Salum Mwalimu ni mmoja wapo wa wagombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.
Ni ukweli ulio dhahiri Salum Mwalim sio chaguo letu wakazi wa jimbo la Kinondoni kutokana na sababu zifuatazo:-
1. Hana Ilani ya uchaguzi
Hii ni sababu inayomfanya Salum Mwalimu kutokufaa kuwa Mbunge jimbo la Kinondoni. Chama kilichoshinda na kushika dola kuanzia 2015 hadi 2020 ni CCM ambacho ilani yake ndio inaongoza Serikali.
Leo Salum Mwalimu anapoomba ridhaa ya kuwa Mbunge ataleta maendeleo kwa ilani ipi? Kwanini wana Kinondoni wamchague Mtu asiye na ilani, asiyeweza kuwaletea maendeleo?
2. Hana pesa za kutekeleza ahadi zake
Salum hakubaliani na ilani ya CCM ambayo ndio inaongoza dola, ndio yenye Serikali inayomiliki pesa zote hapa nchini. Anayowahaidi wana Kinondoni atatekeleza kwa ilani ipi? Salum atapata wapi pesa za kutoa huduma za kijamii? Atatoa wapi pesa za kujenga miundombinu? Atatoa wapi mabilioni ya kuwapa mikopo vijana na kina Mama endapo hakubaliani na ilani ya CCM? Kama hayawezi yote hayo, atawezaje kuwaletea maendeleo wana Kinondoni?
3. Chama chake hakina mahusiano mema na Serikali
Kwa nyakati zote Chadema wamekuwa hawana mahusiano mema na Serikali ndio maana kutwa wanaitukana Serikali majukwaani, mitandaoni na mikutanoni. Wanaitukana Serikali ambayo ndio ina ilani, inamiliki pesa zote, inayopanga namna ya kupeleka maendeleo.
Salum anautaka Ubunge wakati anajua fika chama chake hakina mahusiano mema na Serikali inayotekeleza ilani ya uchaguzi. Atawezaje kuwaletea maendeleo wana Kinondoni?
4. Hana uzoefu
Salum anaomba kura aende Bungeni kwenda kujifunza namna ya kufanya kazi. Hana uzoefu wowote ule, anahitaji muda wa kujifunza na si kipindi hiki ambacho wana Kinondoni wanahitaji kiongozi mwenye uzoefu, wanahitaji maendeleo.
Narudia tena kusema Salum Mwalim hafai kuwa Mbunge wa Kinondoni.
Mussa Seif,
Bodaboda Kinondoni.