Kwanini Rwanda ndio kioo cha Watawala Afrika Mashariki na Kati?

Halafu kioo cha watawala Afrika mashariki na Kati ni Tanzania mkuu.. asikudanganye MTU
 
Rwanda ni nchi ndogo sana kuliko mkoa wa Tabora. Walipata shamba la bibi Congo wakalitumia ipasavyo. Sisi hatuna shamba. Wale wana propaganda nyingi na hawana vyombo huru vya kujua habari zao na ukweli halisi hasa vijijini. Ni nchi masikini sana. Viongozi unaosema wanakimbilia huko kujifunza ni kwa sababu ya uvivu wao wa kufikiri. Ati wanaenda Rwanda kijifunza usafi, really? Kina Sirro wanaenda kijifunza jinsi ya kutesa watu wao na kulinda utawala dhalimu wala hakina kingine. Vinginevyo wangeenda USA, UK nk kujifunza utawala, amani, maendeleo, kilimo bora, viwanda, mpira, nk nk.
Huo ndio ukweriiii 100% ndugu zangu.
 
Rafiki yangu architect alipata kazi Scotland, alipelekwa Rwanda miaka minne, kampuni yao ilipata contract ya kubuni na kujenga majengo ya serikali.

Kila anochofanya Kagame ana lenga miaka 100 ijayo.
 
Kumekuwa na Safari kadhaa kwa watawala na wakuu wa vikosi vya ulinzi katika nchi za afrika mashariki na Kati kwenda Rwanda. Ziara hizo bila ya shaka huwa zinabeba ajenda nyingi.

Ama kwanini Rwanda kioo na kigezo watawala na viongozi waandamizi katika serikali za afrika mashariki na Kati. imekuwa ni Rwanda kwasababu ya unyeti wake kimkakati kwa Mataifa ya kimagharibi katika ukanda huu wa afrika ya mshakariki na Kati. Na sababu za msingi ni hizi.

1. Mtawala wa nchi hiyo. Mtawala wa nchi ya Rwanda Paul Kagame ni zao la mashirika ya kijasusi ya America. Ifahamike kuwa kagame alilelewa katika mashirika hayo miezi 17 kabla ya Kuja kupewa nchi ya Rwanda ili atekeleze ajenda za wamagharibi na hasa Amerika katika ukanda wa afrika mashariki na Kati. Naam kazi hiyo kaifanya vyema sana na katika aliyoyafanikisha ni haya.

a. Kutengeneza njia nyepesi kwa wamagharibi Hasa Amerika kuchota Mali ya Kongo. Na hiyo ni kusimamia machafuko yote ndani ya kongo kwa kuingiza majeshi yake na kuchochea vita nchini humo.

2. Kuizamisha nchi ya Rwanda katika mfumo wa kibepari kwa asilimia Mia. Na kuyafanya maisha ya wanyarwanda Kuwa magumu kuliko sehemu yoyote katika ukanda wa afrika mashariki na kati. Imekuwa ni nchi ambayo kila kitu lazima kitolewe tozo. Raia wamekuwa wakitafuta Mali kwa ajili ya serikali na sio kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Wanyarandwa kula mlo mmoja kwa siku ni jambo la kawaida.

3. Kuwa muhimili mkubwa katika kubeba ya wamagharibi katika yale yanayoitwa mapambano dhidi ya ugaidi. Tumeiona Rwanda ikihudumu vyema katika ajenda hio katika muungano wa Amesom nchini Somalia na Sasa huko msumbiji.

Baada ya Rwanda kuwa mfanikishaji wa ajenda hizi nyeti katika ukanda huu, wamagharibi wakaienzi nchi hiyo kwa mengi. Kama vile kuanzisha baadhi ya viwanda katika nchi hiyo kama viwanda vya magari, simu na kiwanda kusafisha dhahabu. Na kuitangaza kuwa ni nchi inayokuwa kiuchumi kwa kasi kubwa kwa vipimo vya mabepari. Ili kuikuza zaidi kama zawadi ya kufanikisha ajenda zao.

