Kwanini Prince Bagenda na Buberwa Kaiza wanaonesha kumchukia Rais Magufuli japo walikuwa wapiga debe wake mwaka 2015

Ukisubilia huruma ya wanasiasa utakufa kwa stress, ni watu ambao hawaminiki kwa maneno yao iwe Jiwe, lissu au membe
 
Mkuu chinembe ni kwamba watu walikuwa hawajamuelewa Jiwe kama ambavyo hata wewe mwenyewe hujamuelewa.

Wote waliokwisha kumuelewa wamejitenga nae na wengine wameamua kukaa kimya. Wako watu kwa maelfu walioumizwa sana katika utawala huu wa awamu ya tano. Hivyo hao uliowataja kutoshirikiana nae yawezekana ni miongoni mwa wale walioumizwa. Yawezekana pia ndugu au jamaa zao ni miongoni mwa waathirika ktk awamu hii iliyojaa visasi na vitisho.
 
Hahaaa
Ukisubilia huruma ya wanasiasa utakufa kwa stress, ni watu ambao hawaminiki kwa maneno yao iwe Jiwe, lissu au membe
,hakika kabisa,watu wamesubiri milioni 50 kila kijiji....wameachwa kwenye mataa
 
Hivi kumchukia mtu, kupingana nae au kutokukubaliana na anayofanya ni vitu sawa..... Yaani usipokubaliana na mtu basi unamchukia ?
 
Hawa watu walikuwa wapiga debe wakubwa wa JPM 2015, waliandika makala za kumsifu na kumjenga kisiasa.

Lakini naona siku za karibuni wameanza kuonyesha upinzani mkubwa sana kwa Rais wetu mpendwa.

Buberwa Kaiza katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, anafanya ukosoaji mkubwa japo anajaribu kujifichaficha

Prince Bagenda yeye alifikia kutunga kitabu,japo kabla hajakiachia, vyombo vyetu pendwa vya usalama vikampa angalizo

Je watu hawa wana uroho wa madaraka walidhani kwa kuandika vipeperushi tu wangepata uteuzi? Watanzania tumekuwaje? Kila kitu ukifanya mpaka upate kitu?

Viva JPM
#matege
walidhani wana nadi dhahabu wakagungua kumbe ni foolgold
 
Watu walikuwa hawajamuelewa hapo mwanzoni ,walikuwa wanadanganywa kwamba ni mchapa kazi kwasababu amekariri idadi ya samaki,ng'ombe,mbuzi ,kuku na kilometer za barabara .

Katika kipindi chake cha uwaziri alipiga dili nyingi sana za kukupunguza upana wa barabara na kupiga cha juu ,kanunua meli bovu kwa 8B .

Ni mtu wa visasi sana ,alitaka kubomoa jengo la lowassa la tanesco kwa kisirani tu kumkomoa lowassa na alipoingia akaanza nalo amelibomoa lakini barabara yake na daraja wala haijafika hata kama jengo lisingebomolewa,alimfunga Lema wa Northern Engineering kisa tu alitoa mpunga kwenye kampeni ya Ukawa.

Hawakujua Hawakujua.........
true hapo ndipo alipowagilibia watz,wengine tulitahadharisha mapema,hio sio dhahabu bali ni foolish gold but rangi halisi mmeona kila mtu,
rudieni kosa again ili avurunde zaidi,mtalimia kucha this time,
 
Mleta mada uliona zile video za mama kabendera akiomwomba magufuli amwachie mwanae alafu jamaa hakumwachia????

Mie nilivyoona zile video hadi niliumia kwa kweli. Mbaya zaidi mama yake alifariki jamaa na vyombo vyake hata hawakumruhusu Erick Kabendera kwenda kumzika mama yake mzazi.

Hivi ndugu yangu kwa unyama ule wa Magufuli na vyombo vyake nani atamuunga mkono Magufuli????

Amini nakwambia kwa roho mbaya na ukatili wa Magufuli unahitaji kuwa Shetani ili umuunge mkono.
Tunaomuogopa Mungu tumeshajitenga nae na sasa ni rasmi tunaenda kumtoa ikulu hapo October 2020!
 
Kwa levo yako hutakiwi kabisa kuongea hear say kama hiyo ya jengo la Lowasa la TANESCO..
Uzushi mtupu
Sawa liwe la lowasa, au sio kulikuwa na umuhimu gani wa kulivunja wakati hata ujenzi haukufika huko? Hata ofisi za idara ya maji nako vile?!!
 
Ni mtu wa visasi sana ,alitaka kubomoa jengo la lowassa la tanesco kwa kisirani tu
Sikuwahi kufikiria Kama una uwezo mdogo sana wa kufikiria Mambo kiasi Cha kuleta habari za kwenye kahawa
Like eneo lote pale Ni viwanja vya Tanesco na serikali kuanzia huku kwa Gwajima mpaka kuzunguka Mandela mpaka darajani,Lowassa alipataje kiwanja katikati ya eneo la miundo mbinu ya serikali?
 
Back
Top Bottom