Kwanini Patrick Rutabanzibwa (katibu mkuu wa ardhi) anaenda jela? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Patrick Rutabanzibwa (katibu mkuu wa ardhi) anaenda jela?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Natalia, Sep 5, 2011.

 1. N

  Natalia JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Ebu mtuambie amefanya nini
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu hujaeleweka tafadhali,, kulikoni?
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Ameidharau amri halali ya mahakama ya ardhi kuhusu mgogoro wa viwanja viwili msasani peninsula. lakini sio lazima aende jela kuna faini ya shilling laki tano au jela miezi 6. am sure atalipa hizo laki 5.
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Si wampe zote kwa mpigo?
  tena wamuongezee na viboko!
   
 5. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  I FAIL to understand,some say he is cleaner then white,some say he is a fisadi- which is which
   
 6. Deo Corleone

  Deo Corleone JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 14,655
  Likes Received: 2,510
  Trophy Points: 280
  Hv hivyo vi-faini mbona sivielewi? Huyu jamaa hv kwny Richmond hakuwepo?
   
 7. Deo Corleone

  Deo Corleone JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 14,655
  Likes Received: 2,510
  Trophy Points: 280
  Hv hvyo vifain mbna cvielew! Huyu jamaa hv kwny richmond hakwepo?
   
 8. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu hawa ni wakufilisi kabisa. yaani hawa ndo source ya sisi kuwa masikini wakutupwa kwenye nchi ambayo inajiita ina amani kwa miaka 50 ya uhuru wa bendera.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Ninavyomfahamu mimi, PR ndiye the strictiest PS we have now. Ni no-nonsense PS na karibu kila anapowekwa huishia kutofautiana na waziri wake kwasababu mawaziri wengi ni watupu sana. Pale alipo yuko na waziri makini, hao wenye viwanja wanayajua madudu waliyoyafanya na kukimbilia mahakamani.
   
 11. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahahaha! 'Viboko 12,sita akiingia na sita siku ya kutoka akamwonyeshe mkewe' -J.K.Nyerere
   
 12. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  huyu ni msafi aliyakataa ya Kaka yake Richmond yaani IPTL akaletewa matata sana mpaka kutishiwa kifo. Y kuwa fisadi sijui hata ka magufuri wanakasema basi kama ni hiyvo (Majairo) makatibu wote mafisadi.
   
 13. Plummie

  Plummie Member

  #13
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Patrick rutabanzibwa ni msafi...kwake maslahi ya umma ni mbele...
   
 14. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Usikurupuke. Kwanza uliza, mahakamani amepelekwa kama mtuhumiwa au kama mtetezi wa maslahi ya umma? Baada ya hapo utakuwa na haki ya kuhukumu.
   
 15. m

  mjusikafiri Member

  #15
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu tutunze heshima ya kuitwa "Great Thinkers", kama humjui mtu usitende dhambi ya ushabiki na kuchafua hali ya hewa au kumsafisha asiyesafishika. Kwa wanaomfahamu PR na utumishi wake, Tanzania haina watumishi wengi waadilifu kama mtu huyu. Alipinga vikali IPTL, leo (miaka 17 baadaye) hata mtoto mdogo anajua ubaya wa dili la IPTL. Amefanya mengi mazuri kwa taifa hili, wewe nami hatuwezi. Kwanza ukikaa naye nusu saa unagraduate digrii ya kwanza.

  Amesafisha Wizara ya Maji, kasafisha Wizara ya Mambo ya Ndani, na sasa anasafisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. Akiwa Wizara ya Mambo ya Ndani, alishauri kuwa Mradi wa Vitambulisho ulivyobuniwa na wanaotakiwa kutunza usalama wa watu na mali zao utaiingiza Serikali kwenye kashfa nzito (wakamuhamisha) subiri kidogo uone madudu yajayo.

  Huku aliko kakuta UFISADI PAPA WA ARDHI uliokubuhu kwa zaidi ya miongo minne. Huku kuna ka-mchezo ka kuuza viwanja vilivyopangwa kubaki kwa matumizi ya wazi. Kamchezo ako ni kati ya Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na Mafisadi wa Ardhi na ni ka muda mrefu. Kwa mchezo huo, mafisadi huchukua maeneo rasmi ya wazi, wakipigwa stop na mamlaka husika (Kamishna wa Ardhi) hukimbilia Mahakama ya Ardhi kudai "settlement out of court" kwa kuwatisha watumishi wasiojiamini (au wala mlungula) kwamba wakikaidi watafungwa, ili hatimaye, Waheshimiwa wasio waaminifu watumie rungu la Nyumba inayoheshimiwa (Mahakama) kubariki DHULUMA KWA UMMA. Mabadiliko ya matumizi ya viwanja vya wazi hayawezi kufanywa kwa manufaa ya kikundi kidogo au mtu. Huu ni uvunjifu wa Sheria za Ardhi.Safari hii wamegonga mwamba wa kale (PR), hatishwi mtu, hafungwi mtu, na wala halipwi mtu. Wamechimba shimo, wataingia wenyewe. Hata majaji hawako juu ya sheria.

  Ndugu zangu, watumishi wa ardhi wala rushwa na MAFISADI PAPA WA ARDHI, PR kawasambaratisha, baadhi yao naona wakichangi thread hii. Aidha, kumbuka anatafutwa KMK baada ya mzee wa sasa kustaafu na KM mtembeza bakuli kunyea kambi. Eti wanaangalia anayeweza kuwa KMK na kudhamiria kumharibia PR safari! Kama JK anataka kufanya usafi wa Serikali na kurejesha heshima amteue PR muone. Hata ule mtaji wa "POSHO" wa kambi fulani utakuwa kwishney! Anayemfahamu vizuri PR ni Padri Privanus Karugendo ambaye aliandika makala yenye mantiki, siku kumi zilizopita. Uliza ujuzwe.
   
 16. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Uhuru upi mkuu!
   
 17. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh lkn kumbukumbu zangu zinaniambia alikuwa kwenye list of shame! Sijui
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swadakta! Kama wapo wapambanaji basi huyu namweka mbele kabisa ya mstari..Katika list ya Dr.Slaa nadhani huyu akiingizwa jina lake kutokana na wadhifa wake lakini Patrick sii fisadi bali mpambanaji. Huyu ndiye aliyeibua sakata la IPTL na majuzi tu kawapa moyo wakazi wa Kigamboni ktk madai yao ya ardhi. Katika dunia hii ya Ufisadi kila Patrick anapokanyaga wafanyakazi huomba apigwe transfer maanake hukata mirija na urasimu hasa kwa viongozi wa juu.
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Mtu powa sana, ila ndio hivyo huwezi kuosha choo husinuke kinyesi, kwa jinsi system yetu ilivyo hata Malaika akifanya kazi ndani ya hii system lazima achafuke
   
 20. m

  mjusikafiri Member

  #20
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwembe Yanga Dkt alirusha mawe kwenye kichaka ili mafisadi wajitokeze. Hakumaanisha kila aliyetajwa kuwa ni fisadi. Alihisi kwamba kwa kuwa PR alikuwa PS wa Wizara ya Nishati na Madini, basi anajua nani mmiliki wa Meremeta na Tangold. Huyu jamaa ni MSAFI SANA.
   
Loading...