Lakini pia wamagharibi wakamfumbia macho mtawala wa nchi hiyo Pauli kagame kwa mambo yote ya unyama anaoufanya katika nchi hiyo. Kwasababu ya utekelezaji wake mzuri wa kazi zao. Na kwakuwa raia wa Rwanda ni miongoni mwa watu duniani wanaoishi kwa mtutu wa bunduki. Hali hivyo imempelekea kiongozi huyo kuishi kwa tahadhari na khofu ya kupinduliwa. Tahadhari ya kiongozi kwa kupinduliwa imekuwa ni kubwa Sana kwake. Jambo ambalo limemfanya aje na mikakati kadhaa kupambana na kila anaetishia utawala wake na kuuokosoa. Na katika mikakati hiyo ni.

Kuzuia harakati za kidini kwa lengo la kulinda utawala wake. Tahadharini hiyo imemfanya adhibiti maeneo yote ambayo anaona ni hatarishi kwake. Na katika maeneo hayo ni sehemu za ibada misikitini na makanisani. Hilo likienda sambamba na yanayoitwa mpambano yanayoitwa ya ugaidi. Mpambano yanajulikana walengwa ni Waislamu.

Na ndipo alipoamua kuyafunga makanisa zaidi ya 8000 na misikiti miwili na kuweka makachero katika maeneo hayo kuratibu kila kinachofundishwa ili kudhibiti harakati za mapinduzi. Ufungaji wa makanisa ni khofu ya kupinduliwa na hiyo kutokana na wakristo kuwa wengi nchi humo na hawampendi. Kwani anajua wazi kuwa raia wa nchi hiyo hawana mapenzi nae hata kidogo kwani kawafukarisha Sana na kuitajirisha familia yake. Ama kuhusu misikiti ni ajenda dhidi ya kupambana na ugaidi (Uislamu)

Naona uigwaji unachukua nafasi kivitendo.

Haya ndio yanayoenda kuigwa na watawawala na viongozi waandamizi nchini Rwanda. Na baada ya kuchukua hayo ndio tunaambiwa Sasa hivi watu watapita katika msikiti na Madrasa kuangalia namna ya Waislamu wanavyofundisha Q'uran. Maana wao ndio wanajua zaidi namna ya kusomesha Q'uran na Uislamu vizuri kuliko Waislamu wenyewe. Tunasema ajenda ni Uislamu tu kwasababu aliesema maneno hayo ni mtu aliesomea upadri mwenye chuki ya wazi kwa Uislamu na Waislamu anajua kabisa yaliyomo kanisani hayana athari kwakuwa ni Dini ya kiroho tu. (spiritual religion ) kule ni misa, sadaka na mziki mnene. Rwanda ndio wakaoiga kuwaumiza watu na tozo katika kila kitu.

Ama Dini ya kiislamu ndio Dini lengwa kwasababu ni Dini ya kimfumo. Iliyojikamilisha katika nyanja zote maishani. Katika siasa, uchumi na jamii. Na ndio tishio la mfumo utawalao leo duniani ubepari. Kwa hivyo tunarajia kuona vyuo vikifungwa na watu wakibambikiziwa kesi za Ugaidi na kufilisiwa Mali zao.....

Ujumbe.
Ujumbe kwa Waislamu ni wajibu wenu kukamatana na Uislamu wenu bila ya kuogopa lawama za wenye kulaumu. Na hata kama ni kufa kwa ajili ya Uislamu wenu ni bora zaidi na ndio kifo bora zaidi kuliko vifo vyote. Na jitulizeni kutokana na maneno haya ya Allah.

