Kwanini Rais Kikwete haitakii mema Tanzania?

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
ADA ya wanafalsafa, ni kusema ukweli ili taifa la Tanzania linufaike, liendelee kudumu.
Najua Rais Jakaya Kikwete ni rais wa Tanzania, jambo hili sina shaka nalo. Kwamba alichaguliwa na wananchi kwa ushindi wa kishindo, hili sina uhakika, wanajua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) waliotangaza matokeo ila kwamba ni rais aliyetoa ahadi nyingi zaidi huenda kuliko watangulizi wake wote; hili pia nina uhakika. Lakini kuna mengine ambayo sasa inabidi nijiulize. Tena yapo mengi.
Uongozi ni kipaji, na kipaji mwanadamu hujaliwa na Mungu. Hata hivyo tusichanganye utashi wa Mungu na utashi wa wanadamu hata kama wamehongwa (We should not confuse the will of God, and the will of the corrupted majority).
Utashi wa Mungu ni wa kweli na haubadiliki badiliki, wala hauna upendeleo. Huo ni wa haki. Hautegemei nguvu za kupigiwa makofi.
Rais Kikwete, hivi karibuni ametokea ziara nchini Uturuki, baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari kwa kuimarisha mahusiano ya kimataifa. Nampongeza sana ila tujue kuwa nyuma ya utunukiwajij huo kuna hadithi ya kuchekesha.
Inahitaji wanafalsafa kugundua na kuwajulisha Watanzania kuwa “maana yake ni kuwa Rais wetu amekuwa mzungukaji au anayetembea nchi za nje zaidi mpaka anapaswa kutunukiwa kwa kutembelea nchi za nje.”
Kwanini rais hatulii nchini, hilo wanajua wanaompangia ziara, zake na taratibu zake za kazi, japo kuna wakati ilionekana kuwa rais mwenyewe ndiye mkaidi kufuata ushauri wa wale aliowateua kumshauri.
Lakini ukweli ni kwamba rais wetu ameonekana mzungukaji mpaka akatunukiwa shahada. Tuna mengi ya kujiuliza hapa.
Tukianzia suala nililotaja hapo juu, kuwa rais ametunukiwa shahada ya mahusiano ya kimataifa, je, ndani ya taifa atatunukiwa shahada ya mahusiano gani?
Tukianzia suala nililotaja hapo juu, kuwa rais ametunukiwa shahada ya mahusiano ya kimataifa, je, ndani ya taifa atatunukiwa shahada ya mahusiano gani?
Rais Kikwete, aliporejea kutoka Uturuki na Jordan akaenda jijini Mwanza kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambapo aliisifu taasisi hiyo kwa kile alichodai kuwa imefanikiwa kuzuia na kupambana na rushwa.
Rais wetu aliamuaje kuwahadaa Watanzania wanaoona kuwa anasifia kitu kisichofaa?
TAKUKURU iliyoshindwa kumchukulia hatua Andrew Chenge na watuhumiwa wengine wa rushwa ya rada...pia watuhumiwa wote wakubwa walioshiriki kuhujumu uchumi kupitia wizi wa EPA hawajachukuliwa hatua. Tena ushahidi umeshaonekana, rais haoni vibaya kutoa sifa kwa taasisi hiyo?
Mbaya zaidi, wale waliowahi kutajwa kwenye orodha ya mafisadi na ushahidi kuthibitisha hivyo nao hawajachukuliwa hatua.
Mbaya zaidi TAKUKURU ndiyo walioisafisha Richmond ambayo baadaye ilikuja kuthibitika kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Hao ndio Kikwete sasa anawatuma kuwa wakamate hata harufu ya rushwa.
Kama hawakuona rushwa katika Richmond, rushwa iliyoonekana wazi kwa kila aliyefuatilia sakata hili kwa ukaribu, wataweza kuona rushwa katika uchaguzi? Kikwete anatuma watu hawa wafanye nini? Kwa ajili ya nini? Na kwa ajili ya nani?
Rushwa zimetajwa katika chama chake wazi wazi ameshindwa kuwachukulia hatua wahusika iweje leo awatume wengine wakachukue hatua, hata kama walishaonekana hawawezi kuchukua hatua?
Leo wafanyakazi wa TRL wanataka kulazimishwa kupewa likizo bila malipo kwa miezi sita, rais yupo na anajua kuwa kuna ufisadi katika mkataba huo, ameshindwa kuutolea tamko, anataka wafanyakazi wa TRL waendelee kuhangaika katika nchi yao, shahada yake ya mahusiano ya kimataifa kweli itanawagusa wafanyakazi wa TRL?
Kama kweli shahada ya mahusiano ya kimataifa ina msaada mkubwa kwake na kwa taifa kwanini isitumike kuondoa mgogoro unaotaka kuibuka kuleta mgomo wa wafanyakazi?
Shahada hiyo inawasaidiaje TUCTA wasigome kutesa Watanzania, kwa kuwa wanasema serikali yake imewasahau wafanyakazi?
Rais aliyeombwa na Bunge awawajibishe waliopokea rushwa yeye ameshindwa kufanya vile, atawaelekezaje kina Hosea wakafanye kazi ambayo yeye mwenye mamlaka makubwa zaidi ameshindwa kuonyesha njia? Rais Kikwete analaani vitu anavyovitenda yeye. Nashindwa kuelewa.
