Kwanini Patrick Rutabanzibwa (katibu mkuu wa ardhi) anaenda jela?

Ameidharau amri halali ya mahakama ya ardhi kuhusu mgogoro wa viwanja viwili msasani peninsula. lakini sio lazima aende jela kuna faini ya shilling laki tano au jela miezi 6. am sure atalipa hizo laki 5.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
mkuu hawa ni wakufilisi kabisa. yaani hawa ndo source ya sisi kuwa masikini wakutupwa kwenye nchi ambayo inajiita ina amani kwa miaka 50 ya uhuru wa bendera.
 
I FAIL to understand,some say he is cleaner then white,some say he is a fisadi- which is which
Ninavyomfahamu mimi, PR ndiye the strictiest PS we have now. Ni no-nonsense PS na karibu kila anapowekwa huishia kutofautiana na waziri wake kwasababu mawaziri wengi ni watupu sana. Pale alipo yuko na waziri makini, hao wenye viwanja wanayajua madudu waliyoyafanya na kukimbilia mahakamani.
 
huyu ni msafi aliyakataa ya Kaka yake Richmond yaani IPTL akaletewa matata sana mpaka kutishiwa kifo. Y kuwa fisadi sijui hata ka magufuri wanakasema basi kama ni hiyvo (Majairo) makatibu wote mafisadi.
 
mkuu hawa ni wakufilisi kabisa. yaani hawa ndo source ya sisi kuwa masikini wakutupwa kwenye nchi ambayo inajiita ina amani kwa miaka 50 ya uhuru wa bendera.
Usikurupuke. Kwanza uliza, mahakamani amepelekwa kama mtuhumiwa au kama mtetezi wa maslahi ya umma? Baada ya hapo utakuwa na haki ya kuhukumu.
 
Ndugu zangu tutunze heshima ya kuitwa "Great Thinkers", kama humjui mtu usitende dhambi ya ushabiki na kuchafua hali ya hewa au kumsafisha asiyesafishika. Kwa wanaomfahamu PR na utumishi wake, Tanzania haina watumishi wengi waadilifu kama mtu huyu. Alipinga vikali IPTL, leo (miaka 17 baadaye) hata mtoto mdogo anajua ubaya wa dili la IPTL. Amefanya mengi mazuri kwa taifa hili, wewe nami hatuwezi. Kwanza ukikaa naye nusu saa unagraduate digrii ya kwanza.

Amesafisha Wizara ya Maji, kasafisha Wizara ya Mambo ya Ndani, na sasa anasafisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Akiwa Wizara ya Mambo ya Ndani, alishauri kuwa Mradi wa Vitambulisho ulivyobuniwa na wanaotakiwa kutunza usalama wa watu na mali zao utaiingiza Serikali kwenye kashfa nzito (wakamuhamisha) subiri kidogo uone madudu yajayo.

Huku aliko kakuta UFISADI PAPA WA ARDHI uliokubuhu kwa zaidi ya miongo minne. Huku kuna ka-mchezo ka kuuza viwanja vilivyopangwa kubaki kwa matumizi ya wazi. Kamchezo ako ni kati ya Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na Mafisadi wa Ardhi na ni ka muda mrefu. Kwa mchezo huo, mafisadi huchukua maeneo rasmi ya wazi, wakipigwa stop na mamlaka husika (Kamishna wa Ardhi) hukimbilia Mahakama ya Ardhi kudai "settlement out of court" kwa kuwatisha watumishi wasiojiamini (au wala mlungula) kwamba wakikaidi watafungwa, ili hatimaye, Waheshimiwa wasio waaminifu watumie rungu la Nyumba inayoheshimiwa (Mahakama) kubariki DHULUMA KWA UMMA. Mabadiliko ya matumizi ya viwanja vya wazi hayawezi kufanywa kwa manufaa ya kikundi kidogo au mtu. Huu ni uvunjifu wa Sheria za Ardhi.Safari hii wamegonga mwamba wa kale (PR), hatishwi mtu, hafungwi mtu, na wala halipwi mtu. Wamechimba shimo, wataingia wenyewe. Hata majaji hawako juu ya sheria.