(قُل لَّن یُصِیبَنَاۤ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡیَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ)
[Surat At-Tawbah 51]
"Hayatufiki sisi isipokuwa yale aliyopanga Allah yeye ndio Mola wetu na kwa Allah wategemee waumini"

Ama kwa wenye chuki na Uislamu tunawaambia wao sio wa mwanzo wamepita wengi lakini wameicha Dini ikizidi kuenea kwa kasi, pamoja na vigingi vingi inavyokutana navyo. Na kubwa wafanye wafanyavyo wote tunakufa na huenda dhalimu akafa kabla ya mdhulumiwa. Wamepita wengi walionyesha uadui wao dhidi ya Uislam lakini imebaki historia tu. Allah anasema

(وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَـٰفِلًا عَمَّا یَعۡمَلُ ٱلظَّـٰلِمُونَۚ إِنَّمَا یُؤَخِّرُهُمۡ لِیَوۡمࣲ تَشۡخَصُ فِیهِ ٱلۡأَبۡصَـٰرُ)
[Surat Ibrahim 42]

"Wala msidhani kuwa Allah amesahau yale wanayoyafanya madhalimu hakika anawachelewesha mpaka katika Siku zikazozongwa nyoyo na macho"

Hakuna aliewaiga Rwanda kibaraka kiongozi wa wamagharibi isipokuwa atawaumiza raia zake.
Hakuna cha kujifunza kutoka kwa kagame, labda kuiga laana aliyonayo ya mauwaji tu
 
Sisi wenyeji wa karagwe, kyerwa na ngara mkoani kagera ndo tunawafahamu wanyarwanda vzr.

Ni maskini mno wale watu
 
Wakati wa utawala wa awamu ya nne , nchi yetu haikuwa na mahusiano mazuri na Rwanda, matokeo yake ni kwamba vitendo vya ukandamizaji kwa raia vilikuwa ni kidogo sana.

Alipoingia madarakani Rais John Magufuli, katika moja na hotuba zake alikiri kupewa ushauri na rais Kagame juu ya ununuzi wa ndege kwa cash, na nina uhakika alishauriwa na vingine pia.

Katika utawala huo wa John Magufuli, mahusiano ya nchi yetu na Rwanda yakaimalika, na hapo ndipo tukaanza kuona vitendo vya kutekana, kuuana, kupigana risasi, wapinzani kushughulikiwa nk

Juzi hapa IGP Sirro alitoka Rwanda bila aibu wakati akiongea na vyombo vya habari akatangaza kuanza kufuatilia yanayofundishwa kwenye nyumba za ibaada hasa Misikitini na Sunday School, kwa kigezo cha kwamba Rwanda wamefanikiwa sana kwenye njia hiyo ili kuzuia ugaidi.

Kwa kifupi ni kwamba, Jenerali Kagame, Jenerali Museveni na CCM ya Tanzania hawa ndiyo wanaunda utatu haramu ndani ya ukanda huu wa Africa Mashariki.
 
Mimi nilimdharau alipojitokeza kama raisi wa kwanza kusapoti Gadafi avamiwe kijeshi
ajabu na kweli daaando ilivo kuwa????? any way nilikuwa shule wkt huo sikuipata hiii!! ila nikijua kuwa ni kweli nitamdharau sana huyu jamaa daaa!
 
Yote kwa yote!! wazungu wana slogan zao zinasema hivi ''Wao km wao!! hawana Rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu'' Huyo Kagame ajipange kwa matumizi tu, lkn iko siku yatamkuta km yaleeee!! ya

Savimbi wa angola dhidi ya Agostini Neto(mwenzake bado ala bata), Sadadam Hussein yuko wapi!! alitumiwa dhidi ya Ayatolah Khomein! Hissene Habre!! Idd Amini Dada, huyu aliandaliwa maksudi!! lkn akagutuka wkt alishakula vyao!!

so wazungu walimgeuka mbaya........ nyerere kaipata hii kuwa wamemgeuka ikawa fursa kwake so akampa kichapo kileee cha Lukaya!...... Juzijuzi hapa Mobutu aliipata hata hawakumtaka aende kutibiwa tu!! akafa km mbwa!!

