Kwanini Rwanda ndio kioo cha Watawala Afrika Mashariki na Kati?

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
775
1,117
Kumekuwa na Safari kadhaa kwa watawala na wakuu wa vikosi vya ulinzi katika nchi za afrika mashariki na Kati kwenda Rwanda. Ziara hizo bila ya shaka huwa zinabeba ajenda nyingi.

Ama kwanini Rwanda kioo na kigezo watawala na viongozi waandamizi katika serikali za afrika mashariki na Kati. imekuwa ni Rwanda kwasababu ya unyeti wake kimkakati kwa Mataifa ya kimagharibi katika ukanda huu wa afrika ya mshakariki na Kati. Na sababu za msingi ni hizi.

1. Mtawala wa nchi hiyo. Mtawala wa nchi ya Rwanda Paul Kagame ni zao la mashirika ya kijasusi ya America. Ifahamike kuwa kagame alilelewa katika mashirika hayo miezi 17 kabla ya Kuja kupewa nchi ya Rwanda ili atekeleze ajenda za wamagharibi na hasa Amerika katika ukanda wa afrika mashariki na Kati. Naam kazi hiyo kaifanya vyema sana na katika aliyoyafanikisha ni haya.

a. Kutengeneza njia nyepesi kwa wamagharibi Hasa Amerika kuchota Mali ya Kongo. Na hiyo ni kusimamia machafuko yote ndani ya kongo kwa kuingiza majeshi yake na kuchochea vita nchini humo.

2. Kuizamisha nchi ya Rwanda katika mfumo wa kibepari kwa asilimia Mia. Na kuyafanya maisha ya wanyarwanda Kuwa magumu kuliko sehemu yoyote katika ukanda wa afrika mashariki na kati. Imekuwa ni nchi ambayo kila kitu lazima kitolewe tozo. Raia wamekuwa wakitafuta Mali kwa ajili ya serikali na sio kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Wanyarandwa kula mlo mmoja kwa siku ni jambo la kawaida.

3. Kuwa muhimili mkubwa katika kubeba ya wamagharibi katika yale yanayoitwa mapambano dhidi ya ugaidi. Tumeiona Rwanda ikihudumu vyema katika ajenda hio katika muungano wa Amesom nchini Somalia na Sasa huko msumbiji.

Baada ya Rwanda kuwa mfanikishaji wa ajenda hizi nyeti katika ukanda huu, wamagharibi wakaienzi nchi hiyo kwa mengi. Kama vile kuanzisha baadhi ya viwanda katika nchi hiyo kama viwanda vya magari, simu na kiwanda kusafisha dhahabu. Na kuitangaza kuwa ni nchi inayokuwa kiuchumi kwa kasi kubwa kwa vipimo vya mabepari. Ili kuikuza zaidi kama zawadi ya kufanikisha ajenda zao.

Lakini pia wamagharibi wakamfumbia macho mtawala wa nchi hiyo Pauli kagame kwa mambo yote ya unyama anaoufanya katika nchi hiyo. Kwasababu ya utekelezaji wake mzuri wa kazi zao. Na kwakuwa raia wa Rwanda ni miongoni mwa watu duniani wanaoishi kwa mtutu wa bunduki. Hali hivyo imempelekea kiongozi huyo kuishi kwa tahadhari na khofu ya kupinduliwa. Tahadhari ya kiongozi kwa kupinduliwa imekuwa ni kubwa Sana kwake. Jambo ambalo limemfanya aje na mikakati kadhaa kupambana na kila anaetishia utawala wake na kuuokosoa. Na katika mikakati hiyo ni.

Kuzuia harakati za kidini kwa lengo la kulinda utawala wake. Tahadharini hiyo imemfanya adhibiti maeneo yote ambayo anaona ni hatarishi kwake. Na katika maeneo hayo ni sehemu za ibada misikitini na makanisani. Hilo likienda sambamba na yanayoitwa mpambano yanayoitwa ya ugaidi. Mpambano yanajulikana walengwa ni Waislamu.

Na ndipo alipoamua kuyafunga makanisa zaidi ya 8000 na misikiti miwili na kuweka makachero katika maeneo hayo kuratibu kila kinachofundishwa ili kudhibiti harakati za mapinduzi. Ufungaji wa makanisa ni khofu ya kupinduliwa na hiyo kutokana na wakristo kuwa wengi nchi humo na hawampendi. Kwani anajua wazi kuwa raia wa nchi hiyo hawana mapenzi nae hata kidogo kwani kawafukarisha Sana na kuitajirisha familia yake. Ama kuhusu misikiti ni ajenda dhidi ya kupambana na ugaidi (Uislamu)

Naona uigwaji unachukua nafasi kivitendo.

Haya ndio yanayoenda kuigwa na watawawala na viongozi waandamizi nchini Rwanda. Na baada ya kuchukua hayo ndio tunaambiwa Sasa hivi watu watapita katika msikiti na Madrasa kuangalia namna ya Waislamu wanavyofundisha Q'uran. Maana wao ndio wanajua zaidi namna ya kusomesha Q'uran na Uislamu vizuri kuliko Waislamu wenyewe. Tunasema ajenda ni Uislamu tu kwasababu aliesema maneno hayo ni mtu aliesomea upadri mwenye chuki ya wazi kwa Uislamu na Waislamu anajua kabisa yaliyomo kanisani hayana athari kwakuwa ni Dini ya kiroho tu. (spiritual religion ) kule ni misa, sadaka na mziki mnene. Rwanda ndio wakaoiga kuwaumiza watu na tozo katika kila kitu.

