Kwanini Rais Magufuli hafanyi ziara Zanzibar?

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
8,987
14,714
Nimekuwa nafuatilia ziara za Mh.Magufuli mikoani lakini kwa muda mrefu sijamuona akifanya ziara visiwani Zanzibar . Najiuliza hii ni sawa? Au kuna mgongano wa Katiba ya Jamhuri ya muungano na ile ya Zanzibar katika masuala ya kiuongozi. Naomba wenye kufahamu hili watuambie.
 
Akienda huko kufanya hizo ziara atawaambia nini Wazanzibari? Ameamua kwa utashi wake kuwadhulumu watumishi wa umma wa Tanganyika haki zao za msingi ili ajenge Standard gauge? ajenge daraja la Salender? anunue bombardier? Watamuelewa?

Maana wao wanachohitaji zaidi ni nchi yao kutambulika kimataifa kama nchi kamili badala ya kuwa koloni la Tanganyika.
Nadhani Kanda ya ziwa ataeleweka zaidi hasa anapochanganya na ile lugha yake ya asili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom