Kwanini pesa ya mahari hawataki tulipe yote taslimu?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Habari wadau!

Mdogo wangu alitangaza kutaka kuoa, kwa kuwa ni jambo la heri tukapeleka barua na taratibu za mahali zikafua!

Tumechumbia mtoto Wa kirangi mzuri sana!

Mahali wametutajia ng'ombe saba, tukakubali wala hatukulia lia kupunguziwe.

Wakatupa thamani moja ya ng'ombe kwa laki nne.

Kwa kuwa tulienda Dodoma, ili kuepuka usumbufu tulibeba kwa tahadhali million 5.

Ikawa baada ya kutamkiwa mahali yetu tukaingia kwenye hazina yetu tukatoa milioni mbili na laki nane cash! (2,800,000/=) na kuwalipa!

Nashangaa wakakataa katakata kupokea ikawa marumbano makubwa!

Na kikubwa walicholalamikia wale wakwe eti ni kwanini hatujaomba kupunguziwa mahali?

Kingine ni vile utaratibu wa kulipa, kwanini tunalipa yooote?

Walihoji kuwa kwani hatujui kwamba mahali huwa hailipwi yoote?

Walisisitiza kwamba makabila yote Tanzania huwa ni marufuku kutoa mahali yote sasa sisi kwanini tunalipa yoote?

Baada ya msuguano kwa hasira nikachukua Pesa ya mahali waoaji tukakubaliana kwamba tuahirishe tutakuja siku nyingine!

Swali, Kuna kosa gani mahali kulipwa yote?
 
Kwani mngetoa kiasi na si yote mngepungukiwa nini?

Yaelekea wote mliokuwa kwenye msafara ima hamna uzoefu na masuala hayo au mmejaa kiburi.
 
Kwani mngetoa kiasi na si yote mngepungukiwa nini?

Yaelekea wote mliokuwa kwenye msafara ima hamna uzoefu na masuala hayo au mmejaa kiburi.
Kwani wangepokea yote wangepungukiwa nini? Wangetaja nusu basi tujue moja! Kama kulipa zote ni kiburi basi hata kukataa kupokea zote ni kiburi!
 
Back
Top Bottom