Kwanini Rais Samia unafanya maisha yetu Watanzania kuwa magumu hivi?

Ikiwa mpaka sasa hujaitwa Sukuma Gang na wala hujaambiwa unamchukia Samia au kuambiwa Rais Magufuli keshakufa na harudi tena, basi ni hakika tumeshapiga kona kurudi kwenye uhalisia wa siku zote!
Kuna watu walijitoa ufahamu, huko mwanzo, wakajiona wanamjua sana Samia, akawa anawapa vimaneno wanapenda.

Tena wengi walikuwa CHADEMA, hawakutaka kabisa tumkosoe. Ndio maana nasema hata CDM imeshuka viwango sana.

Uwezo wao wa kuona mbali umepungua sana. WANAHEMUKA TU.

Leo nao wanamkosoa.
 
Samia mnamlaumu bure, na yeye anashindwa kusema kweli tu,

Dikteta kafa ameacha hazina nyeupe kabisakabisa, hakuna senti mia
Si kweli. Hazina yetu haijawahi kujaa.

Halafu kwa nini Tz, marehemu wanabebeshwa lawama kila uchao.

Huwa nashangaa, hadi leo kuna watu wanamlaumu Nyerere, kwa yanaoendelea nchini. Hata la KATIBA mbovu, kina Tundu Lissu , n.k wanamlaumu Nyerere.

Shida nini? Nyani Ngabu , Kiranga
 
Nyerere ana lawama karibu zote kuhusu katiba yetu ya sasa.

Kwa sababu aliipitisha yeye, aliipitisha bila kushirikisha wananchi, kwa makusudi kabisa, na hivyo anachukua lawama.

Hadi leo watu wanawalaumu Stalin na Hitler.Ukiwa mwanasiasa, ukaharibu, lawama haziishi ukifa.

Kama hutaki lawama, usiwe mwanasiasa.
 
Taifa zima mnalaumu aliyelala kaburini, na hamfanyi kitu?!

Hapo ndio sielewi..
 
Kwanza si kweli kwamba taifa zima tunalaumu.

Pili, si kweli kwamba wanaolaumu hawafanyi kitu.

Tatu watu wanajifunza katika hizi lawama. Mpaka leo watu wanawalaumu kina Hitler na Stalin, Caesar na Alexander.

Hapo huelewi hata usichoelewa.
 
Habari wanaJF,

Watanzania tunajiuliza kwa nini Rais wetu wa sasa anaruhusu mambo haya.

Una ajenda gani? Je, wewe hutambui wananchi wako walivyo maskini na fukara sana?!

Ngoja niwaoneshe, Chini yako Mh. Rais Samia umeruhusu mambo haya:

1. Umeongeza gharama za kutuma na kupokea hela katika (tozo ya uzalendo) simu tu
Hivi mlishajiuliza, kwa nini "tozo" hizi hazikuwekwa kwenye kutuma na kutoa hela benki, labda na T/T kimataifa?
Kwa sababu benki na kwenye "kimataifa" wapo wenye uwezo (matajiri). Ni watu wa chini tu na wachache wa kipato cha kati, wanatumiana hela kwa simu Tz. Huu ndio ukweli. Leo, Rais umefanya kutuma hela kwa sisi maskini imekuwa ngumu sana. Yani kumtumia Mama elfu 10 kijijini unawaza, hadi uwe na elfu 3 ya ziada. Kweli?
Unakuwaje Rais unayefurahia hili?

Halafu una maneno matamu, vitendo huna! Kwani waTz ni watoto hadi uwape maneno tu!

2. Umeongeza bei za mbolea kwa wakulima
Najiuliza tena, tumekukosea nini sisi "hohehahe" wa Tanzania. Ukaona tozo hazitoshi, ukaja mpaka kwenye kilimo chetu.
Kwamba Samia unataka hata kula yetu iwe ya gharama kiasi hicho. Tutazalishaje chakula.?

Nisaidieni kumuuliza swali Rais wetu.(Hivi Rais wetu unayajua kweli maisha ya Watanzania wako?) wapo mtakaomtetea ktk hili la mbolea, kwamba labda bei ktk soko la dunia imepanda. Ni hoja mufilisi hii. Serikali miaka yote hutoa ruzuku kwa uingizaji wa mbolea nchini. Samia anashindwa nini kufanya hivyo, ili bei ibaki vile vile!
"Halafu akajisemea kwamba kuna kiwanda kinajengwa, kiwanda kitashusha bei, leo?

