Nimshukuru kwa kile alicho kifanya pindi alikwua madarakani ila sasa kwa ninavyomuona nina pendekeza ange staafu siasa hata vikao vya vyama vya siasa asingekuwa anahudhuria, abaki tu kama mshauri wa maswala ya nchi tu basi bila kuweka msimamo au mapendekezo ya kukibeba chama chochote.
Kustaafu siasa na kuwa neutral ni bora zaidi kuliko kushiriki mara kwa mara na lawama zikawa nyingi. Haya ni mawazo binafsi na maoni tu.
- Amekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu nchi zingine kwenye maswala ya amani nay a kisiasa ambayo imegubikwa ka migogoro mingi sana ila nchini kwake kuna mengi ya kisiasa ambayo hayaja kaa sawa na hayakai sawa hadi mataifa kuanza kuikosoa nchi yake, hii yaweza kuwa sio uonevu au ni uonevu ila inatoa picha nyingine tofauti kabisa, kumbuka mataifa yameandika mengi na atakapokuwa anaonekana kwenda kusuluhisha anaweza akanyooshewa kidole kuwa kwake kumemshinda huku ndio atafanya nini, isitoshe huko Burundi nilisikia malalamiko ya wapinzani kuhusu msimamo wa uongozi wa jitihada hizo kuwa unaweza ukawa unaegemea upande flani, yote haya ni ya kuangaliwa yasibezwe,
- Malalmiko yanayo tolewa na wapinzani ndani ya nchi yake kuhusu mchakato wa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na hali ya kisiasa hajawa mstari wa mbele kuhakikisha linapata muarobaini, amekuwa sio mstari wa mbele kuonyesha jitihada ambazo zaweza kuepukana na malalamiko hayo, ila malalamiko kama hayo yakitokea nchi za nje akiitwa kusuluhisha anaweza akaenda kusuluhisha, hili bado sio sawa linamshushia heshima na hadhi kuwa anaona vibanzi nje ya macho ya wengine ila ndani ya nchi yake anakubaliana navyo, sio lazima ashirikishwe ndani ya nchi yake ila anaweza kushauriana na aliyeko madarakani au katoa kauli yake ili kusawazisha.
- Malalamiko ya Umoja wa ulaya hivi karibuni na marekani na mataifa mengine yeye angesimama na kutoa ushauri ambao utasawazisha na kuondoa sintofahamu pia atoe kauli hadharani kwa kile ambacho walikianzisha wa kutaka kukiona kinaendelea.
Kustaafu siasa na kuwa neutral ni bora zaidi kuliko kushiriki mara kwa mara na lawama zikawa nyingi. Haya ni mawazo binafsi na maoni tu.