Kwanini SAUT wawe wababe kiasi hiki?

Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,343
3,280
BARUA YA WAZI KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGUSTINE - MWANZA (MAIN CAMPUS).

Dear all,

Lengo la barua hii ni kuhusu "utaratibu wa ulipaji ada" hapa chuoni na jinsi wanafunzi tunavyoumizwa na utaratibu huu ambao naamini haujajengwa kwenye misingi ya HAKI. Sijaona njia nyingine ya kufikisha ujumbe wangu zaidi ya kuandika barua hii ili na wewe ufikiri na uchukue hatua.

Ni wazi kuwa utaratibu unaotumiwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine - Mwanza, kuhusu kushughulikia wanafunzi wanaoshindwa KULIPA ADA KWA WAKATI unaumiza, unatesa na haufai kuendelea.

Utaratibu huu unaotumika kushughulikia suala nililoainisha hapo juu ni kama ifuatavyo.

> Mwanafunzi yeyote anayeshindwa kulipa ada kwa wakati atalazimika kulipa faini ya kitu wanachoita "USUMBUFU".

> Kwa ajili ya usumbufu huu mwanafunzi atalazimika kulipa Tsh. 100,000/-

> Hata kama mwanafunzi atashindwa kumaliza kiasi cha Tsh. 2000/- (ELFU MBILI) atalazimika kulipa kiasi hiki hiki cha Tsh. 100,000/- kama faini.

> Hata kama mwanafunzi alilipa ada kwa WAKATI ila amechelewa kubadilisha risiti na yeye atalazimika kulipa "tozo" hii. (Hapa chuo hakijali kama pesa ilishaingia kwenye account yao kabla ya deadline date). Good example of DICTATORSHIP.

> Mwanafunzi huyu hatasikilizwa kwa namna yoyote ile (poor conflict resolution skills) kuhusu hitaji lolote linalohusu ulipaji ada.

> Hata kama mwanafunzi aliandika barua ya kuomba kuongezewa muda wa kulipa ada na barua yake IKAPOKELEWA bado suala lake halitosikilizwa kamwe. (Another example of DICTATORSHIP)

Hii ndio SAUT, lakini WANAFUNZI HAWANA SAUTI!

Hebu fikiri kuhusu hili na uone jinsi utaratibu huu unaotumiwa hapa chuoni unavyoweza kuwa na "HARUFU" ya rushwa kwa sababu hata hii faini anayotozwa mwanafunzi haijulikani inatumika katika lipi.

>Tupo wanafunzi tusiopungua 10,000 Chuo cha Mtakatifu Augustine - Mwanza (main campus).

> Wanafunzi wanaoshindwa kukamilisha ada kwa wakati ni wengi kwa sababu nyingi na nzito.

>Kwa kadirio la chini kabisa (inaweza kuwa zaidi ya hapa) wanafunzi 1000 wanashindwa kukamilisha ada kwa wakati kwa sababu tofauti tofauti.

> Idadi hii ya wanafunzi 1000 ni kwa kadirio la semester moja tu. Hivyo kwa semester mbili ni wanafunzi 2000 kwa kadirio lile lile.

> Wanafunzi 2000 kwa semesters zote mbili watalipa jumla ya Tsh MILIONI 200 KAMA FAINI TU.

> Kama idadi hii ya wanafunzi 2000 itaongezeka (obviously itaongezeka kutokana na hali ya maisha kwa ujumla) basi ni kiasi kikubwa sana cha pesa kinatengenezwa.

>Kwa maana hii, kwa miaka mitatu, yaana semester 6 jumla ya MILLIONI 600 inatengenezwa kwa kutoza wanafunzi "hard earned money" toka kwa wazazi, walezi au wanafunzi binafsi.

MASWALI NI JE KIASI HIKI KIKUBWA Tsh 200,000,000/- "KINACHOTENGENEZWA KWA MWAKA" NI MARADI AU NI NINI?

JE, SISI WANAFUNZI KWA HALI HII YA "UONEVU" TUENDELEE KUBAKI KIMYA KAMA HAYATUHUSU?

JE, HATUNA HAKI YA KUTETEA "MASLAHI YETU" KAMA WANAFUNZI?........ MBALI NA KUPATA ELIMU TU?

JE HATUNA HATA HAKI YA KUONGEA KUHUSU JAMBO HILI NA KUTOA "INPUTS" ZETU VILE TUNAPENDA MAMBO YAENDE?

HATUNA HAKI HII?

--------

Concerned student.
 
Nimelipa hiyo laki moja kwa kuchelewa tu kupeleka risiti,mwaja jana.

