Kwanini Serekali inakopa kama inaweza ku-print noti mpya

Vipi Serikali inapopokea pesa za msaada. Mabilioni ya Pesa au Trillions of money. Je, pesa hizo nazo huoni zinaweza kusababisha mdororo wa kiuchumi kwasababu Serikali imezipata bwerere bila ya Ku_create value? Na Je, pesa hizo za msaada zinatofauti gani na kuchapisha pesa mpya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wataalamu wa Uchumi, naomba ufafanuzi wa hili swali mie niliye layman wa Uchumi..
 
Hizo pesa za msaada tayari zina - value na zinakua guaranteed na benki kuu ya taifa husika, zilichapishwa kwa sababu kuna value ilishakuwa created. Tunapoongelea kuchapisha pesa kwa kureplace zile zilizochakaa hiyo huwa haina shida, na pia tunapoongelea kuchapisha pesa ili kujazia kukua kwa uchumi hiyo haina shida pia. Mfano, uchumi wote una jumla ya machungwa 10 na pesa katika mzunguko ni shs.1,000/= basi kila chungwa linawakilisha shs.100/= iliyopo kwenye mzunguko, kwa machungwa 10 (100/= x 10) ndio jumla ya 1,000/= kwenye uchumi, sasa inapotokea mtu akafanya kazi na akazalisha machungwa matano (5), kwahiyo jumla tuna machungwa 15, na serikali sasa inaweza ikachapisha noti za jumla ya shs. 500/= ili kuwakilisha huu ukwasi mpya (created value) ulioingizwa kwenye uchumi, na hivyo jumla
Kutakuwa na shs.1,500/= inakimbiza machungwa 15 na hivyo bei ya kila chungwa inabaki ile ile 100/= kama awali (no negative effect). Halikadhalika kama katika hiyo 1,500/= ikatokea noti za jumla ya shs. 100/= zimechakaa na zikachanwa chanwa na kuchapisha mpya za kiwango hicho hicho basi jumla ya pesa kwenye mzunguko itabaki 1,500/= na bei ya kila chungwa itabaki shs.100/= ile ile (no negative effect). Shida ni pale jitu litakapochapisha pesa bila kuchana kiwango sawia za zilizochakaa au kuchapisha pesa zaidi ya kiwango cha ukuaji wa ukwasi wa taifa (uchumi). Hivyo hao wanaotoa misaada pesa zao kama zilivyo zetu ziko backed na ukwasi uliopo kwenye uchumi wao, otherwise pesa zao zisingekuwa na thamani katika masoko ya kubadilisha pesa endapo wangekuwa wanachapisha pesa ambazo haziwakilishi ukwasi waliouzalisha (value created) katika uchumi wao, sasa nani atapokea msaada wa pesa isiyo na thamani katika soko la fedha?
 
Mkuu, binafsi nakushukuru sana maana jinsi unavyoelezea hata kama mtu kaishia darasa la saba akiwa makini hakika atapata ufahamu wa kile unachomaanisha.

Hata hivyo, hapo kwenye nchi kupokea fedha za misaada kutoka nje nadhani bado panahitaji ufafanuzi zaidi.

1. Je, unamanisha kuwa nchi haiwezi kupokea fedha za msaada bila kwanza ku-create value?
2. Na je, unaweza kuelezea ni kwa namna gani Nchi inaweza ku-create value kabla ya kupokea fedha za misaada?
3. Je, unamanisha kuwa inaweza kufikia hatua nchi ikakataa kupokea fedha za misaada kwa sababu tu haija-create value ili kuepusha mdororo wa kiuchumi?
 
Nayajibu yote kwa pamoja, kuna kitu ume mis understand, anaye create value ni yule aliyekupa msaada, otherwise pesa yake ingekuwa worthless katika soko la fedha endapo angekuwa tu amechapisha pesa ambayo haina value created for it.
 
Mkuu, nakushukuru na ninakuomba uvumilie usichoke kutoa shule hii muhimu.

Swali la msingi la mdau wa kwanza lilikuwa; Je ni kwa nini Serikali inakopa badala ya kuchapisha noti zake mpya?

Jibu: Katika Facts za kiuchumi, kiwango cha fedha katk nchi inatakiwa kiendane na thamani ya shughuli za kiuchumi. Mfano : Kiwango cha uchumi wa nchi ni sawa na thamani ya machungwa 10 yenye jumla ya sh 1,000 yaani @ sh 100. Endapo utazidisha pesa ktk nchi wakati idadi ya machungwa inabakia ileile then lazima kuwepo mfumuko wa bei na hivyo mdororo wa kiuchumi. Mfano; tukiongeza sh 500 ktk mzunguko wa pesa; maana yake jumla itakuwa 1,500 na bei ya Chungwa itapanda na kufikia 150(mfumuko wa bei).

Lakini endapo ikiwa ni kinyume chake kwamba kulikuwa na machungwa 10 yenye thamani ya Tsh 1000. Na ikapatikana fursa ya kuongeza uzalishaji wa machungwa yakafikia 15. Hapo hakuna shida (value created) na Serikali inaweza kuchapisha fedha mpya kujazia ukuaji wa uchumi uendane na thamani ya uzalishaji.

Sasa swali langu likaja.Je; nini hutokea pale Serikali inapopata pesa za msaada ambazo hazikuwa kwenye mpango? Ukasema; Pesa za msaada huko kwa donor country anakuwa amekwisha create value tayari yaani amefikia hadi kuwa na Surplus hivyo akitoa kama msaada haina shida.

Hapo kwa donor country mimi sina shida napo; shida yangu ipo kwa huyu mpokeaji. Nikauliza, Je anapopokea pesa ambayo kule ilikotoka tayari value ilishakuwa created kwa kuwa na surplus; sasa vipi kwa sisi wapokeaji. Huoni tunapokea pesa ambayo sisi huku ndani hatujaongeza kiwango cha uzalishaji wa machungwa yaani tunataka kuongeza pesa wakati machungwa ni yaleyale 10? Na Je pesa hiyo ya msaada itakuwa na tofauti gani na kuchapisha pesa nyingine? Maana imekuja ikiwa huku ndani kwetu hatuja-create value? Naomba usichoke kutoa shule mkuu. Ahsante.!

1.) Hiyo pesa tunayopokea ni fedha ya KIGENI, hatupewi msaada kwa shillingi ya kiTz, hivyo value ya hiyo pesa ya kigeni, mfano kama ni machungwa basi hayo machungwa yapo huko kwenye nchi iliyotupa msaada, yaani kama wametupa msaada wa dollar ambayo exchange rate yake inatupa jumla ya shs. 500/= basi hiyo ni sawa na ametupa msaada wa machungwa matano kwa bei ya 100/= kwa chungwa, ila badala ya kutupa machungwa matano alaona ni rahisi kutupa makaratasi (pesa) ambazo zinawakilisha hayo machungwa matano ambayo yeye anayo nchini kwake alikwisha yazalisha.Hivyo machungwa si yale yale 10, bali ni 15, hayo matano ya ziada yapo nchini kwake anaetusaidia, alikwisha yazalisha., na at anytime, tunaweza kuitumia pesa hiyo ya kigeni kama tukitaka ku-import hayo machungwa matano kuja nchini mwetu.
2.) Hiyo pesa ya msaada si sawa na kuchapisha kwa sababu ni pesa ya kigeni na si pesa ya kiTz tunayopewa msaada, na hiyo pesa value yake inakuwa backed na mali/ rasilimali/ huduma amabzo zimekwisha zalishwa (value creation) huko katika nchi inayotupa msaada, actually jibu na 1.) linafaa hapa pia
 
Back
Top Bottom