Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,058
Katika sherehe za Mei Mosi leo baada ya kuwaambia wafanyakazi hatopandisha mshahara,
Rais Magufuli ili kuwapooza aliwaambia kuwa kikokotoo cha mafao alichoagiza kurudishwa mnamo Disemba 28 mwaka jana kuwa ni ghali mno na kinaisababishia hasara serikali ila alikirudisha cha zamani baada ya kilicholetwa kulalamikiwa sana hivyo wasiwe wanaangalia tu upande mmoja kuwa wanakandamizwa kimaslahi
Rais alisema kikokotoo hiki hakitumiki hata nchi jirani au hata nchi tajiri za Ulaya maana ni gharama sana
Tukirudi nyuma Disemba ile 28 Rais Magufuli alishangaa sana watendaji wake kuondoa kikokotoo cha zamani (hiki alichokilalamikia leo) na kusema kitendo hicho ni kuwaonea sana wafanyakazi na hadi kufikia kumtumbua yule dada wa SSRA na waziri Jenista Mhagama japo hakumtumbua ila aliponda sana uamuzi ule ambao alikuwa akiuunga mkono
Watu wengi walishangaa na kujiuliza ni wizara au SSRA ndio walifanya maamuzi ya kubadili kikokotoo peke yao kwa serikali hii ya JPM ambayo waziri kabla ya kufanya maamuzi yoyote hata madogo inabidi ujiulize zaidi ya mara 10 ili asije kuumbuka.
Iweje uamuzi mkubwa kama wa kikokotoo wafanye wenyewe?