Kwanini serikali hupeleka kesi kwenye mahakama zisizokuwa na uwezo wa kuzisikiliza?

Gogle

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
1,495
867
Habari zenu wakuu,

Mara nyingi nimesikia kwenye habari
"Hakimu amemtaka mshtakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo".

Sasa najiuliza kwanini serikali imepeleka kesi hiyo kwenye mahakama isiyo na mamlaka nayo. Je hawakujua kwamba mahakama waliyoipelekea kesi haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo?

Kama hivyo ndivyo taratibu zinavyoelekeza, je ni kwanini iwe hivyo? Hakuna haja ya kurekebisha taratibu hizo za kisheria ili kesi zipelekwe moja kwa moja kwenye mahakama zenye mamlaka nazo?

Naomba wajuzi wa sheria wanijuze.
 
Briefly & roughly, kisheria baadhi ya mahakama zimepewa mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi kwenye kesi fulani na baadhi ya mahakama kutosikiliza na kutolea uamuzi kwenye kesi fulani. Hiki kitu kisheria wanaita "Jurisdiction "

Jurisdiction ipo kwenye mashauri yote ya madai na jinai. Nitajikita kwenye jinai kwa kuwa umetaja serikali(Jamhuri).

Kama ilivyo kwenye mashauri ya madai, jurisdiction kwenye jinai inaathiriwa na kiasi cha thamani ya fedha kinachohusika kwenye kesi (kosa) mfano kama ni uhujumu uchumi au utakatishaji fedha labda alihujumu au kutakatisha thamani ya sh. billioni moja au millioni 10); aina ya jinai ya kosa linalohusika, etc.

Kesi ya jinai inaweza ikafunguliwa na kusikilizwa kwenye Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi au kusikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania kutegemea na aina na thamani ya kosa.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Cap. 20, R.E. 2002] kuna kesi (makosa) ambazo mahakama za chini ya Mahakama Kuu ya Tanzania (subordinate courts) hazina uwezo wa kuzisikiliza na kutolea maamuzi. Sheria inaelekeza makosa ya namna hiyo yatafunguliwa mahakama hizo za chini halafu upelelezi (ukusanyaji wa ushahidi wa washitaki(jamhuri) hufanyikia hapo na baadae huhamishiwa (hutumwa) Mahakama Kuu kwa ajili ya kesi kusikilizwa na kuamuliwa.

Hapo (mahakama za chini)mtuhumiwa hataulizwa kama anakiri au kutokiri kosa bali atasomewa tu shitaka linalomkabili maana mahakama haina uwezo wa kutolea maamuzi kesi hizo. Hivyo kesi itapelekwa juu Mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika na mtuhumiwa ndo ataulizwa huko kama ametenda kosa au hakutenda kosa analoshitakiwa nalo ili akiri au akane kosa. Kitendo hicho chote kinaitwa "Commital proceeding".

Mfano wa kesi hizo kwa kuzingatia thamani ya fedha inayohusika na/au aina ya kosa ni:

1. Mauaji,
2. Uhujumu uchumi,
3. Utakatishaji fedha
4. Uhaini
Etc. Etc.

Hizi hutumwa Mahakama Kuu ya Tanzania maana ndo ina mamlaka (jurisdiction) ya kuzisikiliza na kutolea uamuzi.

Lengo:
1. kupunguza mlundikano wa kesi Mahakama Kuu, 2. Kuharakisha maamuzi pindi kesi ifikapo huko juu maana upelelezi tayari.
3. Kesi kuweza kupigwa chini na DPP au PP kabla haijaenda Mahakama Kuu kama ushahidi(upelelezi) haueleweki.

4. Etc, Etc.
 
Mambo ya wanasheria haya. Wewe yaache kama yalivyo!

Muone wakili akupe ufafanuzi ili ulipe na ada ya consultation!
 
Briefly & roughly, kisheria baadhi ya mahakama zimepewa mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi kwenye kesi fulani na baadhi ya mahakama kutosikiliza na kutolea uamuzi kwenye kesi fulani. Hiki kitu kisheria wanaita "Jurisdiction "

Jurisdiction ipo kwenye mashauri yote ya madai na jinai. Nitajikita kwenye jinai kwa kuwa umetaja polisi(Jamhuri).

Kama ilivyo kwenye mashauri ya madai, jurisdiction kwenye jinai inaathiriwa na kiasi cha thamani ya fedha kinachohusika kwenye kesi (kosa) mfano kama ni uhujumu uchumi au utakatishaji fedha labda alihujumu au kutakatisha thamani ya sh. billioni moja au millioni 10); aina ya jinai ya kosa linalohusika, etc.

Kesi inaweza ikafunguliwa na kusikilizwa kwenye Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi au Mahakama Kuu ya Tanzania, kutegemea na aina na thamani ya kosa.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Cap. 20, R.E. 2002] kuna kesi (makosa) ambazo mahakama za chini ya Mahakama Kuu ya Tanzania (subordinate courts) hazina uwezo wa kuzisikiliza na kutolea maamuzi. Sheria inaelekeza makosa ya namna hiyo yatafunguliwa mahakama hizo za chini halafu upelelezi (ukusanyaji wa ushahidi wa washitaki(jamhuri) hufanyikia hapo na baadae huhamishiwa (hutumwa) Mahakama Kuu kwa ajili ya kesi kusikilizwa na kuamuliwa.

