Kwanini Rwanda ndio kioo cha Watawala Afrika Mashariki na Kati?

Amigoh

JF-Expert Member
May 15, 2016
853
1,000
Halafu kioo cha watawala Afrika mashariki na Kati ni Tanzania mkuu.. asikudanganye MTU
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
13,563
2,000
Rwanda ni nchi ndogo sana kuliko mkoa wa Tabora. Walipata shamba la bibi Congo wakalitumia ipasavyo. Sisi hatuna shamba. Wale wana propaganda nyingi na hawana vyombo huru vya kujua habari zao na ukweli halisi hasa vijijini. Ni nchi masikini sana. Viongozi unaosema wanakimbilia huko kujifunza ni kwa sababu ya uvivu wao wa kufikiri. Ati wanaenda Rwanda kijifunza usafi, really? Kina Sirro wanaenda kijifunza jinsi ya kutesa watu wao na kulinda utawala dhalimu wala hakina kingine. Vinginevyo wangeenda USA, UK nk kujifunza utawala, amani, maendeleo, kilimo bora, viwanda, mpira, nk nk.
Huo ndio ukweriiii 100% ndugu zangu.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,994
2,000
Rafiki yangu architect alipata kazi Scotland, alipelekwa Rwanda miaka minne, kampuni yao ilipata contract ya kubuni na kujenga majengo ya serikali.

Kila anochofanya Kagame ana lenga miaka 100 ijayo.
 

James H

Member
May 7, 2021
36
95
Kumekuwa na Safari kadhaa kwa watawala na wakuu wa vikosi vya ulinzi katika nchi za afrika mashariki na Kati kwenda Rwanda. Ziara hizo bila ya shaka huwa zinabeba ajenda nyingi.

Ama kwanini Rwanda kioo na kigezo watawala na viongozi waandamizi katika serikali za afrika mashariki na Kati. imekuwa ni Rwanda kwasababu ya unyeti wake kimkakati kwa Mataifa ya kimagharibi katika ukanda huu wa afrika ya mshakariki na Kati. Na sababu za msingi ni hizi.

1. Mtawala wa nchi hiyo. Mtawala wa nchi ya Rwanda Paul Kagame ni zao la mashirika ya kijasusi ya America. Ifahamike kuwa kagame alilelewa katika mashirika hayo miezi 17 kabla ya Kuja kupewa nchi ya Rwanda ili atekeleze ajenda za wamagharibi na hasa Amerika katika ukanda wa afrika mashariki na Kati. Naam kazi hiyo kaifanya vyema sana na katika aliyoyafanikisha ni haya.

a. Kutengeneza njia nyepesi kwa wamagharibi Hasa Amerika kuchota Mali ya Kongo. Na hiyo ni kusimamia machafuko yote ndani ya kongo kwa kuingiza majeshi yake na kuchochea vita nchini humo.

2. Kuizamisha nchi ya Rwanda katika mfumo wa kibepari kwa asilimia Mia. Na kuyafanya maisha ya wanyarwanda Kuwa magumu kuliko sehemu yoyote katika ukanda wa afrika mashariki na kati. Imekuwa ni nchi ambayo kila kitu lazima kitolewe tozo. Raia wamekuwa wakitafuta Mali kwa ajili ya serikali na sio kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Wanyarandwa kula mlo mmoja kwa siku ni jambo la kawaida.

3. Kuwa muhimili mkubwa katika kubeba ya wamagharibi katika yale yanayoitwa mapambano dhidi ya ugaidi. Tumeiona Rwanda ikihudumu vyema katika ajenda hio katika muungano wa Amesom nchini Somalia na Sasa huko msumbiji.

Baada ya Rwanda kuwa mfanikishaji wa ajenda hizi nyeti katika ukanda huu, wamagharibi wakaienzi nchi hiyo kwa mengi. Kama vile kuanzisha baadhi ya viwanda katika nchi hiyo kama viwanda vya magari, simu na kiwanda kusafisha dhahabu. Na kuitangaza kuwa ni nchi inayokuwa kiuchumi kwa kasi kubwa kwa vipimo vya mabepari. Ili kuikuza zaidi kama zawadi ya kufanikisha ajenda zao.

Lakini pia wamagharibi wakamfumbia macho mtawala wa nchi hiyo Pauli kagame kwa mambo yote ya unyama anaoufanya katika nchi hiyo. Kwasababu ya utekelezaji wake mzuri wa kazi zao. Na kwakuwa raia wa Rwanda ni miongoni mwa watu duniani wanaoishi kwa mtutu wa bunduki. Hali hivyo imempelekea kiongozi huyo kuishi kwa tahadhari na khofu ya kupinduliwa. Tahadhari ya kiongozi kwa kupinduliwa imekuwa ni kubwa Sana kwake. Jambo ambalo limemfanya aje na mikakati kadhaa kupambana na kila anaetishia utawala wake na kuuokosoa. Na katika mikakati hiyo ni.

