Kwanini Serikali haitaki kuruhusu kamari ya Karata (MAKATO) iwe ni halali kama michezo mingine ya Kamari?

Swizzy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
773
511
Habari wanaJF!!!

Kwanini Serikali haitaki kuruhusu kamali ya Karata (Makato) iwe ni halali kama kamali zingine?

Kwa wale wasio ujua huu mchezo wa karata (kamali ya MAKATO) huwa unachezwa hivi;

Mchangishaji anachanga karata then wewe unakatua zile karata kwa kuomba namba/card yako ya bahati. Mchangishaji anaanza kutupa karata moja moja upande wake na wako, karata yenye namba uliyo iomba ikidondokea upande wako basi wewe ndio unakuwa umekula (mshindi) na hivyo hivyo kwa upande wa mchangishaji.

Watu wamekuwa wakiwekeana viwango tofauti vya pesa kwenye huu mchezo, lakini huu mchezo serikali haiutaki kabisa jambo linalo pelekea wachezaji wa huu mchezo kucheza kwa kujificha huko vichakani.

Ombi langu kwa serikali iruhusu hii kamali ya huu mchezo kama kamali zingine zilizo ruhusiwa rasmi mfano, kamali ya Pool table, Betting zote, Biko, Tatu Mzuka, Gulugulu. etc
Nakama ni suala la mapato basi bei ya Karata iongezwe kidogo ili hawa vijana wa hii kamali ya karata (MAKATO) nao wacheze kwa uhuru kama ilivyo kwa hizo kamali nyingine, wakati huohuo wanazidi kulichangia taifa kwa kununua hizo karata.

Uzuri wa hii kamali (MAKATO) karata zikichakaa kidogo tu zina nunuliwa nyingine, maximum ni kila baada ya masaa mawili zinabadilishwa, zikichafuka kidogo tu lazima zibadilishwe. Hapo unajionea mwenyewe ni jinsi gani serikali itapata mapato mengi kupitia huu mchezo.

Najua ulishawahi kupita baadhi ya maeneo ukakutana na karata nyingi zilizo chanwa chanwa/ karata nzima zikiwa zime tapakaa eneo moja basi ujue eneo hilo huu mchezo wa kamali ya MAKATO ndio mahali pake hapo wala hata usishangae.

Serikali iuangalie huu mchezo kwa jicho la tatu kama ilivyo fanya kwenye michezo mingine ya kamali na kuacha kukimbizana/kuwakamata hawa vijana wanao cheza huu mchezo kwa kujificha.

NB: Huu mchezo wa MAKATO na LASTCARD ni michezo miwili tofauti kabisa, watalaamu wa mambo najua mmenisoma.


KAMA KUNA MCHEZO MWINGINE WA KAMALI AMBAO UNGEPENDA SERIKALI IURUHUSU UCHEZWE FREE BILA WASIWASI KAMA KAMALI ZINGINE USISITE KUUTAJA HAPA



...........NAWASILISHA........

Swizzy
 
playing-cards.jpg
playing-cards.jpg
 
Mchezo huo haufai unagharimu muda wa kufanya kazi vijana ndio nguvu kazi ya taifa
 
Mi nshacheza sana nilivyokua sekondary 2006 form 1 hyo daah huo mchezo mtamu jina jingine watt wa uswazi tunauita "NGOZI"
 
Tatizo wahusika huwa ni wezi, na huwa wako pale kwa ajiri ya kuiba tuu.
 
Mchezo huo haufai unagharimu muda wa kufanya kazi vijana ndio nguvu kazi ya taifa
utatengwa mda maalumu wa kuanza huo mchezo kama ilivyo kwa mchezo wa pool table ambao mara nyingi huwa una anza kuchezwa saa8 mchana
 
Back
Top Bottom