Rais Kikwete amedai kwamba tayari ana taarifa za baadhi ya wanasiasa waliokwishaanza kutumia rushwa ili kupata uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Hivyo ameitaka TAKUKURU kuanza kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wanasiasa wa aina hiyo kwa kutumia vizuri sheria mpya ya matumizi ya fedha za uchaguzi iliyopitishwa na Bunge katika kikao kilichopita, kwani inaruhusu rushwa kudhibitiwa kabla na wakati wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi.
Lakini Kikwete ni kauli ngapi ulizotoa, na kuahidi kuwa ungezifanyia kazi? Wewe kila taarifa unayo, lakini unazifanyia kazi wapi? Taarifa na orodha za wauza dawa za kulevya unayo, taarifa na orodha za wanaoendesha vitendo vya kijambazi unazo, taarifa za watendaji wabovu ndani ya serikali yako unazo, taarifa za wanasiasa wanaotumia rushwa kupata uongozi unazo.
Je, kuwa na taarifa hizi kunatusaidia nini Watanzania? Kama hujazifanyia kazi na kutusimulia kuwa unazo, ni kama kumwonyesha mbwa kiko wakati hajui hata matumizi yake. Haisaidii.
Kauli ya kudhibiti rushwa nayo ni kauli nzuri, lakini Rais Kikwete atuambie Watanzania, yeye kwanini alihonga kanga, kofia na fulana kwa Watanzania wakati wa uchaguzi uliopita?
Ina maana anaona kuwa rushwa ni mbaya kwa sababu inaweza kumtoa madarakani, au rushwa ni mbaya kwa sababu ilimwingiza madarakani?
Sijui au sina uhakika na lengo la kiongozi wetu kumtuma Hosea afuatilie wenzake wakati naye ni miongoni mwao. Hii ni kama vile Rais Kikwete anafukuzia nyani katika shamba la jirani yake.
Ingefaa aache tabia ya jicho ya kuangalia wenzake na yeye kutojiangalia. Aangalie wajibu wake awawajibishe watuhumiwa wake, ndipo atume walio safi kuwawajibisha wengine.
Si tabia njema sana kutunga sheria zinazowafunga wenzako na kukuacha huru wewe. Ni dalili ya udikteta. Hata hivyo mabadiliko mazuri yaanze na nafsi ya ‘mimi’ kwanza ndipo tufikie na ‘wewe’ na ‘yeye’.
Kikwete umenena vema rushwa iko kila mahali, sote tuhusike na kuhusishwa katika mapambano hayo, vema sana anza wewe kwa kuonyesha mfano. Vinginevyo utathibitisha hukudhamiria kutenda kile ulichosema.
Kwanini Rais Kikwete analaani vitu anavyovitenda yeye, hivi sasa kila kona ya nchi yetu kunabandikwa mabango, au wananchi wanapoitwa katika mikutano ya hadhara wanapewa mabango hayo yanayosomeka: “Tumefanya vizuri kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tuikamilishe kwa kuhakikisha wapo walimu wa kutosha, maabara, vifaa vya kusomea, vifaa vya kufundishia na nyumba za Walimu.”
Tujiulize, hivi kama rais wetu anatutakia mema, aseme ukweli, shule ngapi za kata zina vyumba vya madarasa?
Shule ngapi zina viti (madawati) ya kukalia? Mbona watoto wa Kitanzania bado wanakalia ndoo madarasani? Shule ngapi zina vifaa vya kusomea, shule ngapi zina walimu?
Mbona serikali inaokoteza shule ya msingi kuhamishia sekondari bila kujua huku shule ya msingi itabakisha pengo la walimu?
Kama hiyo haitoshi, sehemu ya mabango hayo yanayoashiria kuanza kwa kampeni, au shughuli za kumkampenia Kikwete kabla ya muda inasomeka hivi:
“Kwa nguvu ile ile, na kwa moyo ule ule, sasa tuelekeze jitihada hizo katika ujenzi wa zahanati vijijini, vituo vya afya kwenye kila kata na nyumba za watumishi wa kutoa huduma hizo.”
Ina maana hapa Kikwete anataka tena changisha changisha iliyopora mali za Watanzania kwa michango haramu ya sekondari iendelee?
Kuna nyumba zimebaki hazina baba kwa sababu ya michango ya sekondari, sasa Kikwete anataka kuongeza na zahati, tutachangishwa mpaka lini? Watanzania watajiletea lini maendeleo yao kama kila siku wanachangishwa tu?
Walimu wameokotezwa shule ya msingi, je, manesi, waganga na madaktari wataokotezwa wapi kuchezea afya za Watanzania, tufe kwa kiwango kile kile wanavyofeli watoto wa Kitanzania kwa tabia ya serikali kuokoteza walimu?
Na kwanini Rais Kikwete utoe mabango yapelekwe vijijini muda huu wakati mnasisitiza watu waache kujipitisha majimboni? Kufanya kampeni kwa mabango inaruhusiwa?
Hata kama inaruhusiwa mbona ujumbe katika mabango hayo unawahadaa Watanzania kusadiki kitu ambacho hakipo? Safari ni ndefu, kuwajulisha Watanzania watambue uhalisia wa mazingira yao. Lakini tunahitaji kuwa wakweli zaidi, maana ni heri ukweli unaouma kuliko uongo unaofurahisha.
SOURCE: http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=13951
 