Kuzuia harakati za kidini kwa lengo la kulinda utawala wake. Tahadharini hiyo imemfanya adhibiti maeneo yote ambayo anaona ni hatarishi kwake. Na katika maeneo hayo ni sehemu za ibada misikitini na makanisani. Hilo likienda sambamba na yanayoitwa mpambano yanayoitwa ya ugaidi. Mpambano yanajulikana walengwa ni Waislamu.

Na ndipo alipoamua kuyafunga makanisa zaidi ya 8000 na misikiti miwili na kuweka makachero katika maeneo hayo kuratibu kila kinachofundishwa ili kudhibiti harakati za mapinduzi. Ufungaji wa makanisa ni khofu ya kupinduliwa na hiyo kutokana na wakristo kuwa wengi nchi humo na hawampendi. Kwani anajua wazi kuwa raia wa nchi hiyo hawana mapenzi nae hata kidogo kwani kawafukarisha Sana na kuitajirisha familia yake. Ama kuhusu misikiti ni ajenda dhidi ya kupambana na ugaidi (Uislamu)

Naona uigwaji unachukua nafasi kivitendo.

Haya ndio yanayoenda kuigwa na watawawala na viongozi waandamizi nchini Rwanda. Na baada ya kuchukua hayo ndio tunaambiwa Sasa hivi watu watapita katika msikiti na Madrasa kuangalia namna ya Waislamu wanavyofundisha Q'uran. Maana wao ndio wanajua zaidi namna ya kusomesha Q'uran na Uislamu vizuri kuliko Waislamu wenyewe. Tunasema ajenda ni Uislamu tu kwasababu aliesema maneno hayo ni mtu aliesomea upadri mwenye chuki ya wazi kwa Uislamu na Waislamu anajua kabisa yaliyomo kanisani hayana athari kwakuwa ni Dini ya kiroho tu. (spiritual religion ) kule ni misa, sadaka na mziki mnene. Rwanda ndio wakaoiga kuwaumiza watu na tozo katika kila kitu.

Ama Dini ya kiislamu ndio Dini lengwa kwasababu ni Dini ya kimfumo. Iliyojikamilisha katika nyanja zote maishani. Katika siasa, uchumi na jamii. Na ndio tishio la mfumo utawalao leo duniani ubepari. Kwa hivyo tunarajia kuona vyuo vikifungwa na watu wakibambikiziwa kesi za Ugaidi na kufilisiwa Mali zao.....

Ujumbe.
Ujumbe kwa Waislamu ni wajibu wenu kukamatana na Uislamu wenu bila ya kuogopa lawama za wenye kulaumu. Na hata kama ni kufa kwa ajili ya Uislamu wenu ni bora zaidi na ndio kifo bora zaidi kuliko vifo vyote. Na jitulizeni kutokana na maneno haya ya Allah.

(قُل لَّن یُصِیبَنَاۤ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡیَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ)
[Surat At-Tawbah 51]
"Hayatufiki sisi isipokuwa yale aliyopanga Allah yeye ndio Mola wetu na kwa Allah wategemee waumini"

Ama kwa wenye chuki na Uislamu tunawaambia wao sio wa mwanzo wamepita wengi lakini wameicha Dini ikizidi kuenea kwa kasi, pamoja na vigingi vingi inavyokutana navyo. Na kubwa wafanye wafanyavyo wote tunakufa na huenda dhalimu akafa kabla ya mdhulumiwa. Wamepita wengi walionyesha uadui wao dhidi ya Uislam lakini imebaki historia tu. Allah anasema

(وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَـٰفِلًا عَمَّا یَعۡمَلُ ٱلظَّـٰلِمُونَۚ إِنَّمَا یُؤَخِّرُهُمۡ لِیَوۡمࣲ تَشۡخَصُ فِیهِ ٱلۡأَبۡصَـٰرُ)
[Surat Ibrahim 42]

"Wala msidhani kuwa Allah amesahau yale wanayoyafanya madhalimu hakika anawachelewesha mpaka katika Siku zikazozongwa nyoyo na macho"

Hakuna aliewaiga Rwanda kibaraka kiongozi wa wamagharibi isipokuwa atawaumiza raia zake.
Hakuna cha kujifunza kutoka kwa kagame, labda kuiga laana aliyonayo ya mauwaji tu
 

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
8,636
2,000
Sisi wenyeji wa karagwe, kyerwa na ngara mkoani kagera ndo tunawafahamu wanyarwanda vzr.

Ni maskini mno wale watu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom