa 2014, nililipwa ya siku 7 tu
 
Mwajiriwa mpya hupewa pesa ya kujikimu kwa siku saba tu! Hivi ni kwa nini? Baada ya siku saba kuisha aishi vipi maana mshahara wa kwanza huchukua hadi wiki tatu baada ya kumalizika kwa siku saba hizo!
kwasababu wanaamini utakukwa umezoea ofisi na tayari umejua mianya ya kukukimu
 
Hapa naona kuna gap kubwa sana la uelewa, kuna kitu kinaitwa subsistance allowance nahisi ni kati ya shilingi 200,000-80,000/- kwa siku, inategemana na wadhifa wako, sasa ukipewa say 80,000/-*7days=560,000/-wakati unasubiri mshahara wako wa kwanza kuna ubaya gani? wakati wewe ulikua hauna kazi na nauli yenyewe ya daladala ya kwenda kwenye interview ulikopa
 
Mwajiriwa mpya hupewa pesa ya kujikimu kwa siku saba tu! Hivi ni kwa nini? Baada ya siku saba kuisha aishi vipi maana mshahara wa kwanza huchukua hadi wiki tatu baada ya kumalizika kwa siku saba hizo!
Mbona mkuu unalalamika hela za kujikimu hazitoshi kwan umeajiriwa karibuni?, maana sasa wahitimu wanaisoma no ww unahangaika na hela za kujikimu
 
Waliositishiwa Ajira zao June walipewa za siku 7, 80*7 mjn, 70*7 wilayan!

Sasa subrin fungulia dog(Ajira) zijazo hata hizo yawezekana zisiwepo! Mwendo kubana matumiz, mpaka vijana mtie adabu!
 
Hela ya kujikimu!!!!!!!!!!!!!!!
Huyu jamaa kashapata ajira mpaka anazungumzia hela kujikimu.
 
Ajira zenyewe zipo wapi?

Back
Top Bottom