Kwanini Rais Magufuli hataki kutumbua jipu la BRELA?

RAY DONOVAN

Senior Member
Jul 2, 2015
153
145
Rais Magufuli anasema anasema serikali yake imeweka mazingira mepesi kwa watu kufanya biashara zao kihalali na walipe kodi

Lakini watu wake aliowaweka BRELA ambayo iko chini ya wizara ya Biashara wao wanaendelea kum kumhujumu

kwa kufanya urasimu usio na kichwa wala miguu na kwenda kinyume na maagizo ya Rais

Nitatoa mifano ya namna Frank Kanyusi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa BRELA na bodi yao wanavyo mhujumu mheshimiwa Rais, serikali yake na Watanzania kwa ujumla:

1. Ukitaka kusajili kampuni jambo la kwanza utatataka kutazama kama jina la kampuni lipo au halipo mfano nataka kutumia jina la Jamiiforums....katika mazingira ya kawaida naweza kuingia kwenye mtandao wa jamiiforums na kufanya search kisha majibu yanakuja kama jina lipo au la. Lakini ukweli ni kuwa BRELA hiyo hawataki. Wanataka ufunge safari, ujaze form, kisha ulipie kiasi cha shilling elf 50 (including rushwa) kisha rudi nyumbani ukae wiki nzima kisha BAADA YA wiki nzima ufunge safari tena kufuata majibu.

Solution:
BRELA wanatakiwa kuweka kifute cha ku search business name online tena free kwa kila mtu ili kuachana na upotezaji wa muda na kukwamisha maendeleo na kufuata maagizo ya ya Mheshimiwa Rais.

2. Kwanini ichukue takriban mwezi mmoja (tena baada ya kutoa rushwa) kusajili kampuni na kupata docs zote? Kwa nini isichukue masaa walau 3? kama mtu kaweza jina , kitambulisho, na kalipia kwa nini process owe ndefu kiasi hicho?

Solution:
BRELA waweke waweke access ya ku register business online kama wanavyofanya Rwanda ambako kusajili kampuni online ni 1 hour maximum baada ya kuwasilisha vitambuisho vyote. Pia waweke access ya kufanya malice online au kupitia mobile money na mtu apish sajili ana weza kwenda ku print mwenyewe hiyo certificate of registration akitaka. Muhim ni Company number

3. Problem nyingine ni BRELA hawaruhusu watu kufanya submission ya returns online. Hii pia ni kuweka miaya ya rushwa.

Solution:
Waweke option ya mtu au agent (kama vile mhasibu) ku submit returns online ili kuongeza efficiency.

4. Hawataki kuweka records za kampuni online. Sielewi kwa nini hawataki kuweka majina, na anuani za kampuni zote zilizosajiliwa, zilizofutwa na majina ya directors na shareholders na kiasi gani wanazo hizo shares na returns na docs zote za kampuni kama articles/memorandum. Hii inapelekea kuwepo kwa hali ya sintofaham kujua who does what and who owns what.

Solution:
Records one zine online tena open kwa kila mtu kuona mfano infor kama vile:
1.Registered office address
2.Company status (kama iko active au imekufa)
3.Company type (kama ni Limited company au LLP au vinginevyo)
4.Date of incorporation
5.Pia waweke Accounts za hizo kampuni na lini accounts ziko due

Pia waweke filing history ya hiyo kampuni na vitu kama vile:
1. accounts
2. Capital
3. Confirmation statements annual returns
5. Charges
6. Officers wa hiyo kampuni (wallop na waliojiuzulu) na kama pia ni wakurugenzi wa makapuni mengine ndani ya Tanzania na majina ya hayo makampuni

Naamini kupata baadhi ya tarifa inaweza ikawa na charges kidogo (isizidi shilling elf 10)

Ukitaka kujua zaidi hebu soma hii taarifa ya world Bank inayozungumia ranking of doing business

http://www.doingbusiness.org/~/media/GIAWB/Doing Business/Documents/Fact-Sheets/DB16/FactSheet_DoingBusiness2016_SSA_Eng.pdf

zaidi soma hapa: Doing Business in Tanzania - World Bank Group


Hayo yote niliyosema hayana ugumu wowote ule ni software kuiambia ifanye nini na itafanya
 
Safi sana tunatakiwa kuwa na watu kama wewe ili twende mbele ....

Brela bado ni jipu hawako on time wanatengeneza mazingira ya kupewa hongo ....
 
Huko Ndiko Simba Trust Zilikosajiliwa Halafu Na Yake Makampuni Ya Ukwapuaji Millions Of Money
Ndiyo Maana Hawataki Kuwa Wawazi Kwenye Usajili
Wa Makampuni Online
Wanafanya Hongo Kama Ndiyo Mtaji
 
Kuna jamaa mmoja hapo anaitwa Nyarara huyo ndo kinara wa kupokea rushwa za usajili wa kampuni. Nina jamaa yangu ameshaliwa hadi Sh. 2M na hajasajiliwa kampuni yake.
 
Jipu kubwa linaloelekea kuleta kansa nchini ni dubwasha linaloitwa CDA kule Dodoma.
Mh tafadhali tusaidie tunateseka wananchi wako.
 
waweke ofisi kwenye kanda,wamekaa dar tu miaka nenda rudi,

Kila wilaya watu wawe na urahisi wa kusajili kampuni tena kirahisi kabisa na hata kwa kutumia simu ya mkononi afterall detals za zote zishaunganishwa na kitambulisho cha taiga.
 
Tatizo hii nchi kila kitu tumemuachia mkuu, kwani waziri anashindwa kufanya ka ubunifu kadogo kama haka, kwanini asikutafute ukampa maelezo mazuri namna ya kufanya hiyo?
 
online au kwenye database!
anyway kuweka rekodi kwenye mafaili ni issue ya kizamani
 
Huko Ndiko Simba Trust Zilikosajiliwa Halafu Na Yake Makampuni Ya Ukwapuaji Millions Of Money
Ndiyo Maana Hawataki Kuwa Wawazi Kwenye Usajili
Wa Makampuni Online
Wanafanya Hongo Kama Ndiyo Mtaji
the plot thickens....
 
Tatizo hii nchi kila kitu tumemuachia mkuu, kwani waziri anashindwa kufanya ka ubunifu kadogo kama haka, kwanini asikutafute ukampa maelezo mazuri namna ya kufanya hiyo?

HAWAWEZI KISHA WANAKUJA jf KULALAMIKA KUWA WANAFANYIWA MAJUNGU
 
Brela endeleeni kukaza, watu wanataka wafungue makampuni ya mifukoni watupige sisi maskini.
 
Back
Top Bottom