Kwanini polisi wastaafu huwa hawapewi nafasi Serikalini?

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
28,903
10,534
Ni jambo la kawaida kwa askari jeshi kupewa kazi zingine kama u-DC,RC,balozi na nafasi nyinginezo mara wanapostaafu.Ni kwa nini askari polisi huwa hawapewi nafasi hizi?Huwa najiuliza sana.
 
Ni kweli kwakiasi fulani,ila Adadi alikuwa polisi kwasasa ni Balozi Zimbabwe,unajua tatizo la hawa ngunguri wakitoka jeshini huku uraia hawa kubaliki sana,kwasababu wana madhambi mengi sana,kama vile kuwa bambikia watu kesi za uongo...
 
wakiwa makazini wanajishugulisha sana na majambazi wakubwa wakubwa serikali imeshindwa kuwaamini hata mmoja ndio maana mpaka leo wizi wowote ukisikia umepigwa akuna aliekamatwa katafute uhalisia wahusika wakuu wake wako pale karibu na ralway usiniulize ipi
 
mtoa mada nadhani majibu ya Pdidy yatakuwa muafaka kukupa picha, pia waliowengi hawajasoma
 
Polisi wengi watanzania Shule hamna ni darasa la saba, sasa wewe unadhani wakistaafu watapewa wizara gani kule polisi kazi ni kupeana amri tu, unaweza kukuta polisi 50 wasomi wa chuo kikuu 3 hawa wengine wote ni na nani kauwa! Labda vijana wa sasa hivi wanaotoka vyuoni nakujiunga na jeshi la polisi ndio wanaweza kupata kazi serikalini pindi watakapostaafu
 
Ni jambo la kawaida kwa askari jeshi kupewa kazi zingine kama u-DC,RC,balozi na nafasi nyinginezo mara wanapostaafu.Ni kwa nini askari polisi huwa hawapewi nafasi hizi?Huwa najiuliza sana.
Kinachowaaponza ni rekodi zao kama ilivyosemwa hapo juu...

lakini ziada ya yote ni kwamba, MUDA WAO WA KUTUMIKA AMA KUTUMIKIA SERKALI HUWA UMEISHA! EXPIRED......
Wasichokifahamu wao ni kuwa wao si matumizi mzungunguko (recycled) wa serikali bali ni matumizi ya mara moja tu (single use)...na hawajifunzi!!!
maana ukianzia kwa yule wa enzi za kina mzee wa kiraracha mpaka huyu wa enzi za mzee wa safari bado ni walewale
 
Ni jambo la kawaida kwa askari jeshi kupewa kazi zingine kama u-DC,RC,balozi na nafasi nyinginezo mara wanapostaafu.Ni kwa nini askari polisi huwa hawapewi nafasi hizi?Huwa najiuliza sana.
Sasa mtu bogus kama Mahita utampa cheo cha udc unawatakia wema wakazi wa wilaya husika? yule hakuna anachojuwa zaidi ya maguvu na kukunja sura.
 
Police wa Tanzania ni wapumbavu wanaotumikishwa na CCM naweza kuwafananisha na Diaper ikishatumika basi haina matumizi mengine ni kuitupa tu au kuipiga kiberiti.
 
Nasikitika kuwa wengi mliochangia hamfahamu vema historia ya u-dc kwa wanajeshi au polisi. wengi mna jazba juu ya Polisi kutokana na majukumu yake. Kwa ukweli ni kuwa Askari Polisi wengi wamesoma kuliko wa Jeshi la wananchi (usiniulize takwimu) kwani nature ya kazi tu inaonyesha hivyo. wahitimu wa chuo kikuu walianza kuingia Jeshi la Polisi miaka ya Sabini mwanzoni. Tukija katika hoja ya U DC Je Mnamfahamu Tatu Ntimizi? Je akuwahi kuwa DC? No research no right to speak
 
Sasa mtu bogus kama Mahita utampa cheo cha udc unawatakia wema wakazi wa wilaya husika? yule hakuna anachojuwa zaidi ya maguvu na kukunja sura.
khaaah!umenikumbusha enzi za ngangari na ngunguri..
 
Polisi hawana tabia ya kumpindua rais madarakani ndo maana wanaachwa wakistaafu ila kwa wajeda hiyo ni mbinu ya serikali kuonyesha inawajali wasiwaze sana kuleta mabalaa.
 
Nasikitika kuwa wengi mliochangia hamfahamu vema historia ya u-dc kwa wanajeshi au polisi. wengi mna jazba juu ya Polisi kutokana na majukumu yake. Kwa ukweli ni kuwa Askari Polisi wengi wamesoma kuliko wa Jeshi la wananchi (usiniulize takwimu) kwani nature ya kazi tu inaonyesha hivyo. wahitimu wa chuo kikuu walianza kuingia Jeshi la Polisi miaka ya Sabini mwanzoni. Tukija katika hoja ya U DC Je Mnamfahamu Tatu Ntimizi? Je akuwahi kuwa DC? No research no right to speak
Sasa wewe hapa umechangia nini? unatuuliza sisi swali kuhusu Tatu Ntimizi wakati alieanzisha hii thread ameauliza swali anataka kujibiwa sasa badala ya kumjibu na wewe unakuja na swali! Hizi elimu za kata ni janga kwa Taifa.
 
wakiwa makazini wanajishugulisha sana na majambazi wakubwa wakubwa serikali imeshindwa kuwaamini hata mmoja ndio maana mpaka leo wizi wowote ukisikia umepigwa akuna aliekamatwa katafute uhalisia wahusika wakuu wake wako pale karibu na ralway usiniulize ipi

Mkuu una hoja hapa,pale karibu na railway kuna matatizo mengi sana.
 
Sasa wewe hapa umechangia nini? unatuuliza sisi swali kuhusu Tatu Ntimizi wakati alieanzisha hii thread ameauliza swali anataka kujibiwa sasa badala ya kumjibu na wewe unakuja na swali! Hizi elimu za kata ni janga kwa Taifa.

Sawa mimi nina elimu ya kata wewe una elimu ya "mtaa". Mimi najua kuwa Tatu Ntimizi aliwahi kuwa DC,wilaya aliyofanya kazi ni Mpwapwa mkoani Dodoma,kwa hiyo nilichokuwa namaanisha ni kwa wewe ambaye hujui kwenda sasa kwenye net na kufanya utafiti si kuropoka ropoka tu kwa kuwa mdomo unao.
 
Asichojua ni kwamba Tatu Ntimizi alikuwa askari polisi kabla ya kuwa DC na baadae naibu waziri.
 
Usichojuwa wewe ni kwamba haujui nini maana ya topic, kama ungejuwa maana ya topic ungekuja na orodha ya maaskari polisi waliopewa U dc na U RC baada ya kustaafu. orodha ya JWTZ ni kubwa hakuna hata haja ya kuwataja hii ndio maana ya topic hii.
 
Poa mkuu nadhani nimedandia daladala kwa mbele! Big up.
 
Usichojuwa wewe ni kwamba haujui nini maana ya topic, kama ungejuwa maana ya topic ungekuja na orodha ya maaskari polisi waliopewa U dc na U RC baada ya kustaafu. orodha ya JWTZ ni kubwa hakuna hata haja ya kuwataja hii ndio maana ya topic hii.
Uko sahihi kabisa mkuu Matola,polisi hakika ni wa kuhesabu.JWTZ sijui wana mvuto gani kwa watawala mi sielewi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom