Kwanini Serikali haiongelei juu ya matumizi ya gesi yetu kupunguza matumizi ya mafuta?

Urusi Wanazalisha mbolea nyingi duniani kutokana na jeuri ya kuwa na gesi, sisi hapa hehe heheeee, wanataka tuagize urusi ili sijui iwe nini!
 
Wizara ya Nishati kimyaa kama vile haijui kama matumizi ya gesi yanapunguza wingi wa mafuta yanayohitajika nchini.

Ningetarajia kusikia kuwa Serikali inakwenda kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika KUBADILisha mifumo ya mafuta kwenye magari kwenda kwenye gesi
Karibu mitaa hii msikilize huyu hapa.

P
 
Siyo mafuta tu, hata kuokoa miti inayiharibiwa na watengenezaji wa mikaa
 
Hii gesi yetu kama ingekuwa iko Kenya wakenya wangetengeneza pesa nyingi sana. Wakenya wangekuwa Sasa hivi wanatuuzia gesi ya kupikia majumbani, gesi ya kutumia kwenye magari na viwandani, vifaa vya kuwezesha magari ya aina zote kutumia gesi asilia na kutusambazia vituo vya kujazia gesi kwenye magari yetu.

Sisi tunayo hii gesi kwa zaidi ya miaka 20 Sasa lakini tunalia kuhusu bei za mafuta sawasawa na wasiokuwa na gesi, nanī katuroga?

Wizara ya Nishati kimyaa kama vile haijui kama matumizi ya gesi yanapunguza wingi wa mafuta yanayohitajika nchini. Nadhani Kuna watu hawataki gesi itumike kupunguza uagizaji wa mafuta., Ufisadi.

Ningetarajia kusikia kuwa Serikali inakwenda kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika KUBADILisha mifumo ya mafuta kwenye magari kwenda kwenye gesi, vijana wengi wanapatiwa mafunzo ya ufundi wa KUBADILisha mifumo ya magari iweze kutumia gesi, nk. Lakini weee
Mawazo constructive kama haya hawayataki kwakuwa kampuni zao zinauza mafuta
 
Wanajua mijikodi waliorundika kwenye mafuta. Tukipunguza matumizi ya mafuta na huku mawazo mapya hawana yale mav8 yatakaa juu ya mawe.
Inayotuharibia hii nchi ni familia moja tu tena ya watu watatu
 
Hv Hawa mabeberu ambao muda wote huwa wanalalamikia suala la demokrasia na utawala Bora hawawezi pia kutusaidia na hii mikataba mibovu inayoidhinishwa na viongozi wa kiafrika angalao basi waafrika wafaidi rasilimali zao coz naona viongozi wa Afrika wameshindwa
 
Nilimuona Kwenye clouds tv Dr Abel kanyondo Mchumi mbobezi wa Udsm akihojiwa na Paul James ,akasema mikakati ya muda mrefu Tanzania nikutumia nishati mbadala itumie Fursa ya kuwepo gesi kwa matumizi ya Kwenye magari , majumbani , viwandani na kuzalisha umeme wa upepo na jua Kwenye gridi ya taifa kukabiliana na matatizo ya kuagiza mafuta nje ya nchi.

Akashangaa msisitizo umewekwa wa kujenga matanki ya mafuta wakati gesi ipo nchini kilichobaki ni Kuwekea miundombinu kwa matumizi mbalimbali

Mikakati ya muda mfupi ya kukabiliana na matatizo ya gharama za mafuta ni serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na hio Ela kuja kuziba pengo la gharama ya mafuta

Akaulizwa je amewahi kuwaona viongozi wa wizara na kuwapa huo mpango akajibu yeye sio msemaji wa chuo

Nchi inawataalamu wabobezi wasikilizwe na watunga sera kwa maendeleo na ustawi
 
Hii gesi yetu kama ingekuwa iko Kenya wakenya wangetengeneza pesa nyingi sana. Wakenya wangekuwa Sasa hivi wanatuuzia gesi ya kupikia majumbani, gesi ya kutumia kwenye magari na viwandani, vifaa vya kuwezesha magari ya aina zote kutumia gesi asilia na kutusambazia vituo vya kujazia gesi kwenye magari yetu.

Sisi tunayo hii gesi kwa zaidi ya miaka 20 Sasa lakini tunalia kuhusu bei za mafuta sawasawa na wasiokuwa na gesi, nanī katuroga?

Wizara ya Nishati kimyaa kama vile haijui kama matumizi ya gesi yanapunguza wingi wa mafuta yanayohitajika nchini. Nadhani Kuna watu hawataki gesi itumike kupunguza uagizaji wa mafuta., Ufisadi.

Ningetarajia kusikia kuwa Serikali inakwenda kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika KUBADILisha mifumo ya mafuta kwenye magari kwenda kwenye gesi, vijana wengi wanapatiwa mafunzo ya ufundi wa KUBADILisha mifumo ya magari iweze kutumia gesi, nk. Lakini weee
Mkuu, yaani utafikiri hii gesi haipo kabisa maana hakuna hata anayeiongelea.........au mikataba ya timu wahuni walimmilikisha mchina asilimia mia moja.
 
Nilimuona Kwenye clouds tv Dr Abel kanyondo Mchumi mbobezi wa Udsm akihojiwa na Paul James ,akasema mikakati ya muda mrefu Tanzania nikutumia nishati mbadala itumie Fursa ya kuwepo gesi kwa matumizi ya Kwenye magari , majumbani , viwandani na kuzalisha umeme wa upepo na jua Kwenye gridi ya taifa kukabiliana na matatizo ya kuagiza mafuta nje ya nchi.

Akashangaa msisitizo umewekwa wa kujenga matanki ya mafuta wakati gesi ipo nchini kilichobaki ni Kuwekea miundombinu kwa matumizi mbalimbali

Mikakati ya muda mfupi ya kukabiliana na matatizo ya gharama za mafuta ni serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na hio Ela kuja kuziba pengo la gharama ya mafuta

Akaulizwa je amewahi kuwaona viongozi wa wizara na kuwapa huo mpango akajibu yeye sio msemaji wa chuo

Nchi inawataalamu wabobezi wasikilizwe na watunga sera kwa maendeleo na ustawi
Hebu fikiria nchi ina gesi lakini tunapalangana na bwawa la kuzalisha umeme wa Maji yanayotegemea mvua. Hayo matrillions ya bwawa kwanini hayawekezwi kwenye gesi izalishe umeme mwingi? Kwanini bashe hasemi kuhusu kujenga kiwanda cha mbolea Badala yake anaongelea Kuagiza na kutoa luzuku? Kwanini kuna mazungumzo marefu kwenye Kuzalisha gesi ya kukikia majumbani?
 
Unavyoizungumzia Kenya kama vile nchi inamendeleo wakati hiyo nchi ni mali ya watu 7 tuu na familia zao
Wakenya tunawauZia Mahindi ghafi wao WAnAKWENDA KUTENGENEZa bia, chakula Ch kuku na vifaranga na kuleta huku tena. TunawauZia MaTUNDA wanakwendA kupaki kwenye vifungashio Na Kurudisha huku kama juice ya nanASI tunawanunuza.
 
Back
Top Bottom