Hapo (mahakama za chini)mtuhumiwa hataulizwa kama anakiri au kutokiri kosa bali atasomewa tu shitaka linalomkabili maana mahakama haina uwezo wa kutolea maamuzi kesi hizo. Hivyo kesi itapelekwa juu Mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika na mtuhumiwa ndo ataulizwa huko kama ametenda kosa au hakutenda kosa analoshitakiwa nalo ili akiri au akane kosa. Kitendo hicho chote kinaitwa "Commital proceeding".

Mfano wa kesi hizo kwa kuzingatia thamani ya fedha inayohusika na/au aina ya kosa ni:

1. Mauaji,
2. Uhujumu uchumi,
3. Utakatishaji fedha
4. Uhaini
Etc. Etc.

Hizi hutumwa Mahakama Kuu ya Tanzania maana ndo ina mamlaka (jurisdiction) ya kuzisikiliza na kutolea uamuzi.

Lengo:
1. kupunguza mlundikano wa kesi Mahakama Kuu, 2. Kuharakisha maamuzi pindi kesi ifikapo huko juu maana upelelezi tayari.
3. Kesi kuweza kupigwa chini na DPP au PP kabla haijaenda Mahakama Kuu kama ushahidi(upelelezi) haueleweki.

4. Etc, Etc.
Hivi huyo anakulipa 'ada ya wakili'?
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi, ila bado naona kuna ukakasi kuhusu utaratibu hiu
Briefly & roughly, kisheria baadhi ya mahakama zimepewa mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi kwenye kesi fulani na baadhi ya mahakama kutosikiliza na kutolea uamuzi kwenye kesi fulani. Hiki kitu kisheria wanaita "Jurisdiction "

Jurisdiction ipo kwenye mashauri yote ya madai na jinai. Nitajikita kwenye jinai kwa kuwa umetaja serikali(Jamhuri).

Kama ilivyo kwenye mashauri ya madai, jurisdiction kwenye jinai inaathiriwa na kiasi cha thamani ya fedha kinachohusika kwenye kesi (kosa) mfano kama ni uhujumu uchumi au utakatishaji fedha labda alihujumu au kutakatisha thamani ya sh. billioni moja au millioni 10); aina ya jinai ya kosa linalohusika, etc.

Kesi ya jinai inaweza ikafunguliwa na kusikilizwa kwenye Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi au kusikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania kutegemea na aina na thamani ya kosa.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Cap. 20, R.E. 2002] kuna kesi (makosa) ambazo mahakama za chini ya Mahakama Kuu ya Tanzania (subordinate courts) hazina uwezo wa kuzisikiliza na kutolea maamuzi. Sheria inaelekeza makosa ya namna hiyo yatafunguliwa mahakama hizo za chini halafu upelelezi (ukusanyaji wa ushahidi wa washitaki(jamhuri) hufanyikia hapo na baadae huhamishiwa (hutumwa) Mahakama Kuu kwa ajili ya kesi kusikilizwa na kuamuliwa.

Hapo (mahakama za chini)mtuhumiwa hataulizwa kama anakiri au kutokiri kosa bali atasomewa tu shitaka linalomkabili maana mahakama haina uwezo wa kutolea maamuzi kesi hizo. Hivyo kesi itapelekwa juu Mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika na mtuhumiwa ndo ataulizwa huko kama ametenda kosa au hakutenda kosa analoshitakiwa nalo ili akiri au akane kosa. Kitendo hicho chote kinaitwa "Commital proceeding".

Mfano wa kesi hizo kwa kuzingatia thamani ya fedha inayohusika na/au aina ya kosa ni:

1. Mauaji,
2. Uhujumu uchumi,
3. Utakatishaji fedha
4. Uhaini
Etc. Etc.

Hizi hutumwa Mahakama Kuu ya Tanzania maana ndo ina mamlaka (jurisdiction) ya kuzisikiliza na kutolea uamuzi.

Lengo:
1. kupunguza mlundikano wa kesi Mahakama Kuu, 2. Kuharakisha maamuzi pindi kesi ifikapo huko juu maana upelelezi tayari.
3. Kesi kuweza kupigwa chini na DPP au PP kabla haijaenda Mahakama Kuu kama ushahidi(upelelezi) haueleweki.

4. Etc, Etc.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi, ila bado naona kuna ukakasi kuhusu utaratibu hiu
Nadhani unaweza (I'm not certain):

Either;

Kafungue kesi ya kuiomba mahakama ikifute kifungu cha sheria hiyo kwa sababu utakazoziorodhesha.

Or;

Peleka muswada Bungeni, hata kwa hati ya dharura, kupendekeza marekebisho ya sheria, kiondolewe kifungu hicho.

Humu hautapsta ufumbuzi.

He heeee
 
Back
Top Bottom