Ama Dini ya kiislamu ndio Dini lengwa kwasababu ni Dini ya kimfumo. Iliyojikamilisha katika nyanja zote maishani. Katika siasa, uchumi na jamii. Na ndio tishio la mfumo utawalao leo duniani ubepari. Kwa hivyo tunarajia kuona vyuo vikifungwa na watu wakibambikiziwa kesi za Ugaidi na kufilisiwa Mali zao.....

Ujumbe.
Ujumbe kwa Waislamu ni wajibu wenu kukamatana na Uislamu wenu bila ya kuogopa lawama za wenye kulaumu. Na hata kama ni kufa kwa ajili ya Uislamu wenu ni bora zaidi na ndio kifo bora zaidi kuliko vifo vyote. Na jitulizeni kutokana na maneno haya ya Allah.

(قُل لَّن یُصِیبَنَاۤ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡیَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ)
[Surat At-Tawbah 51]
"Hayatufiki sisi isipokuwa yale aliyopanga Allah yeye ndio Mola wetu na kwa Allah wategemee waumini"

Ama kwa wenye chuki na Uislamu tunawaambia wao sio wa mwanzo wamepita wengi lakini wameicha Dini ikizidi kuenea kwa kasi, pamoja na vigingi vingi inavyokutana navyo. Na kubwa wafanye wafanyavyo wote tunakufa na huenda dhalimu akafa kabla ya mdhulumiwa. Wamepita wengi walionyesha uadui wao dhidi ya Uislam lakini imebaki historia tu. Allah anasema

(وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَـٰفِلًا عَمَّا یَعۡمَلُ ٱلظَّـٰلِمُونَۚ إِنَّمَا یُؤَخِّرُهُمۡ لِیَوۡمࣲ تَشۡخَصُ فِیهِ ٱلۡأَبۡصَـٰرُ)
[Surat Ibrahim 42]

"Wala msidhani kuwa Allah amesahau yale wanayoyafanya madhalimu hakika anawachelewesha mpaka katika Siku zikazozongwa nyoyo na macho"

Hakuna aliewaiga Rwanda kibaraka kiongozi wa wamagharibi isipokuwa atawaumiza raia zake.
 
Kagame ni dikteta katili anayejua kutengeneza propoganda na kucheza vizuri na vyombo vya habari
 
Rwanda ni nchi ndogo sana kuliko mkoa wa Tabora. Walipata shamba la bibi Congo wakalitumia ipasavyo. Sisi hatuna shamba. Wale wana propaganda nyingi na hawana vyombo huru vya kujua habari zao na ukweli halisi hasa vijijini. Ni nchi masikini sana. Viongozi unaosema wanakimbilia huko kujifunza ni kwa sababu ya uvivu wao wa kufikiri. Ati wanaenda Rwanda kijifunza usafi, really? Kina Sirro wanaenda kijifunza jinsi ya kutesa watu wao na kulinda utawala dhalimu wala hakina kingine. Vinginevyo wangeenda USA, UK nk kujifunza utawala, amani, maendeleo, kilimo bora, viwanda, mpira, nk nk.
 
Ni viongozi gani wa vyombo vya ulinzi na usalama na kutoka nchi gani wamekuwa wakikimbizana kwenda Rwanda? Navyojua kwa hapa kwetu wao ndio walikuwa wa kwanza kuja bila shaka ni baada ya kupata mualiko na baadae wao wakawaalika wenzao waende kwao lakini naona kama jambo limegeuzwa sijui kwa maslahi gani!
 
Mleta Mada kasimama upande wa kukosoa sana, kagame kabla ya kwenda kusoma ujasusi mbele alianza kusoma mafunzo ya kijeshi Tanzania.hilo watu hawasemi hata kidogo
 
Upo sahihi kule Ni kijifunza kutesa na kuuwa watu. Uwezi kwenda kijifunza kutoka kwa wauwaji
 
Mleta Mada kasimama upande wa kukosoa sana, kagame kabla ya kwenda kusoma ujasusi mbele alianza kusoma mafunzo ya kijeshi Tanzania.hilo watu hawasemi hata kidogo
Sikuwa nalijua hilo na ndio maana sikulisema
 
Ni viongozi gani wa vyombo vya ulinzi na usalama na kutoka nchi gani wamekuwa wakikimbizana kwenda Rwanda? Navyojua kwa hapa kwetu wao ndio walikuwa wa kwanza kuja bila shaka ni baada ya kupata mualiko na baadae wao wakawaalika wenzao waende kwao lakini naona kama jambo limegeuzwa sijui kwa maslahi gani!
Bila shaka utakua unafurahia ukandwamizaji wa elimu ya dini ya kiislam
 
Mleta Mada kasimama upande wa kukosoa sana, kagame kabla ya kwenda kusoma ujasusi mbele alianza kusoma mafunzo ya kijeshi Tanzania.hilo watu hawasemi hata kidogo
Uyo kagame amesomea mafunzo ya TISS psle morogoro hana lolote uyo yy mwenyewe kagame anaijua TZ vzr ndoma anaogopa kuingizs chokochoko zake hapa kama anavyofanta Congo.
 
Kwenye swala la dini umezingua mzee.. Kagame ameona dini zinatumika vibaya huo uislamu bila waarabu kuja kuwatoboa miguu Babu zetu msinge ujua yani kama ulivyo ukristo Tu kimsingi kila MTU aishi maisha yake.. hizi dini zimeirudisha Sana Afrika nyuma Kwa kuwa brain washed to the extent mpaka Mungu mwenyewe anashangaa yani..

So hakuna cha uislam wala ukristo.. fainali mbinguni ukijikuta unashika mtutu utatangulia huko ambako Hamna mwenye uhakika kama kupo au hakupo
emoji23.png

Hahahaha
 
Back
Top Bottom