3. Umeongeza kodi kwenye nishati ya Mafuta
Ndio, wewe ndio umesaini bajeti mpya. Ina kodi nyongeza za uingizaji nishati za mafuta dizeli, petroli na taa.Kama ulivyosaini tozo za simu.Kwa hiyo na gharama za usafirishaji zimeongezeka chini yako. Hapo bado kuna zile nyongeza mpya za EWURA kila mwezi.
Kwa hiyo nikimtumia mama yangu hela kijijini, inakatwa mara mbili. Mama akienda kununua mbolea, anakuta bei mara mbili. Mazao yakiiva shambani, akiita Toyo ambebee, gharama ya usafiri imepanda mara mbili. Kwa hiyo kila hitaji hapo inabidi hela yake mama huko kijijini aiongeze mara mbili, kuna maisha hapo kwa masikini nchi hii tena?

4. Bei ya gesi majumbani nayo imeongezeka
Sasa hii nayo ni funga kazi, nendeni mkaulize bei mlizokuwa mnajaza gesi za majumbani.Hivi kweli, hela inakatwa mara mbili, tukienda shambani, mbolea haishikiki, kusafirisha chochote gharama ya dizeli juu, ukija kwa mama kijijini asitumie mkaa, au kuni, anakuta gesi bei juu, hivi kuna mzunguko wa maisha kwa maskini hapo? Hata kijana akitaka kujiajiri shambani, ataweza vipi?

Halafu kuna "mijitu" inasema "Mama anaupiga mwingi"

Ukitazama hivyo vitu vyote hapo juu gesi, mafuta dizeli, petroli, mbolea, n.k. wawekezaji wake ni matajiri, na wanufaika wake ni masikini hohehahe. Je, Mama ameamua kuchukua hela kwa maskini na kuwapa matajiri?

Maskini tunaumia sana.
Kuna wanaye mtafutia agenda ya kushindwa kirahisi kwenye chama 2025.
 
Nasema hivi:

Gharama zipo chini sana. Mama aongeze tena kidogo ili wote tupate akili ili ukifika muda wa kuimba " wataisoma namba" tubadilishe iwe " tutaisoma namba"
Aisee wewe una akili ya kuku. Nenda ikulu wskussifie
 
mbona unajiondoa akili km hujaelewa, keshatamka hizo TOZO zote anazijua zipo na zitakuwepo ila waziangalie ili zisiwaumize wananchi.
Kodi ilikuwa inakusanywa kwa walipa Kodi 500 tu katika Tanzania yenye watu milioni 60 na wenye uwezo wa kulipa ni zaidi ya milioni 20 umeshaambiwa na Waziri
Wamachinga wote na Wajasiriamali hawalipi chochote
sasa km una simu na unaweza kuijaza pesa utasaidia UCHUMI wa Nchi hii
Mwendazake alvamia a.c za Watanzania wanaolipa riba na huduma za benki unataka tena wakamuliwe peke yao
sasa ni Watanzania wote tuchangie Maendeleo
Hatupingani na tozo but imewekwa kwa kiasi kikubwa tena zimewekwa kwenye sekta nyeti,mfano mbolea kwa mtanzania wa kawaida hawez nunua mbolea hata 5 bei ipo juu mno,ambapo ukiangalia karibia asilimia 60 ya watanzania wanategemea kilimo unafkiri inakuwaje? tena mazao bei chini vifaa gharama.
 
Habari wanaJF,

Watanzania tunajiuliza kwa nini Rais wetu wa sasa anaruhusu mambo haya.

Una ajenda gani? Je, wewe hutambui wananchi wako walivyo maskini na fukara sana?!

Ngoja niwaoneshe, Chini yako Mh. Rais Samia umeruhusu mambo haya:

1. Umeongeza gharama za kutuma na kupokea hela katika (tozo ya uzalendo) simu tu
Hivi mlishajiuliza, kwa nini "tozo" hizi hazikuwekwa kwenye kutuma na kutoa hela benki, labda na T/T kimataifa?
Kwa sababu benki na kwenye "kimataifa" wapo wenye uwezo (matajiri). Ni watu wa chini tu na wachache wa kipato cha kati, wanatumiana hela kwa simu Tz. Huu ndio ukweli. Leo, Rais umefanya kutuma hela kwa sisi maskini imekuwa ngumu sana. Yani kumtumia Mama elfu 10 kijijini unawaza, hadi uwe na elfu 3 ya ziada. Kweli?
Unakuwaje Rais unayefurahia hili?

Halafu una maneno matamu, vitendo huna! Kwani waTz ni watoto hadi uwape maneno tu!

2. Umeongeza bei za mbolea kwa wakulima
Najiuliza tena, tumekukosea nini sisi "hohehahe" wa Tanzania. Ukaona tozo hazitoshi, ukaja mpaka kwenye kilimo chetu.
Kwamba Samia unataka hata kula yetu iwe ya gharama kiasi hicho. Tutazalishaje chakula.?

Nisaidieni kumuuliza swali Rais wetu.(Hivi Rais wetu unayajua kweli maisha ya Watanzania wako?) wapo mtakaomtetea ktk hili la mbolea, kwamba labda bei ktk soko la dunia imepanda. Ni hoja mufilisi hii. Serikali miaka yote hutoa ruzuku kwa uingizaji wa mbolea nchini. Samia anashindwa nini kufanya hivyo, ili bei ibaki vile vile!
"Halafu akajisemea kwamba kuna kiwanda kinajengwa, kiwanda kitashusha bei, leo?

3. Umeongeza kodi kwenye nishati ya Mafuta
Ndio, wewe ndio umesaini bajeti mpya. Ina kodi nyongeza za uingizaji nishati za mafuta dizeli, petroli na taa.Kama ulivyosaini tozo za simu.Kwa hiyo na gharama za usafirishaji zimeongezeka chini yako. Hapo bado kuna zile nyongeza mpya za EWURA kila mwezi.
Kwa hiyo nikimtumia mama yangu hela kijijini, inakatwa mara mbili. Mama akienda kununua mbolea, anakuta bei mara mbili. Mazao yakiiva shambani, akiita Toyo ambebee, gharama ya usafiri imepanda mara mbili. Kwa hiyo kila hitaji hapo inabidi hela yake mama huko kijijini aiongeze mara mbili, kuna maisha hapo kwa masikini nchi hii tena?

4. Bei ya gesi majumbani nayo imeongezeka
Sasa hii nayo ni funga kazi, nendeni mkaulize bei mlizokuwa mnajaza gesi za majumbani.Hivi kweli, hela inakatwa mara mbili, tukienda shambani, mbolea haishikiki, kusafirisha chochote gharama ya dizeli juu, ukija kwa mama kijijini asitumie mkaa, au kuni, anakuta gesi bei juu, hivi kuna mzunguko wa maisha kwa maskini hapo? Hata kijana akitaka kujiajiri shambani, ataweza vipi?

Halafu kuna "mijitu" inasema "Mama anaupiga mwingi"

Ukitazama hivyo vitu vyote hapo juu gesi, mafuta dizeli, petroli, mbolea, n.k. wawekezaji wake ni matajiri, na wanufaika wake ni masikini hohehahe. Je, Mama ameamua kuchukua hela kwa maskini na kuwapa matajiri?

Maskini tunaumia sana.
Mtu mwenyewe wa kuja atajua shida zenu nyie wanyarukoro ?
 
Naunga makato ya simu yaendelee, gesi ipande lakini manufaa ya yote hayo tutayaona baada ya serikali kuboresha miundo mbinu,nawasihi watanzania wenzangu tuwe wavumilivu na wazalendo, sidhani kama kulalamika kwetu kutayaleta mabeberu yaje yatulipie Kodi.

Lakini tukumbuke kuwa hakuna taifa linaweza simama bila Kodi, serikali ya rais inatakiwa kuwa imara katika kusimamia Mambo haya, iachane na kelele za mitandaoni,ukija huku uraiani watu wanaiunga mkono serikali isipokuwa watu wachache tu hasa mitandaoni
Uzalendo maana yake nini?
Nani aliesema kuna taifa linaweza kusimama bila ya kodi?
Kama unaifaham nchi hii, umeona hizo kodi zinazo lalamikiwa ndio kodi pekee zinazoweza kuinua pata la nchi kwa kiwango kua zisipokuwapo inchi hawezi kujimudu?
 
Back
Top Bottom