Kwanini Serikali haijatoa tamko rasmi mpaka sasa kuhusu Makonda kufungiwa?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,211
113,520
Ni zaidi juma sasa, tokea serikali ya Marekani itoe tamko la kumpiga marufuku ‘Gavana wa jimbo la Dar es Salaam’ pamoja na mkewe, kukanyaga ardhi ya Marekani. Kwenye tamko lake hilo ilitangaza vikwazo vingine vidogo vidogo dhidi ya Tanzania na nchi zinginezo.

Mpaka sasa mimi sijasikia tamko lolote rasmi kutoka serikali ya Tanzania kuhusiana na hilo tamko la Marekani.

Sasa, yawezekana labda ni mimi tu ndiyo nipo nje ya ‘loop’ [si unajua tena siye tulioishia fom foo ya divisheni foo...vichwa vyetu vizito 🤣. Labda mpo mlio na ufahamu wa hilo. Kama mpo, kwa niaba ya wengine walio kama mimi, tunaomba msaada kwenye tuta.

Ni kwamba serikali ya Rais Magufuli haina cha kusema?

Ni kwamba imeamua kupuuza, kwa makusudi kabisa, hilo tamko la Marekani?

Au bado inafikiria cha kusema?

Au imeamua kuua soo chini kwa chini?

Au wasemaji wote wa serikali wamepangiwa shughuli za kukabiliana na Kinana?

Nashindwa jinsi ya kukitafsiri kimya hicho.
 
USA sio muhimu sisi kwenda kwanza wengine toka tuzaliwe hatujawahi kwenda na maisha yanaenda na tukitaka kusafiri zipo nchi nyingi sana duniani tunaweza kwenda..

Lakini pia tunampiga ban Trump na Pompeo kukanyaga Tanzania, huyu Balozi wao soon tutamtimua..
 
USA sio muhimu sisi kwenda kwanza wengine toka tuzaliwe hatujawahi kwenda na maisha yanaenda na tukitaka kusafiri zipo nchi nyingi sana duniani tunaweza kwenda..

Lakini pia tunampiga ban Trump na Pompeo kukanyaga Tanzania, huyu Balozi wao soon tutamtimua..


Mtaacha na kutumia mtandao wa intaneti?

Mtazirudisha Dreamliners?

Mtaacha na kunywa Pepsi?
 
Back
Top Bottom