Nashukuru nimemalizana nalo,ila kwa mbinde saana.

Na ukiwagomea warumi wanakufukuza.
 
Hama!!! Umelazimishwa....Wanafunzi mnakula ada kwa kufanya starehe na kulala club usiku kucha na guest house...

Halafu Ngoja nikuambie kitu.....Kitu chochote kinachoongozwa na Kanisa Katoliki huwa kanisa halina cha kupoteza.....(The church has nothing to loose)

Ukibainika hata wewe ni mara moja unafukuzwa na hakuna negotiation.
 
Solution ni kugoma tu

Catholic has nothing to loose....Wanaweza fukuza wote na wakaanza upya....Nakumbuka Seminary fulani walifukuza wanafunzi wote wa kidato cha nne mwezi mmoja kabla ya mtihani.....

Darasa hilo la Form 4 lilikuwa Best in the country matokeo ya kidato cha pili....Ila wote walifukuzwa...
 
duh! hii ni hatari,,,,kama ulikosa kwa wakati ile ya mwanzo, hiyo nyingine itakuwaje? ni sawa faini lakini ni kubwa au ingetozwa kulingana na uzito wa sababu.
 
hao ndio SAUT nawapenda sana
moja mwanafunzi ujifanya mjanja mjanja kulipa ada unaumbuka
mbili ukijifanya mjanja mjanja ki academic at the end unaumbuka
tatu wakatoriki wananjenga mtu kujua wajibu wake si porojo na siasa wewe kama umeamua kusoma acha mambp mengine soma ukiona mambo yamepandan milango iko wazi ailisja mwaka

sasa wewe baada ulipe ada unajifanya mfanyabishara, mpenda anasa, unatakas kuishi maishi kama mtumishi lazima ikukost

kwa wale mnaoshindwa lipa ada kwa wakati pelekeni tarifa mapema mwanjonde anapokea n fine hupati wewe omba special exam to tarifa wanakubali

siyo uchezee pesa hesabu zigome uje ilaumu SAUT wewe utakuwa una matatozo.
 
Ulitaka utaratibu gani. Nenda kasome chuo chenyeutaratibu unaoutaka wewe. Kazi kula ada afu mnalalamika
 
hao ndio SAUT nawapenda sana
moja mwanafunzi ujifanya mjanja mjanja kulipa ada unaumbuka
mbili ukijifanya mjanja mjanja ki academic at the end unaumbuka
tatu wakatoriki wananjenga mtu kujua wajibu wake si porojo na siasa wewe kama umeamua kusoma acha mambp mengine soma ukiona mambo yamepandan milango iko wazi ailisja mwaka

sasa wewe baada ulipe ada unajifanya mfanyabishara, mpenda anasa, unatakas kuishi maishi kama mtumishi lazima ikukost

kwa wale mnaoshindwa lipa ada kwa wakati pelekeni tarifa mapema mwanjonde anapokea n fine hupati wewe omba special exam to tarifa wanakubali

siyo uchezee pesa hesabu zigome uje ilaumu SAUT wewe utakuwa una matatozo.

Hawa jamaa huwa wanajifanya wajuaji sana na tamaa ya kuongeza vyuo huku wameshikilia ardhi kubwa Mwanza main compus kujenga hawawez wanatuletea mapori ndani ya jiji! Tibaijuka wanyang'anye ardhi watu wajenge jiji lipendeze shenz gete!
 
Hapa ni chuki zimekujaa!!!
 
Hapa ni chuki zimekujaa!!!

Sina chuki ila huo n ushaur wajenge kwanza chuo kimoja kieleweke sio kuwa na tamaa! huwaioni UDOM au UDSM vinavyovutia na kuchochea maendeleo sehemu vilipo wao wanaendelea kukumbatia mapor na vichaka katikat ya jiji huku wanakimbilia kuanzisha vyuo mikoani?
 
Namshukuru Mungu chuo nilichosoma baada ya kulipa registration semester ya kwanza nimekuja kupewa hesabu ya madai siku nimerudi kuchukua transcipt.

Hivi wanavyosema public university SAUT siyo ndo maana iko hivyo?

Lakini mbona daladala ni public transport wakati ni ya mtu binafsi?
 
BARUA YA WAZI KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGUSTINE - MWANZA (MAIN CAMPUS).

Dear all,

Lengo la barua hii ni kuhusu "utaratibu wa ulipaji ada" hapa chuoni na jinsi wanafunzi tunavyoumizwa na utaratibu huu ambao naamini haujajengwa kwenye misingi ya HAKI. Sijaona njia nyingine ya kufikisha ujumbe wangu zaidi ya kuandika barua hii ili na wewe ufikiri na uchukue hatua.

