Kwanini Russia hataki kuwekeza kwenye Aircraft Carrier kama USA?

Zinaitwa TORPEDO/TORPEDOES.

Kuhusu hizo Torpedoes tayari nimekwisha ku-Address ama kulitolea ufafanuzi.

Moja ya jukumu kubwa la Battle Group ni kuhakikisha hayo yote uliyoyasema yanashughulikiwa.

Kuna vitu kama Electronic Warfare bila kusahau Anti-Submarine Warfare ambapo tayari uwekezaji mkubwa umefanyika hapo na kuhakikisha kuwa masuala mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mashambulizi kama hayo hususani kupitia Submarines yanadhibitiwa.
Likewise,huku wewe ukija na carrier,wenzako nao wanajua jinsi ya kufanya counter attack. Inakua rahisi kuleta hayo madubwana kwa nchi dhaifu tu. Lakini huwez kusema unaanzisha vita na Russia halafu eti upeleke Carrier hizo. Kwa sasa US huzitumia kwa hawa wadogo na kuwatisha ila kwa Russia haiwezekani zikapelekwa eti akapigane na Urusi vita kamili this shall never happen na wala room hiyo HAITAKUWEPO.
 
Ukiwa na hela huwezi kuogopa kununua gari zuri kiss eti litapata ajali... Russia hana hela ya kuendesha huo mtambo
Sio kwamba Russia hawezi kuendesha tu huo mtambo/ kutumia hiyo mitambo yaani aircraft carrier .Bali Russia anaweza kutengeneza/ kinda,anazo alisaunda na nyingine iko jikoni.Namaanisha kusema technolojia ya kuzalisha AC anayo kubwa tu.je ni hitajio kwake? Sio kill silaha aliyonayo USA ni lazima Russ awe nayo au kinyume chake.Warusi wao walishatoa sbb kwa Nini hawahitati AC nyingi kijeshi,kisiasa,kiuchumi na kiteknolojia
-Kijeshi- wanna silaha za kufika mbali mbadala wa AC
-kisiasa- hawana mpago wa kuzitawala/kuzivamia nchi za mbali Kama US
-kiuchumi-ni hasara kuzitunza hamna faida kwa mda huu,ikitokea Vita na wakubwa wenza zanabutuliwa kirahisi tu na kuleta maafa ya kimbali Kama sio ya halaiki
-kiteknolojia-kadri siku zinavyokwenda teknolojia ya kuzipiga inakuja kwa kasi Sana tofauti na zamani Hadi sasa China wameshapata Aircraft carrier killer,Urusi anazo tangu zamani na anaendelea kuboresha na kuja na vitu vipya vys kuziua AC.
Sio kwamba Urudi Hana kabisa AC,anazo moja au mbili nadhani.
 
Lakini mbona sasa hivi Russia ina tengeneza manuari za kubeba ndege mbili kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba ndege 75 za kivita na zina uwezo wa kurusha ndege 5 kwa wakati mmoja kila baada ya dakika 5 na zitakamilika mwaka 2023?
Watu wengi huwa ni "wajinga Sana" hawataki kujielimisha,Mimi huwa swaelewi,je wait wanaaminje? kua Urusi hawezi tengeneza Carriers au Hana hela ya kuzitengeneza?
Kama an technology ya kutengeneza Basi yupo vizuri
Lkn Kama Hana tech hiyo ndio shida sasa.
Kutoka na hila sio ishu,hell intafutwa,ishu ni kutoka na tech.
Sasa HIV Russ wamesnza kuwa na hell za kuendesha miradi mikubwa Kama Zama za USSR ndo maana tunona wakija na zana mpya kill siku.
 
Vita kubwa ni Vita inayo weza kihusisha Powerful countries, mfano China, Russia na Usa, hawa sio tu Silaha za atamizi bali pia wana kila aina ya silaha za hatari kabisa ambazo kamwe hazowezi fanya vita kuwa rahisi.

Na ndo nikasema hizo Carrier sio kwa vita kati ya USA na RUSSIA.
Sawa kabisa Vita kubwa ipo na Vita ndogo zipo.
Huwezi pingana na watalaban,Al shabab,isis, watu wanaotumia bunduki tu,halafu wewe ukawapelekea aircraft carier ukajiona wewe supapawa.
Kiduku tu kazipiga biti hizo Air Carriers zikapiga U turn.
 
Kipindi cha cold war, wakati USA anainvest kwenye kumodernise Nuclear Warheads zake yeye Russia aliamua kuproduce Nuclear Warheads nyingi zaidi. Ina maana US akawa anazo chache advanced lakinj Mrusi akawa na nyingi za kawaida!, bado haingeweza kufanya nani ashindwe sababu ilikuwa hakuna mshindi anayebakia.
Mwaka huu tu Wachambuzi wa masuala ya Ulinzi US wakafanya Simulation kuangalia jinsi gani hii vita itaamulika bado wanaona Mrusi akiingia vitani anaenda imaliza Ulaya nzima kabla hajaenda US hiyo yote akitokea Moscow!.
Aircraft Carrier sio uwanja mzuri kuutumia kwa nchi kama Russia na China labda kwa North Korea na sisi nchi za tatu huku. Kule zitazamishwa na nyumbani patapigwa tu.
Kumbukeni Russia hajasaini First Strike Policy, kwake kutumia Nuclear ni kugusa tu!.
 
Hahaaaa Mkuu kuna silaha za kuzamisha Carrier na zinabebwa na either Nyambizi au Ndege au meli. Kwa kifupi jua labisa China na Russia wana makombola ya kuweza kuazamisha carrier
Kitu pekee duniani chenye chance ya kuifikia carrier kwa sasa na kuleta damage sio kuizamisha ni ‘Zircon Missles’ na kwa sababu ya speed tu.

Hata hizo Zircon kufikia carrier kama Gerald Ford inahitaji kupita system nne tofauti za defence ambazo zote ngumu na ya mwisho ni laser iliyopo kwenye meli sasa sijui kitu gani unakijua kina speed kushinda laser.

Na majini alikadhalika stealth submarine zitabaki kuwa ivyo at low speed, hizi carrier za kisasa zipo powered na nuclear energy, kwenye Gerald Ford wanadai electricity produced on that ship is enough to power New York City kwa ivyo hilo dude linazalisa energy ya kuweza kuikimbiza mno. Submarine yoyote iliyo stealth kwenda nayo sambamba lazima itatoa sauti ambazo sonar devices will detect them.

Ni hivi hizo meli wahusika wanafikiria kila kitu.
 
Kwenye kamati iliyoundwa na Bunge la Congress kuiangalia budget ya trump kwenye ulinzi, jamaa walikuja na jibu moja tu.
Kwenye vita kati ya US-China au US-Russia zote USA atapigwa vibaya, hakuna eneo anapoweza furukuta!!..
Taarifa nyeti kama hiz za mamabo ya kiusalama kwa taifa kubwa kama usa huwa naona zinatumika ili kuwa mislead hawa washindani wao.Huwa nahis hivyo binafsi.
Huwez ku publicise taarifa nyeti namna hiyo.
Ni kama ile memo ya Bwwana Pompeo ilisomeka kama bahat mbaya kwa wana habari kusema "5000 troops to columbia" (somethinf like dat kama sijakosea) wakat wa choko choko za venezuela zikiendelea.mkijichanganya tu china na russia kuzifanyia kazi andiken mmeumia
 
Bahari ilizo izunguka Russia na hari ya hewa yake ni disadvantage(hasara) kwa Urusi. Urusi kasikazini imepakana na bahari ya Arctic(barafu tupu), Mashariki(Kamchatika) Urusi ina eneo dogo la bahari lenye barafu muda mwingi, uku ikipakana na Alaska ya Marekani. Magharibi kasikazini(Baltic Sea) baridi pia ni Kali,pia kazungukwa na maadui Sweden, Finland na kazalika, uku akiwa na Pwani ndogo ya Santa Petersburgh. Kusini Magharibi( Black Sea/Sochi), hapo kidogo kuna Joto lakini pwani ni ndogo sana, amebanwa na Ukraine, Georgia Na Turkey. Kwahiyo kijiografia ya bahari ,Urusi akiwa na Carriers, zitatekwa mapema kwenye vita, sababu Urusi hana Makoloni ya mbali kuzilinda meli zake katika Missions. Marekani(USA), ana fedha, ana bahari zenye joto kusini(Savvana Texas, New Orleans, Miami, Kalolinas, e.t.c), ana bahari kubwa ya Mashariki ya Atlantic ambapo hakuna nchi au bara lingine mbele yake, anaenjoy Carriers suplimacy, USA ana bahari Magharibi (Pacific), anaenjoy suplimacy sababu hakuna nchi nyinhine mbele yake. USA ana Alaska, visiwa vya American Samoa, Guam, Hawaii, Solomoni islands, Puerto Rico na vingine vingi mbali na ardhi yake kumuwezesha kupaki Carriers zake kabla na baada ya Missions. USA ana faida kwa kila jambo kuliko nchi yeyote duniani.
Reasonable mkuu
 
Taifa timamu haliwezi onesha mabavu yake yote,hili ndicho kinachotucost dunia ya tatu maana sherehe za Uhuru tunaonesha hadi vya uvunguni,N Korea imekuwa ngumu kudhibitiwa maana amecontrol utokaji wa taarifa za taifa nje ya mipaka,na hii ndio inampa pumzi kiduku
Sure mana.Na ndio maana binafsi naamin hiz report zinaweza kuwa zinatumika strategically ku mislead opponents
 