Hao na wengine weeengi! sana walitumikia Mibeberu!! lkn walitoswa km hawajawahi tumika!!!! Nyerere alikataa kutumikia weupe kabisaaa!! akajiunga na ndg zake Frontline state!! alizikwa kwa heshima mpaka leo! Africa hii atakumbukwa mnooo!!

kIFUPI urafiki na Mweupe ukiwa km mkuu wa nchi hauna mwisho mwema, nakwambia!!! hii ni sheria ya Historia watakuendesha weee!! kwa faida yao! ipo siku utasema duuu nimekuwa sana Dikteta lkn ''hapa??? hapana sitaki!!

Hapo hapo ndo patamu wanakumaliza wao dakika sifuri km Saddam!! kivipi?? wanakuacha au kuongezea nguvu kwa adui yako! ....Sasa huyu kagame huyu???????? weee!!.... muache tu!! iko siku isiyo kuwa na tarehe atakufa kifo kibaya sana tena na hao hao!!

Weupe watamnyonga live!! sijui atamlilia nani???? Najua muheshimwa unapita pita humu! soma uelewe hii ikamate kabisaaa!! bora uwe na urafiki na ndg zako Africa, watakuhifadhi utaishi wanajua!! si unaona Mengistu Haile Maliamu anakula Bata kiulainiiii!!

Kaunda kazomewa weeee!! na chiluba huyo hapo!! walewale ndg zake wa south/Namibia alio kuwa nao wkt wa dhiki wamemzika kwa heshima!! na bado familia yake inatunzwa na kufarijiwa wewe Kagame kichwa km papai jifanye mjanja tu!!...unacheka??????

Kwanza mdogo wako Major Loraa Nkunda yuko wapi??? km siyo Kigali umemficha anakula bata?? huyu si ndo mliyeshirikiana naye kupora Mali za DRC Siyo?? ''The Haegue kaenda mwingineeee!!'''.....yaani.... au unadhani tumesahau? wewe ulimkamata Major kirahisi tu!! eti na kumzuia Rwanda .. ndo ika jiiii mpaka leo... wewe ulimkamata km nani?? kwa malipo yapi??

Mwisho Kagame!!! Nisikie uzuri navosema na ukumbuke Maneno yangu ''Mchuma janga hula na wa kwao!! sasa wewe unakula na hao Nefilims utaona cha moto . make kwa maksudi kabisa unacheza na moto!! unaoujua vyema! kifupi umeuza uhai hayaa!

yangu ni hayo ila huna mwisho mwema, hao kina Angela na urefu huo waandalie urithi Kabisaa!! sasa sijui wataulia wapi make wanajulikana Dunia nzima!........
 
Wakati wa utawala wa awamu ya nne , nchi yetu haikuwa na mahusiano mazuri na Rwanda, matokeo yake ni kwamba vitendo vya ukandamizaji kwa raia vilikuwa ni kidogo sana.

Alipoingia madarakani Rais John Magufuli, katika moja na hotuba zake alikiri kupewa ushauri na rais Kagame juu ya ununuzi wa ndege kwa cash, na nina uhakika alishauriwa na vingine pia.

Katika utawala huo wa John Magufuli, mahusiano ya nchi yetu na Rwanda yakaimalika, na hapo ndipo tukaanza kuona vitendo vya kutekana, kuuana, kupigana risasi, wapinzani kushughulikiwa nk

Juzi hapa IGP Sirro alitoka Rwanda bila aibu wakati akiongea na vyombo vya habari akatangaza kuanza kufuatilia yanayofundishwa kwenye nyumba za ibaada hasa Misikitini na Sunday School, kwa kigezo cha kwamba Rwanda wamefanikiwa sana kwenye njia hiyo ili kuzuia ugaidi.