Ndugu zangu, watumishi wa ardhi wala rushwa na MAFISADI PAPA WA ARDHI, PR kawasambaratisha, baadhi yao naona wakichangi thread hii. Aidha, kumbuka anatafutwa KMK baada ya mzee wa sasa kustaafu na KM mtembeza bakuli kunyea kambi. Eti wanaangalia anayeweza kuwa KMK na kudhamiria kumharibia PR safari! Kama JK anataka kufanya usafi wa Serikali na kurejesha heshima amteue PR muone. Hata ule mtaji wa "POSHO" wa kambi fulani utakuwa kwishney! Anayemfahamu vizuri PR ni Padri Privanus Karugendo ambaye aliandika makala yenye mantiki, siku kumi zilizopita. Uliza ujuzwe.
 
mkuu hawa ni wakufilisi kabisa. yaani hawa ndo source ya sisi kuwa masikini wakutupwa kwenye nchi ambayo inajiita ina amani kwa miaka 50 ya uhuru wa bendera.
<br />
<br />
Uhuru upi mkuu!
 
Ndugu zangu tutunze heshima ya kuitwa "Great Thinker", kama humjui mtu isitende dhambi ya ushabiki na kuchafua hali ya hewa au kumsafisha asiyesafishika. Kwa wanaomfahamu PR na utumishi wake, Tanzania haina watumishi wengi waadilifu kama mtu huyu. Alipinga vikali IPTL, leo (miaka 17 baadaye) hata mtoto mdogo anajua ubaya wa dili la IPTL. Amefanya mengi mazuri kwa taofa hili, wewe nami hatuwezi. Kwanza ukikaa naye nusu saa unagraduate digrii ya kwanza.Amesafisha Wizara ya Maji, kasafisha Wizara ya Mambo ya Ndani, na sasa anasafisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Akiwa Mambo ya Ndani, alishauri kuwa Mradi wa Vitambulisho ulivyobuniwa na wanaotakiwa kutunza usalama wa watu na mali zao utaiingiza Serikali kwenye kashfa nzito (wakamuhamisha) subiri kidogo uone madudu. Huku alikokakuta UFISADI PAPA WA ARDHI. Huku kuna ka-mchezo ka kuuza viwanja vilivyopangwa kubaki kwa matumizi ya wazi kati ya Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na Mafisadi wa ardhi ka muda mrefu. Kwa mchezo huo, mafisadi huchukua maeneo rasmi ya wazi, wakipigwa stop na mamlaka husika hukimbilia Mahakama ya Ardhi kudai "settlement out of court" kwa kuwatisha watumishi wasiojiamini (au wala mlungula) ili hatimaye waheshimiwa wasiowaaminifu watumie rungu la nyumba inayoheshimiwa kubariki DHULUMA KWA UMMA. Safari hii wamegonga mwamba wa kale (PR), hatishwi mtu, hafungwi mtu, na wala halipwi mtu. Wamechimba shimo, wataingia wenyewe. Ndugu zangu, watumishi wa ardhi wala rushwa na MAFISADI PAPA WA ARDHI, PR kawasambaratisha, baadhi yao naona wakichangi thread hii. Aidha, kumbuka anatafutwa KMK baada ya mzee wa sasa kustaafu na KM mtembeza bakuli kunyea kambi. Eti wanataka kumharibia safari! Kama JK anataka kufanya usafi wa Serikali na kurejesha heshima amteue PR muone. Hata ule mtaji wa "POSHO" wa kambi fulani utakuwa kwishney! Anayemfahamu vizuri PR ni Padri Privanus Karugendo ambaye aliandika makala yenye mantiki, siku kumi zilizopita. Uliza ujuzwe.
Swadakta! Kama wapo wapambanaji basi huyu namweka mbele kabisa ya mstari..Katika list ya Dr.Slaa nadhani huyu akiingizwa jina lake kutokana na wadhifa wake lakini Patrick sii fisadi bali mpambanaji. Huyu ndiye aliyeibua sakata la IPTL na majuzi tu kawapa moyo wakazi wa Kigamboni ktk madai yao ya ardhi. Katika dunia hii ya Ufisadi kila Patrick anapokanyaga wafanyakazi huomba apigwe transfer maanake hukata mirija na urasimu hasa kwa viongozi wa juu.
 
Back
Top Bottom