Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
POLICE TRAFFIC WABORESHE CUSTOMER CARING KWA NAMNA HII.
Shikamooni wakubwa zangu wote.
Kitu ambacho police traffic wanapaswa kukumbushwa ni kuwa si wote wanaoendesha magari hapa Tanzania ni wamiliki wa magari hayo.
Wengine wameazima kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zao. Wanatenda makosa ya barabarani lakini hawatoi taarifa kwa wamiliki halisi. Naomba police watusaidie kwa hili kama sehemu ya kuboresha huduma zao kwa jamii (hususan wamiliki wa vyombo vya usafiri)
Kama mtu akitoa pesa kutoka kwenye ATM ya bank anapata SMS notification wakati huo huo, kwanini Police Traffic wakitoza fine kwa ile machine yao (Mobile Ticket Printer) SMS notification isiende kwenye simu ya mmiliki wa chombo cha usafiri automatically muda ule ule??
Juzi jumapili nilienda kumtembelea classmate wangu Beautiful Nkosazana maeneo ya gongo la mboto dar es salaam. Wakati ananisindikiza mida ya saa kumi jioni tukiwa ndari ya gari yake ndogo maeneo ya airwing tulikutana na tuta dogo la plastic/rubber ambapo baada ya kulivuka mbele tukasimamishwa na police traffic wakiwa na turubai ndogo pembeni pamoja na camera system ambayo baada ya udadisi baada ya tukio nikagundua kumbe ile camera ilikuwa kwa ajili ya ku detect gari zilizotozwa fine kwa makosa ya barabarani lakini wamiliki hawakulipia fine hizo.
Baada ya mazungumzo na mvutano kama wa dakika 15 na yule askari, classmate akaja kugundua kuwa ile gari ilikuwa inadaiwa kiasi cha shillings 60,000 kwa makosa mawili ya barabarani yaliyofanywa na mdogo wake ambaye aliazima tu gari ya dada mwezi uliopita.
Sasa hapa nikawaza, endapo wakati traffic anatoa ile receipt ya kutoza fine kwa yule dogo, sms notification ingeweza kwenda kwa mmiliki wa gari automatically kusingekuwa na mvutano baina ya police na classmate wangu, pia itakuwa ni njia nzuri ya kuboresha uhusiano mwema baina ya police na wamiliki wa vyombo vya usafiri.
Kwa wataalamu wa ICT hii inawezekana??
Sipo sahihi muda wote. Haya ni mawazo yangu binafsi and I STAND TO BE CORRECTED.
OUR MOTTO
=======
KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USITUMIKE VIBAYA KUICHAFUA NCHI YAKO.
Espionage: Majasusi wa Mossad alivyoiba mkojo wa rais Hafez kwa kutumia CHOO CHA BANDIA - JamiiForums
Secretariat ya ajira, kwanini interview za kazi zisifanyike kwa kanda (Zones)? Kwanini wote tujazane Dar? - JamiiForums