Kwanini Russia hataki kuwekeza kwenye Aircraft Carrier kama USA?

Jamani tuendeleeni tulipoishia huyu chizi 1 tuachane nae habaki kama anavyojua maana huyu inaonekana ubishi ni hasiri yake
 
Maandazi kabisa kwaio Helicopter ni water craft?
IMG_20210113_132537.jpg

Unaongelea water craft kama hii hapa?..
 
We chizi acha upimbi kubisha kila kitu, unaonekana kabisa dish limeyumba kwa akili izo una haki ya kutomiliki hata paka pimbi wewe.ushashiba ubwabwa wa shemeji unakuja kutusumbua
Mwanzo nilidhani kwamba wew ni mjinga, ila sasa nimegundua wewe ni mpumbavu
 
Russia ni power inayodidimia,inazidi kuachwa nyuma kiteknolojia.
Kivipi? Kwamba wao hawajui hatari?

Russia kwenye Vita kwanza elewa kawekeza sana kwenye vita kubwa kuliko huzi Ragional Conflict.

Na ndo maana yeye ni kiongozi kwenye siraha za masafa marefu na makombola ya masafa marefu na ya hatari sana.

Techinolojia ya Murusi ni ya kupekee na ina last kwa karine ba karine.
 
Uzi mzuri sana huu, sema tunapoingiza ushabiki tunaharibu hoja.
Yani uzi umejaa sana ushabiki huu.eti mtu anakuja mbele za watu anakwambia Urusi hana uwezo wa kutengeneza Aircraft carrier.huu si utani huu jamani kwani kwenye Aircraft carrier kuna nini cha ajabu pale.hata Tanzania tukiamua kutengeneza wala hatuwezi kushindwa maana ile sio siraha bali ni uwanja
 
Kuna sababu nyingi kwanini Russia haina Aircraft carrier nyingi kama USA, Sababu zake zina mizizi milefu ambayo ilikuwapo kabla hata ya Russia ya sasa yani zilikuwapo tangu kipindi cha USSR, Soviet Union ilikuwa na uchu wa kutaka kuwa na jeshi kubwa la majini lakini kuna vikwazo vingi vilivyo zuia jitihada hizo na vikwazo hivyoviyvo ndio vilivyolithiwa na Russia ya sasa.
Russia mpaka sasa ina Aircraft carrier moja tu inayofanyakazi ambayo ni Admiral Kuznetsov, hii ilianza kutumika mwaka 1990, na zilitakiwa ziwe mbili lakini moja haikufanikiwa kumalizika na ilitelekezwa baada ya kuvunjika Umoja wa Kisoviete, ilikuwa chuma chakavu mpaka China ilipo inunua kutoka Ukraine mwaka 1998, hii ndio imekuja kuwa Liaoning, Na hata hiyo moja iliyo baki bado haina uwezo wowote wa kivita bali ni mkangafu tu, moja ya operation yake inayo kumbukwa ni ile ya Syria ya mwaka 2016 ambapo kelele za vyombo vya habari vya Russia viliipamba wakati wa operation hiyo na hakukuwa na matokeo yeyote katika uwanja wa vita zaidi ya kupoteza ndege mbili kwenye operation hiyo na tangu tarehe 15 Oktoba 2016 wakati ikiwa inatoka Kola bay, mwanzoni kabisa wa operation hiyo Kuznetsov ilionesha kutokuwa na imani na utengemavu wake ambapo ilibidi iongozane na na meli zingine saba (7) za kijeshi ikiwemo Pyotr Velikiy hii ni battlecruiser inayotumia nuclear kama chanzo kikuu cha nishati, pia iliongozana na Udaloy-class destroyers mbili swala ambalo ni la kawaida kwa Aircraft carrier kuongozana na kundi kama hili lakini uwepo wa Tugboat ulionesha hakuna ukawaida bali kuna chombo kibovu kinachotiliwa shaka kwa maana kazi kubwa ya Tugboat ni sawa na za gari za Breakdown yani kuvuta meli mbovu. Tangu iliporudi kutoka kwenye kampeni ya Syria mpaka sasa Admiral Kuznetsov ipo tu inafanyiwa ukarabati na si combat ready hii inaonesha wazi kuwa Russia haiwezi kumudu gharama za kukarabati kikamilifu vyombo vikubwa kama Aircraft carrier maana kuna nyingine ambazo zilitelekezwa bila ya ukarabati hadi kufikia hatua ya kuwa decommissioned.
Zipo sababu nyingi za Russia kushindwa kufikia malengo ya kuwa na jeshi kubwa la majini lenye Aircraft carrier nyingi, kwa mimi binafsi nahisi ni kama zifuatazo;

Kwanza kabisa Russia haina nguvu za kiviwanda, hakuna assembly line za kuaccommodate miradi mikubwa kama ya kuunda aircraft carrier na kama ina mpango wa kumiliki kwa wingi nyambizi hizi inapaswa kuagiza kwa nchi kama china au counterpart wake USA, ukilinganisha na uweza wa marekani kwenye nguvu za kiviwanda au China ya sasa, na hii hoja inadhihilishwa wazi kipindi cha WW2 USA ilikuwa inauza siraha na mahitaji ya vita kwa nchi zote za Allied forces mpaka Russia yenyewe na Marekani iliisaidia sana Russia kwenye vita hii, Henry Tzard aliona ni bora kukabidhi kwa USA vumbuzi zote za kivita na sayansi za Uingereza ili tu iweze kutumia Assembly line za USA. Kama ulikuwa haujui, jumla ya Ammunitions ambazo USA ilizarisha katika kipindi cha 1943 mpaka 1945 zinaweza kutokemeza population ya sasa ya dunia mara 11 net.

Pili mazingira ya kijiografia, Russia haijazungukwa na maji mengi kama ilivyo USA, na hata sehemu zenye maji bado hazipo kwenye tension ya kufanyikia vita yani sio sehemu za kimikakati ya kivita hususani eneo la bahari ya Arctic ambalo sehemu kubwa ni polar kiasi kwamba hata Aircraft carriers zinaweza kupata changamoto nyingi na kiuchumi ns ufanisi si salama kuoperate hizi meli kwenye barafu ngumu na nene kama za Arctic, Arctic Ocean huwa ni sehemu Russia inaogopa sana kushambuliwa lakini kimkakati si sehemu tishio kama inavyodhani. Admiral Kuznetsov ni moja ya vessels zinazounda Arctic Fleet maarufu kama Red Banner Northern Fleet ambayo kwa sasa inajulikana kama White Sea Flotilla, Ukiacha Finnish blokade kwenye kikosi cha Petsamo kipindi cha Winter War ya 1939 na 1940, engagement nyingi za kamandi hii huwa zinatokea Atlantic ocean hii inamaana kimikakati eneo kubwa la maji yanayo pakana na Russia si tishio kiasi cha kuhitaji kuwa na Aircraft carrier nyingi, kitu ambacho ni tofauti kwa USA ambae anapaswa kujirinda katika bahari ya Pacific sehemu ambayo haina historia nzuri kwenye vita, hii ni sehemu ya kimkakati sana kwa USA kwenye kurinda masilahi yake kwenye nchi za Asia lakini pia kurinda pwani ya magharibi (west coast) United States Indo-Pacific Command (USINDOPACOM) zamani United States Pacific Command (USPACOM) ina jukumu la kurinda zaidi ya maili milioni mia moja (100) za mlaba hii ni sawa na asilimia 52 ya eneo lote la uso wa Dunia.

Tatu, Russia anaoneka kuvutiwa sana kwenye kuwa na nguvu za ardhini yaani land powers, hii ni kutokana na mahusiano na nchi anazopakana nazo, na historia ya vita za nyuma, ukiacha Russo Japanese war 1904-1905, Vita nyingine zote za Russia kama WW1 and WW2 uwanja wa vita ulikuwa ni main land ya Russia, Kwa sasa Russia inahisi maeneo hatari ni mipaka inayo pakana na nchi za kibeberu sanasana Ulaya ya magharibi ambapo nchi nyingi inapakana nazo kwa ardhi.

Nne Russia, imewekeza sana kwenye ballistic missile na nyingi ni intercontinental long-range missles mfano mzuri ni makombora aina ya РС-28 Сармат yanayo julikana na NATO kama SS-X-29 au SS-X-30 haya ya operational range ya zaidi ya kilomita 18,000 na yana kasi ya zaidi ya mara ishirini (20) ya sauti yani Mach 20.7 sawa nazaidi ya kilomita 7 kwa sekunde, makombora ya hivi yanadhihirisha wazi kuwa hakuna haja ya kuwa na platform kama Aircraft carrier ili kumsogelea adui kwa maana yana uwezo wakufika mahala popote hapa duniani.

Hata hivyo Russia bado ina nia ya kuendereza mpango wake kupanua vikosi vya majini hii ni pomoja na kuwepo kwa mpango ulio vunjika wa kununua Aircraft carrier mbili kutoka Ufaransa ambapo Ufaransa iliasitisha mazungumzo hayo baada ya Russia kuvamia visiwa vya Crimea, Pia Russia ina mpango wa kumiliki Aircraft carrier sita (6) ifikapo 2025 japokuwa si mpango wa kuaminika kwani Russia imejawa na siasa na propaganda za kikomunisti ambazo huwa si rafiki kwenye uvumbuzi wa mambo ya kivita kwa kuwa watu binafsi hawapo huru kufanya tafiti za kivita kwa lengo la kuja kuizia serikali, jambo ambalo ni tofauti kwa Marekani ambao wao wanasoko huria na kila mtu anaweza kuiuzia serikali ubunifu au uvumbuzi wowote wenye lengo la kuboresha nguvu za kijeshi za nchi.​
Mkuu uko sahihi zaidi kuliko comments zote nilizosoma. Watu wengine wanaleta ushabiki kwenye uhalisia
 
Tuongea kidogo kuhusu Aircraft carrier. Ni kwamba kuna vitu viwili air( hewa) and craft ( skill, ability, uwezo). Carrier( uwezo wakubeba).

Ni hivi aircraft ni kifaa chochote kinachoweza kuruka kutumia engine na upepo.

Ukitumia nguvu ya upepo kupaa na màarifa yako (engine) you are aircraft.

Tofauti ya aeroplane na helicopter is very simple. Normal plane their wing stay fixed while helicopter rotate.
 
Halafu kuna airplanes ndogo kuliko helicopters. Powerful hellcopters kuliko small planes.

Many effective hellicopters than planes.
 
Icnonito tz is techically right, while mohamed is also right on what he is thinking regarding only airplane ( fighters, bombers etc)
 
Yani uzi umejaa sana ushabiki huu.eti mtu anakuja mbele za watu anakwambia Urusi hana uwezo wa kutengeneza Aircraft carrier.huu si utani huu jamani kwani kwenye Aircraft carrier kuna nini cha ajabu pale.hata Tanzania tukiamua kutengeneza wala hatuwezi kushindwa maana ile sio siraha bali ni uwanja
Urusi kwa sasa hana uwezo wa kutengeneza aircraft carrier. Usije dhani yale ni mavyuma tu wanaunganisha, ona US wana Ford class yao ya kwanza imetumia dola bilioni 13 lakini hadi leo haina weapons systems miaka zaidi ya mitatu tangu ikamilike. Walikuwa na stealth Zumwalt destroyers nazo zilikaa sana hazina effective weapons. Na hii ni nchi yenye aircraft carriers 10 zikiwemo Nimitz kubwa zaidi kuliko kina HMS Queen Elizabeth, Admiral Kuznetsov, Liaoning, Vikramaditya na nyingine.

Military industrial complex ya Soviet Union ilikuwa imegawanywa kwamba meli zinatengenezwa Ukraine. Wao Ukraine mpaka ile 2014 ndio walikuwa wanaiuzia Russia steam engine na gas engine kubwa za kuendeshea meli za kivita. Crimea ilipotwaliwa kulikuwa na order zikakatishwa. Kama Russia ana teknolojia ya meli kubwa za kivita, kwanini alinunua Mistral mbili kutoka Ufaransa. Tena kwenye mkataba kuna maelezo kuwa nyingine order zitatengenezwa Russia na watapewa baadhi ya tech. Kwanini NATO ilikataa mkataba huo?

Shipyards za USC, Sevmash (wazuri sana kwa submarines), Admiralty shipyard, Zvezda ambao ni wakubwa hawana uwezo wa kujenga carrier yenye kuhitaji resources nyingi sana na experience kubwa.

Kuna mtu kalinganisha icebreaker na mapichapicha kibao hapo juu kuonesha uwezo wa kujenga meli kubwa. Huwezi linganisha dude linalotembea tu baharini likipasua barafu dhidi ya meli ya kisasa yenye ulinzi na kushambulia. Yani kwa vile Massey Ferguson na John Deere wanatengeneza trekta basi utataka udhani wanaweza kifaru.
 
Urusi kwa sasa hana uwezo wa kutengeneza aircraft carrier. Usije dhani yale ni mavyuma tu wanaunganisha, ona US wana Ford class yao ya kwanza imetumia dola bilioni 13 lakini hadi leo haina weapons systems miaka zaidi ya mitatu tangu ikamilike. Walikuwa na stealth Zumwalt destroyers nazo zilikaa sana hazina effective weapons. Na hii ni nchi yenye aircraft carriers 10 zikiwemo Nimitz kubwa zaidi kuliko kina HMS Queen Elizabeth, Admiral Kuznetsov, Liaoning, Vikramaditya na nyingine.

Military industrial complex ya Soviet Union ilikuwa imegawanywa kwamba meli zinatengenezwa Ukraine. Wao Ukraine mpaka ile 2014 ndio walikuwa wanaiuzia Russia steam engine na gas engine kubwa za kuendeshea meli za kivita. Crimea ilipotwaliwa kulikuwa na order zikakatishwa. Kama Russia ana teknolojia ya meli kubwa za kivita, kwanini alinunua Mistral mbili kutoka Ufaransa. Tena kwenye mkataba kuna maelezo kuwa nyingine order zitatengenezwa Russia na watapewa baadhi ya tech. Kwanini NATO ilikataa mkataba huo?

Shipyards za USC, Sevmash (wazuri sana kwa submarines), Admiralty shipyard, Zvezda ambao ni wakubwa hawana uwezo wa kujenga carrier yenye kuhitaji resources nyingi sana na experience kubwa.

Kuna mtu kalinganisha icebreaker na mapichapicha kibao hapo juu kuonesha uwezo wa kujenga meli kubwa. Huwezi linganisha dude linalotembea tu baharini likipasua barafu dhidi ya meli ya kisasa yenye ulinzi na kushambulia. Yani kwa vile Massey Ferguson na John Deere wanatengeneza trekta basi utataka udhani wanaweza kifaru.
Ndugu kiukweli unaferi ile mbaya.kwa iyo nuclear ice breaker na iyo aircraft carrier ipi ni technolojia rahisi ndugu maana naona kama vile umeizarau Ice breaker.kifupi ni kwamba hakuna kitu amacho marekani atatengeneza alafu urusi hasiweze kutenveneza, icho kitu kwa duniani kiukweli hakuna ndugu.

Kazi kubwa ya iyo Aircraft carrier ni kubeba ndege na kuzirusha wala hakuna kazi nyingine tofauti na iyo ndugu, sasa kwa Urusi yeye hana umuhimu wa kubeba ndege na kuzunguka nayo baharini.msilazimishe kitu kuonekana muhimu wakati kiukweli wala hakina umuhimu kwa mataifa makubwa
 
Back
Top Bottom