Kwanini RC wa Morogoro anang'ang'ania kupewa Barakoa za Devota Minja ili azigawe yeye?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,506
217,767
Subpost 5 - MH Devota Minja mbunge viti Maalum mkoa wa Morogoro Leo ametoa msaad ( 426 X 640 ).jpg

Taarifa kutoka Morogoro zinadokeza kwamba Mbunge wa Chadema Mh Devota Minja amekamatwa na jeshi la polisi kwa Amri haramu ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , kwa kosa la kufuata muongozo wa kuzuia Corona wa shirika la Afya la dunia ( WHO ) na kugawa Barakoa bora kabisa za viwango vya N 95 kwa Wakazi wa Morogoro ili kuwakinga na maambukizi ya virusi hivyo hatari .

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mh Mbunge ametakiwa kusalimisha Baracoa zake kwa RC huyo ili ofisi ya RC izigawe kwa wananchi , sasa sisi wafuatiliaji wabishi tumejiuliza kisa cha RC kung'angania barakoa za Mh Mbunge ili azigawe yeye , kwanini Ofisi ya Mkoa isitafute barakoa zake na kuzigawa badala ya kutaka kuchukulia kiki kwenye barakoa za mbunge wa Chadema ?

Bali kinachofahamika ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kabla ya kuteuliwa kuwa RC alikuwa Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha .
 
Devotha aache siasa kwenye jambo serious kama hili. Afya za watu ni issue sensitive sana.

Mkuu wa Mkoa akichukua asizigawe tu kiholela, akahakikishe zinakaguliwa tena kama hazifai zichomwe moto.

Abood hakuwa mjinga kukabidhi ambulance, ndoo za maji na sanitizers kwa mamlaka.

Mtaua watu kwa tamaa zenu za madaraka aisee!
 
Mmeishazoea kutiliana sumu kama mlivyomfanyia Mangula , sasa mnaona kila mtu ni muuaji !
 
Devotha aache siasa kwenye jambo serious kama hili. Afya za watu ni issue sensitive sana.

Mkuu wa Mkoa akichukua asizigawe tu kiholela, akahakikishe zinakaguliwa tena kama hazifai zichomwe moto.

Abood hakuwa mjinga kukabidhi ambulance, ndoo za maji na sanitizers kwa mamlaka.

Mtaua watu kwa tamaa zenu za madaraka aisee!
Acha ubwege wewe mbweha kilaza hizo barakoa za Abood zilipimwa wapi lini? Tamaa zipi za madaraka kwenye kulinda Afya za watu? Ataua watu gani? Acheni ujinga wa kishamba huo
 
Ujinga huu wa RC wa morogoro usiigwe na maRC wengine acheni RC wa morogoro abakie na ujinga wake wa kuonea wapinzani mwenyewe
 
Acha ubwege wewe mbweha kilaza hizo barakoa za Abood zilipimwa wapi lini? Tamaa zipi za madaraka kwenye kulinda Afya za watu? Ataua watu gani? Acheni ujinga wa kishamba huo
Nyie alama yenu ya utambulisho ni matusi. Usitarajie nitajitambulisha hivyo pia.

Devotha nia yake ni nzuri lakini njia aliyoitumia sio sahihi. Anawaza kujipatia umaarufu bila kujali afya za watu.

Mamlaka zipo. Leo kila mtu akiachwa abebe barakoa zake za mitaani huko kupelekea watu, tutakuza tatizo badala ya kupunguza.

Mamlaka zipo. Abood alishirikiana na mamlaka kama alivyofanya Rostam na wengine. Sio kwenda kwa bodaboda kinyeji enyeji tu.

Hamfundishani uongozi?
 
Back
Top Bottom