Kwa kifupi ni kwamba, Jenerali Kagame, Jenerali Museveni na CCM ya Tanzania hawa ndiyo wanaunda utatu haramu ndani ya ukanda huu wa Africa Mashariki.

kwan ni uongo??? nchi nyingi zisizodhibiti dini zinaingia kwene machafuko lazma kuwe na mkono wa chuma kwa wale wanaotumia dini kisiasa au kutimiza azma zao chafu
 
Yote kwa yote!! wazungu wana slogan zao zinasema hivi ''Wao km wao!! hawana Rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu'' Huyo Kagame ajipange kwa matumizi tu, lkn iko siku yatamkuta km yaleeee!! ya

Savimbi wa angola dhidi ya Agostini Neto(mwenzake bado ala bata), Sadadam Hussein yuko wapi!! alitumiwa dhidi ya Ayatolah Khomein! Hissene Habre!! Idd Amini Dada, huyu aliandaliwa maksudi!! lkn akagutuka wkt alishakula vyao!!

so wazungu walimgeuka mbaya........ nyerere kaipata hii kuwa wamemgeuka ikawa fursa kwake so akampa kichapo kileee cha Lukaya!...... Juzijuzi hapa Mobutu aliipata hata hawakumtaka aende kutibiwa tu!! akafa km mbwa!!

Hao na wengine weeengi! sana walitumikia Mibeberu!! lkn walitoswa km hawajawahi tumika!!!! Nyerere alikataa kutumikia weupe kabisaaa!! akajiunga na ndg zake Frontline state!! alizikwa kwa heshima mpaka leo! Africa hii atakumbukwa mnooo!!

kIFUPI urafiki na Mweupe ukiwa km mkuu wa nchi hauna mwisho mwema, nakwambia!!! hii ni sheria ya Historia watakuendesha weee!! kwa faida yao! ipo siku utasema duuu nimekuwa sana Dikteta lkn ''hapa??? hapana sitaki!!

Hapo hapo ndo patamu wanakumaliza wao dakika sifuri km Saddam!! kivipi?? wanakuacha au kuongezea nguvu kwa adui yako! ....Sasa huyu kagame huyu???????? weee!!.... muache tu!! iko siku isiyo kuwa na tarehe atakufa kifo kibaya sana tena na hao hao!!

Weupe watamnyonga live!! sijui atamlilia nani???? Najua muheshimwa unapita pita humu! soma uelewe hii ikamate kabisaaa!! bora uwe na urafiki na ndg zako Africa, watakuhifadhi utaishi wanajua!! si unaona Mengistu Haile Maliamu anakula Bata kiulainiiii!!

Kaunda kazomewa weeee!! na chiluba huyo hapo!! walewale ndg zake wa south/Namibia alio kuwa nao wkt wa dhiki wamemzika kwa heshima!! na bado familia yake inatunzwa na kufarijiwa wewe Kagame kichwa km papai jifanye mjanja tu!!...unacheka??????

Kwanza mdogo wako Major Loraa Nkunda yuko wapi??? km siyo Kigali umemficha anakula bata?? huyu si ndo mliyeshirikiana naye kupora Mali za DRC Siyo?? ''The Haegue kaenda mwingineeee!!'''.....yaani.... au unadhani tumesahau? wewe ulimkamata Major kirahisi tu!! eti na kumzuia Rwanda .. ndo ika jiiii mpaka leo... wewe ulimkamata km nani?? kwa malipo yapi??

Mwisho Kagame!!! Nisikie uzuri navosema na ukumbuke Maneno yangu ''Mchuma janga hula na wa kwao!! sasa wewe unakula na hao Nefilims utaona cha moto . make kwa maksudi kabisa unacheza na moto!! unaoujua vyema! kifupi umeuza uhai hayaa!

yangu ni hayo ila huna mwisho mwema, hao kina Angela na urefu huo waandalie urithi Kabisaa!! sasa sijui wataulia wapi make wanajulikana Dunia nzima!........

nimecheka sana !! watz tuna uswahili sana !! siamini unavoongea kama unachamba mtu anakusikia
 
Back
Top Bottom