Kwanini Serikali haitekelezi sera ya Elimu ya 2014. Ila bado 95% tunatekeleza sera ya Elimu ya 1995 ambayo tayari imefutwa?

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Juzi Alhamis nilialikwa ITV, Malumbano ya Hoja kuhusu Mfumo wetu wa elimu.

Ukweli ni kwamba nchi yetu tuna sera nzuri sana ya 2014 na ilizinduliwa na Kikwete kwa Shamrashamra watu wakisifu sasa tunakwenda kuleta mapinduzi ya mfumo wetu wa elimu nchini ,ila hadi sasa tunatekeleza sera ya elimu ya 1995 kwa asilimia 95.

Hii sera ya 2014 Sijui imetukosea nini, Tanzania tunatatizo la "Implementation Gap" tunatunga sera hatuzitekelezi .

Sera hii ingetatua angalau changamoto za kielimu tulio nazo nchini japo kwa asilimia kadhaa,sababu imeanisha masuala,malengo na matamko yenye suluhu ila hakuna utekelezaji wowote .

Sera hii ukiisoma vizuri unaona namna ambavyo ingekuja kutuondoa katika mkwamo huu wa elimu ya yenye mtaala wa kitaaluma na nadharia tuu na sio zaidi ya hapo .Huku tukifumbia macho suala la Vyuo vya VETA bila kuwekeza nguvu kubwa huko.

Mfano, wanafunzi nchini tulioandikishwa kufanya mtihani wa Darasa la Saba shule za Serikali 2008 , tulikuwa 1,017,967 (Milion moja ,elf kumi na Saba ,mia tisa sitini na Saba).

Tukafanya mtihani 2008 ,tuliofaulu kidato cha kwanza 2009 tulikuwa 536,672 (Laki 5 elf 36 mia sita sabini na mbili ) sawa na 52.7% ,nusu walifeli na hawakwenda kidato cha kwanza .

Hao laki 5 tulio kwenda kidato cha kwanza 2009,2010 kidato cha pili,2011 cha tatu ,2012 kidato cha nne tukasajiliwa kufanya mtihani wa Necta tuliosajiliwa tuu kwa hii miaka 4 tulipungua tena kutoka laki 5 hadi laki nne ,elf 11 mia mbili ishirini na tano (411,225).

Hao laki nne tukafanya mtihani 2012 , Matokeo yakatoka tar 30 Mei 2013 yale ya pili achana na yaliyofutwa mwanzo ,tuliopata Dvsn 1,2 na 3 ni 35,349 (Elf 35, mia tatu na arobaini na tisa) tuu. Kati ya laki nne waliofanya mtihani kidato cha nne.

kati ya Milion 1 (1,017,967) waliosajiliwa kufanya mtihani darasa la saba 2008 , Uliza hao wote waliofeli au kutoendelea na masomo wapo wapi ? hakuna jibu ,je elimu waliyoipata waliweza itumia kujiajiri au kufanya shughuli ya kuingizia kipato hakuna jibu.

JIBU NI MOJA TUU SIKU ZOTE,VIJANA ACHENI KULIA LIA AJIRA ,MJIAJIRI WENYEWE.

Sera tuu ya elimu ya 2014 mliyoitunga nyinyi wenyewe yenye majibu mahususi juu ya mfumo wetu wa elimu,hamtaki kuitekeleza tangu 2014.Mnataka nini sasa ?.

Huo ni upande wa Elimu,ukija upande wa uwezeshwaji vijana bado kuna shida juu ya shida,ukija upande wa Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili ziajiri vijana wengi ndio hatari,ukija upande wa sheria zinazozuia fursa za vijana kujiajiri ndio tele tuzidi kuzitunga ,ukija maeneo vijana walipoajiriwa ndio wanazidi kukosa kazi kwa kufungiwa ,mfano Kwanza TV,Wasafi Tv,Mwanahalisi Gazeti , Tanzania Daima Gazeti ,Watetezi Tv na vyombo au magazeti mengine.

Bado Bodi ya mikopo nayo inataka fedha yake miaka miwili ukichelewa Riba ya 10% ,ukianza katwa makato ni 15% kutoka 8% kwa mwezi ,Bado tozo ongezeko ya thamani ya mkopo 6% (Value Retention fee) ,Tozo ya Loan adminstration fee 1% . Act wazalendo katika Ilani yetu tuliahidi kugharamikia elimu ya juu na kufuta mikopo kutokana na changamoto kama hizi .

Changamoto za vijana ni nyingine sana zinahitaji mjadala wa pamoja na kuzisemea na kuzipigania.

Ngome ya vijana Act wazalendo tutaendelea kupigania na kusemea changamoto za vijana nchini bila kuchoka.

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Act wazalendo-Taifa.
 
Mzee ile sera ikitekelezwa unaweza kukuta yanahitajika madarasa na miundo mbinu mara mbili ya hii iliyopo.

Pia, mwisho ni darasa la 6 shule ya Msingi na walimu wengi wa primary wanatakiwa wapumzike.

Serikali inae akili kutotekeleza hiyo mambo kwenye sera ya elimu ya akina mkumbo
 
Back
Top Bottom