Kwanini serikali haitoi kifuta jasho kwa wakulima wa nafaka wakiathiriwa na ukame? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini serikali haitoi kifuta jasho kwa wakulima wa nafaka wakiathiriwa na ukame?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 3, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuona Rais akitoa kifuta "jasho" kwa wafugaji wa Monduli na kuanzisha mpango wa serikali kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi (hawajasema kwa miezi mingapi) najiuliza kwanini serikali haitoi kifuta jasho kwa wakulima wa nafaka au mazao ya chakula ambao wanaathirika na ukame? kwa watu wanaokumbuka mwaka ule wa 2008/2009 pia kulikuwa na watu wengi walioathirika na ukame na mazao yao kunyauka.

  Lakini hadi hivi sasa ni wakulima wa pamba ambao walifidiwa na serikali (kwenye zile triliioni 1.6) na sasa wafugaji wa Monduli (sijui sehemu nyingine nchini wana mpango gani). Binafsi ningependa kujua ni kigezo gani kimetumiwa na serikali kuamua haya mambo (la pamba na sasa la ng'ombe); yaani kigezo ambacho hakifai kutumiwa kwa walimaji wa nafaka.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika sana ila nadhani issue hapa population tu, kwamba wakulima ni wengi sana na ukisema Serikali itoe kifuta jasho kwa kila mkulima, basi shughuli zingine zitakwama.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Majibu rahisi kwa swali zito!
  Huu ndiyo mchezo unaowaumiza walimu nchini, kwamba "tukikubaliana na madai yenu tutaunguza 80 ya bajeti!".
  Swali ni kwanini wale wengine wanaongezewa kila kukitokea upenyo, na hawa wanaambiwa hali mbaya?

  Taarifa:
  Habari nilizo nazo ni kuwa wale ng'ombe waliopelekwa Longido awamu ya kwanza wengi wamekufa kwa kiu, na ugeni wa mazingira...!
   
 4. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Mkuu siyo wakulima tu. Wapo wale wananchi wanaopatwa na majanga kama mafuriko (Kilosa), wafugaji wa kiti moto kule Mbeya ambao mifugo yao ilipuputika kwa ugonjwa na wengine wengi!
   
Loading...