pumba tupu.


Kweli lakini yapo pia mzuri aliyofanya kama kujenga shule za kata ambazo ziko chini ya kiwango na hamna walimu wala sustainable dvelopment plan ya hizo shule, lakini majengo yapo.

Kajitahidi kukamata senior officers watatu yona, mramba na mgonja hata kama ni danganya toto lakini kafanya.

Alimficha lowassa report ya richmond asiipate baada ya kuona inamwi-implicate na lowasa na wengine wawili wakaporomoka hata kama amekataa kutekeleza maagizo ya mengine ya bunge mfano kumnyima lowassa ulaji wa waziri mkuu mstaafu
 
Kajitahidi kukamata senior officers watatu yona, mramba na mgonja hata kama ni danganya toto lakini kafanya.

Alimficha lowassa report ya richmond asiipate baada ya kuona inamwi-implicate na lowasa na wengine wawili wakaporomoka hata kama amekataa kutekeleza maagizo ya mengine ya bunge mfano kumnyima lowassa ulaji wa waziri mkuu mstaafu

JK anatumia style ya kuuma na kupiliza
 
Kweli lakini yapo pia mzuri aliyofanya kama kujenga shule za kata ambazo ziko chini ya kiwango na hamna walimu wala sustainable dvelopment plan ya hizo shule, lakini majengo yapo.

Kajitahidi kukamata senior officers watatu yona, mramba na mgonja hata kama ni danganya toto lakini kafanya.

Alimficha lowassa report ya richmond asiipate baada ya kuona inamwi-implicate na lowasa na wengine wawili wakaporomoka hata kama amekataa kutekeleza maagizo ya mengine ya bunge mfano kumnyima lowassa ulaji wa waziri mkuu mstaafu

How true is the contention that Jakaya did not agree with the parliament in denying Lowassa pension benefits of retired Prime Ministers? Can someone knowledgeable enlighten us on this issue.
 
Jamaa anapoint nyingi ambazo amezitoa na nashangaa bado kuna watanzania wapuuzi wanashindwa kujua kitu kinachoitwa ukweli.Huu ni ukweli na mtu au watu wowote wanaotaka kumjibu watumia point ambazo mwandishi amezieleza mfano watu ambao wametajwa kwenye rushwa ya rada, Je ni hatua gani zimechukuliwa? Kuna ushahidi wa kutosha kwani waliingiziwa ela kwenye account zao.Wameliingiza taifa kwenye madeni ambayo hayakustahili thamani ya rada ni £12 million wao wamenunu kwa £40 million kwahiyo £28 Million wameweka kibindoni.
Sasa swali kwa watanzania wenzangu ni nini kikwete amefanya kuhusu hilo? au nyinyi wenzetu vipofu na viziwi.
Lets be honest here na tuache porojo.

Popo
 
Inasikitisha kuona baadhi yetu kutokuona ukweli kuhusu mambo yanavyokwenda Tz. viongozi hawajui wajibu wao.

mwaka huu tuwawajibishe viongozi jamii ya JK, hatuwezi kuwavumilia tena.
 
Back
Top Bottom