Kwanini Rais Samia unafanya maisha yetu Watanzania kuwa magumu hivi?

Habari wanaJF,

Watanzania tunajiuliza kwa nini Rais wetu wa sasa anaruhusu mambo haya.

Una ajenda gani? Je, wewe hutambui wananchi wako walivyo maskini na fukara sana?!

Ngoja niwaoneshe, Chini yako Mh. Rais Samia umeruhusu mambo haya:

1. Umeongeza gharama za kutuma na kupokea hela katika (tozo ya uzalendo) simu tu
Hivi mlishajiuliza, kwa nini "tozo" hizi hazikuwekwa kwenye kutuma na kutoa hela benki, labda na T/T kimataifa?
Kwa sababu benki na kwenye "kimataifa" wapo wenye uwezo (matajiri). Ni watu wa chini tu na wachache wa kipato cha kati, wanatumiana hela kwa simu Tz. Huu ndio ukweli. Leo, Rais umefanya kutuma hela kwa sisi maskini imekuwa ngumu sana. Yani kumtumia Mama elfu 10 kijijini unawaza, hadi uwe na elfu 3 ya ziada. Kweli?
Unakuwaje Rais unayefurahia hili?

Halafu una maneno matamu, vitendo huna! Kwani waTz ni watoto hadi uwape maneno tu!

2. Umeongeza bei za mbolea kwa wakulima
Najiuliza tena, tumekukosea nini sisi "hohehahe" wa Tanzania. Ukaona tozo hazitoshi, ukaja mpaka kwenye kilimo chetu.
Kwamba Samia unataka hata kula yetu iwe ya gharama kiasi hicho. Tutazalishaje chakula.?

Nisaidieni kumuuliza swali Rais wetu.(Hivi Rais wetu unayajua kweli maisha ya Watanzania wako?) wapo mtakaomtetea ktk hili la mbolea, kwamba labda bei ktk soko la dunia imepanda. Ni hoja mufilisi hii. Serikali miaka yote hutoa ruzuku kwa uingizaji wa mbolea nchini. Samia anashindwa nini kufanya hivyo, ili bei ibaki vile vile!
"Halafu akajisemea kwamba kuna kiwanda kinajengwa, kiwanda kitashusha bei, leo?

3. Umeongeza kodi kwenye nishati ya Mafuta
Ndio, wewe ndio umesaini bajeti mpya. Ina kodi nyongeza za uingizaji nishati za mafuta dizeli, petroli na taa.Kama ulivyosaini tozo za simu.Kwa hiyo na gharama za usafirishaji zimeongezeka chini yako. Hapo bado kuna zile nyongeza mpya za EWURA kila mwezi.
Kwa hiyo nikimtumia mama yangu hela kijijini, inakatwa mara mbili. Mama akienda kununua mbolea, anakuta bei mara mbili. Mazao yakiiva shambani, akiita Toyo ambebee, gharama ya usafiri imepanda mara mbili. Kwa hiyo kila hitaji hapo inabidi hela yake mama huko kijijini aiongeze mara mbili, kuna maisha hapo kwa masikini nchi hii tena?

4. Bei ya gesi majumbani nayo imeongezeka
Sasa hii nayo ni funga kazi, nendeni mkaulize bei mlizokuwa mnajaza gesi za majumbani.Hivi kweli, hela inakatwa mara mbili, tukienda shambani, mbolea haishikiki, kusafirisha chochote gharama ya dizeli juu, ukija kwa mama kijijini asitumie mkaa, au kuni, anakuta gesi bei juu, hivi kuna mzunguko wa maisha kwa maskini hapo? Hata kijana akitaka kujiajiri shambani, ataweza vipi?

Halafu kuna "mijitu" inasema "Mama anaupiga mwingi"

Ukitazama hivyo vitu vyote hapo juu gesi, mafuta dizeli, petroli, mbolea, n.k. wawekezaji wake ni matajiri, na wanufaika wake ni masikini hohehahe. Je, Mama ameamua kuchukua hela kwa maskini na kuwapa matajiri?

Maskini tunaumia sana.
Tatizo si SSH.Tatizo ni sisi wananchi.Kama miaka 60+ hata maji safi,madarasa,vidaraja na zahanati sehemu nyingi ni hadithi za kufikirika,unadhani ndani ya miezi 4 atafanya nini cha ajabu?
 
Mama anafungua nchi!

Mama anawakomesha mataga na sukuma gang

Mama anaupiga mwingi sana!

Maama ana rudisha hela mtaani ili sisi mibavicha tuwe tunaziokota.

Polepole na Bashiru wanakiona cha moto!
Huko waliko wamekaa wanajiuliza,tutawaambia nini wananchi,maana tulichekelea alipokufa mwendazake.sasa mama anawanyoosha sio kitoto,tukianza kumsema na tulimsifia tutaonekana hatuna msimamo.
 
50 Reactions
Reply
Back
Top Bottom