Kwanini Pesa za serikali zilizoongezwa kwenye bajeti ya kununua Mahindi zinaitwa pesa za Rais?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,307
217,306
Amesikika Mh Waziri Mkuu bungeni akimpongeza Rais Samia kwa kuongeza pesa ya kununua Mahindi ya Wakulima zilizofikia Bilioni hamsini.

Kwa kadri ya ufahamu wangu Mh Rais hakuitoa hela hii kutoka kwenye Mshahara wake bali ametoa hela hii kutoka kwenye Mfuko wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , sasa PM na viongozi wengine wameshindwaje kusema Serikali ndio imetoa hii bilioni 50, na badala yake anatajwa Rais binafsi , as if hela hii ametoa kwenye pochi yake ya kwapani , huu utamaduni wa upotoshaji tumeiga kutoka wapi, tumeamua kudanganya kwa faida ya nani, hivi tukisema ukweli kwamba serikali ndio imetoa pesa huku kiongozi wa Serikali hiyo akiwa yeye Mh Rais tutapungukiwa nini?
 
Kusifu na kuabudu kumeanza tena kama ilivyokuwa katika awamu iliyopita. Kila kitu sasa ni sifa kwa Mamaa, Mamaa.....!?
Hii kitu hata hayati Mkapa aliwahi kwa uwazi kabisa kuonyesha kutoridhishwa nayo, na hata kuwaonya mawaziri wa JPM.

Urais ni taasisi, si jambo jema hata kidogo kufanya "attribution" ionekane ni ya kiongozi wa juu binafsi pale serikali inapopaswa kutimiza wajibu wake wa kikatiba. Naye Rais anapaswa kuikemea tabia kwa kumaanisha pale anapokuwa ndani ya Baraza la Mawaziri
 
Hii inakuonesha jinsi mawaziri wenyewe wanaona wako pale kwa hisani tu wa Mama hawajiamini. Angesema Rasi ameidhinisha serikali kutoa kiasi cha pesa kwa ajili ya mahindi sio Mama Samia ametoa hili jambo lilianza awamu ya tano na linatakiwa likemewe kisheria ndio Rais atajwe kama kiongozi wa serikali ila kuna tofauti ya kutoa na kuidhinisha. Ndio nchi yetu imefikia hapa chawa wako mitaani na chawa wako mpaka serikalini imekuwa kama ndio sifa siku hizi kuwa chawa.
 
Amesikika Mh Waziri Mkuu bungeni akimpongeza Rais Samia kwa kuongeza pesa ya kununua Mahindi ya Wakulima zilizofikia Bilioni hamsini.

Kwa kadri ya ufahamu wangu Mh Rais hakuitoa hela hii kutoka kwenye Mshahara wake , bali ametoa hela hii kutoka kwenye Mfuko wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , sasa PM na viongozi wengine wameshindwaje kusema serikali ndio imetoa hii bilioni 50 , na badala yake anatajwa Rais binafsi , as if hela hii ametoa kwenye pochi yake ya kwapani , huu utamaduni wa upotoshaji tumeiga kutoka wapi , tumeamua kudanganya kwa faida ya nani , hivi tukisema ukweli kwamba serikali ndio imetoa pesa , huku kiongozi wa Serikali hiyo akiwa yeye Mh Rais tutapungukiwa nini ?
Bado kidogo watampa utukufu au malkia. Viva Royal highness

Sent from my A71 using JamiiForums mobile app
 
Ila na sisi wakosowaji tujifunze linapokosewa jambo katika Wizara fulani tuilaumu Serikali badala ya kumlaumu Mama Samia hapo ndio tutakuwa tumetenda haki kwa wote
 
Amesikika Mh Waziri Mkuu bungeni akimpongeza Rais Samia kwa kuongeza pesa ya kununua Mahindi ya Wakulima zilizofikia Bilioni hamsini.

Kwa kadri ya ufahamu wangu Mh Rais hakuitoa hela hii kutoka kwenye Mshahara wake , bali ametoa hela hii kutoka kwenye Mfuko wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , sasa PM na viongozi wengine wameshindwaje kusema serikali ndio imetoa hii bilioni 50 , na badala yake anatajwa Rais binafsi , as if hela hii ametoa kwenye pochi yake ya kwapani , huu utamaduni wa upotoshaji tumeiga kutoka wapi , tumeamua kudanganya kwa faida ya nani , hivi tukisema ukweli kwamba serikali ndio imetoa pesa , huku kiongozi wa Serikali hiyo akiwa yeye Mh Rais tutapungukiwa nini ?
kaongeza Rais au kaongeza yeye mwenyewe??! ( Just thinking out loud)
 
Rais akikosea analaumiwa yeye.

Akifanya vizuri hatakiwi kusifiwa yeye.

Aisee, haya ndio matatizo ya watu walioshiba halafu wana bando lisilo na kazi.
 
Back
Top Bottom