Ni wazi kuwa utaratibu unaotumiwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine - Mwanza, kuhusu kushughulikia wanafunzi wanaoshindwa KULIPA ADA KWA WAKATI unaumiza, unatesa na haufai kuendelea.

Utaratibu huu unaotumika kushughulikia suala nililoainisha hapo juu ni kama ifuatavyo.

> Mwanafunzi yeyote anayeshindwa kulipa ada kwa wakati atalazimika kulipa faini ya kitu wanachoita "USUMBUFU".

> Kwa ajili ya usumbufu huu mwanafunzi atalazimika kulipa Tsh. 100,000/-

> Hata kama mwanafunzi atashindwa kumaliza kiasi cha Tsh. 2000/- (ELFU MBILI) atalazimika kulipa kiasi hiki hiki cha Tsh. 100,000/- kama faini.

> Hata kama mwanafunzi alilipa ada kwa WAKATI ila amechelewa kubadilisha risiti na yeye atalazimika kulipa "tozo" hii. (Hapa chuo hakijali kama pesa ilishaingia kwenye account yao kabla ya deadline date). Good example of DICTATORSHIP.

> Mwanafunzi huyu hatasikilizwa kwa namna yoyote ile (poor conflict resolution skills) kuhusu hitaji lolote linalohusu ulipaji ada.

> Hata kama mwanafunzi aliandika barua ya kuomba kuongezewa muda wa kulipa ada na barua yake IKAPOKELEWA bado suala lake halitosikilizwa kamwe. (Another example of DICTATORSHIP)

Hii ndio SAUT, lakini WANAFUNZI HAWANA SAUTI!

Hebu fikiri kuhusu hili na uone jinsi utaratibu huu unaotumiwa hapa chuoni unavyoweza kuwa na "HARUFU" ya rushwa kwa sababu hata hii faini anayotozwa mwanafunzi haijulikani inatumika katika lipi.

>Tupo wanafunzi tusiopungua 10,000 Chuo cha Mtakatifu Augustine - Mwanza (main campus).

> Wanafunzi wanaoshindwa kukamilisha ada kwa wakati ni wengi kwa sababu nyingi na nzito.

>Kwa kadirio la chini kabisa (inaweza kuwa zaidi ya hapa) wanafunzi 1000 wanashindwa kukamilisha ada kwa wakati kwa sababu tofauti tofauti.

> Idadi hii ya wanafunzi 1000 ni kwa kadirio la semester moja tu. Hivyo kwa semester mbili ni wanafunzi 2000 kwa kadirio lile lile.

> Wanafunzi 2000 kwa semesters zote mbili watalipa jumla ya Tsh MILIONI 200 KAMA FAINI TU.

> Kama idadi hii ya wanafunzi 2000 itaongezeka (obviously itaongezeka kutokana na hali ya maisha kwa ujumla) basi ni kiasi kikubwa sana cha pesa kinatengenezwa.

>Kwa maana hii, kwa miaka mitatu, yaana semester 6 jumla ya MILLIONI 600 inatengenezwa kwa kutoza wanafunzi "hard earned money" toka kwa wazazi, walezi au wanafunzi binafsi.

MASWALI NI JE KIASI HIKI KIKUBWA Tsh 200,000,000/- "KINACHOTENGENEZWA KWA MWAKA" NI MARADI AU NI NINI?

JE, SISI WANAFUNZI KWA HALI HII YA "UONEVU" TUENDELEE KUBAKI KIMYA KAMA HAYATUHUSU?

JE, HATUNA HAKI YA KUTETEA "MASLAHI YETU" KAMA WANAFUNZI?........ MBALI NA KUPATA ELIMU TU?

JE HATUNA HATA HAKI YA KUONGEA KUHUSU JAMBO HILI NA KUTOA "INPUTS" ZETU VILE TUNAPENDA MAMBO YAENDE?

HATUNA HAKI HII?

--------

Concerned student.

Ni katika hali ya kujenga jiji la Mungu
 
SAUT sio chuo, ni secondary. Vyuo ni UDSM,SUA , MZUMBE na UDOM ukishindwa kabisa kasome IFM au IAA. Umeenda choo cha kike, SAUT ni chuo cha wanafunzi waliopata division 3 na 2 za mwisho. Ila jitahidi umalize mwaka wa mwisho, masters kasome UDSM uimprove cheti chako cha SAUT
 
Back
Top Bottom