Taarifa nyeti kama hiz za mamabo ya kiusalama kwa taifa kubwa kama usa huwa naona zinatumika ili kuwa mislead hawa washindani wao.Huwa nahis hivyo binafsi.
Huwez ku publicise taarifa nyeti namna hiyo.
Ni kama ile memo ya Bwwana Pompeo ilisomeka kama bahat mbaya kwa wana habari kusema "5000 troops to columbia" (somethinf like dat kama sijakosea) wakat wa choko choko za venezuela zikiendelea.mkijichanganya tu china na russia kuzifanyia kazi andiken mmeumia
Umeisoma vizuri lakini hiyo taarifa?.
 
sio kweli, ili kulinda maslahi yako kama Taifa inabidi kuionyesha dunia una mabavu ya kutosha wasichezee maslahi yako!.
Angalia USA anavyoonyesha mabavu yake south china sea, Middle east na hata Africa.
Angalia Russia anavyoonyesha mabavu yake Crimea na Syria.
Angalia China anavyozidi kujitutumua South China Sea kumuondoa USA ili aweze kuwa superior pekee ukanda ule!.
Angalia Kagame anavyojiimarisha East Africa, nenda Middle east kwenye power struggle ya Iran na Israel. Rudi kwa Palestina na India.
Mabavu ni kila kitu kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani, ukijifanya msiri dunia itakuadhibu!.
Kila napokutana na suala la kagame kujimwambafy east africa halaf waasis wa jumuia yenyewe n
ss tupo tu like tumemshindwa huwa it hurts me to my soul.Roho huwa inaniuma sanaaaaa.
 
Vita kubwa ni Vita inayo weza kihusisha Powerful countries, mfano China, Russia na Usa, hawa sio tu Silaha za atamizi bali pia wana kila aina ya silaha za hatari kabisa ambazo kamwe hazowezi fanya vita kuwa rahisi.

Na ndo nikasema hizo Carrier sio kwa vita kati ya USA na RUSSIA.
Vita kati ya Marekani na Urusi au Marekani na Uchina ni vita kati ya nchi zenye nguvu kijeshi lakini haimaanishi na wala sio Guarantee kwamba ni vita kubwa.

Vita kubwa ni matokeo ya vita kutokana na aina ya vita inayopiganwa, silaha zinazotumika, idadi ya majeshi na mataifa inayojumuisha.

Ni rahisi sana kuzungumza kuizamisha Carrier kuliko kutenda na hilo limekwisha kufanyika kitaalamu na si 'kisiasa' ili kupata majibu ya uwezo wa hizi Carrier kimapambano.

Katika Conventional Warfare yoyote ile kati ya hizo 'nchi kubwa' itahusisha vitengo vya kijeshi zaidi ya kimoja. Hapa nazungumzia, kutakuwa na uhusika wa Air-Force n.k. kuweza kuiendesha hii vita.

Wakati wowote ambao Carrier inakuwepo katika majukumu yake, lazima kunakuwa na vitengo vingine vya kuiendesha Operesheni ya kijeshi ama vita.

Airforce inakuwa na jukumu la kuziwinda Missile Launch Facilities pamoja na Missile Batteries zilizopo katika Range ili kuzidhibiti kwa mtindo wa Electronic Warfare ama kuzishambulia kwa makombora pale inapobidi.

Navy inaiendesha Carrier Group inayohusisha pia Submarines za kisasa zitakazokuwa na kazi maalumu ya kukabiliana na hatari zote za majini hususani zile zitakazokuwa zikiiwinda Carrier.

Wakati adui anaiwinda ama anauwinda msafara wa Carrier Group atalazimika kuzipenya hizi Layers zote za kiulinzi na hili si jambo la kuleta ushabiki na maneno ya kisiasa. Ni jambo lenye madhara makubwa kwa jeshi lolote la adui litakalojaribu kufanya hivyo.

Ni kiasi gani cha Firepower atakacho Risk adui ili kutekeleza Mission kama hii ya kuizamisha tu Carrier huku pia akijaribu kuikabili Retaliation yake hata kama ni nchi yenye nguvu kijeshi kama China ama Urusi?

Uendeshaji na masuala ya kiulinzi ya Carrier Battle Groups ni suala la 'Uwezo' tu na hilo linafanyika kwa wenye uwezo huo. Mengine ni maneno tu ya kisiasa.
 
Duh! Hongereni wachambuzi wote hapo juu 👏👏👏 mmeupamba huu uzi vizuri Sana.
 
Back
Top Bottom