MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Otorong'ong'o,
Hawawezi kuelewa wanadhani wakatoliki tunakurupuka mpaka jambo litambulike lazima lipitie upelelezi yakinifu. Mfano watu wenye kuombea mapepo kupata kibali hiko kwa kanisa katoliki lazima upitie process nyingi lazima utoe pepo mbele ya viongozi ili idhihirike hufanyi utani
 
lete vifungu vinavyosema Mungu alisema acha porojo yapo mengi kibiblia Mungu alisema na mengine watu wanasema nenda kamauulize Paulo atakwambia
Sasa kwenye biblia mbona mungu ameongea Mara chache I.e Adam kaini na musa na wengine wachache Sasa unataka sema biblia Nzima is useless maana mungu ameongea Mara chache sana tuwe makini
 
Tunataka maandiko ndani ya Biblia Takatifu yaliyoandikwa mtu ukifanya dhambi ukatubu lwa binaadamu mwenzi pengine na yeye ana mizigo kukuzidi eti Maria Mtakatifu utuombee kasema nani? Utavuna ulichopanda leta maandiko acha kupotosha
Soma yohane kuanzia 20 utapata jibu
 
Tunataka maandiko ndani ya Biblia Takatifu yaliyoandikwa mtu ukifanya dhambi ukatubu lwa binaadamu mwenzi pengine na yeye ana mizigo kukuzidi eti Maria Mtakatifu utuombee kasema nani? Utavuna ulichopanda leta maandiko acha kupotosha
Yohane 20:21-23 ukisoma utaelewa tatizo wewe biblia husomi unamsikiliza mchungaji wako akikueleza mstari mmoja kwa masaa 6. Kuhusu kutoa sadaka
 
Ni kwl mkuu nina mjomba wangu ni padri nilienda kumtembelea pale ofcn kwao kurasini nkakuta friji yake imejaa mivinyo plus bia za kutosha akawa anapga bia kama kawaida kwhyo kwa mujibu wa biblia yao pombe kwao ni halali kbsa sikushangaa hata maparoko huwa wananyonya sana mivinyo
Soma barua ya Paulo kwa timotheo
 
amesahau october 15 kila mwaka ni siku ya bikira maria mpalizwa mbinguni, kapewa cheo cha queen of heaven cheo alichokuwaw akishikilia samiramis mke wa nimrod katika ibada za babeli iliyokuwa ikiadhimiswa kwa huyo mungu jua siku ya kwanza ya juma, jumapili sunday worshipers. rozari ni ibada za kipagani za miungu wa babeli ambayo imeridhishwa kizazi hata kizazi, Mungu kasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,katika karne hizo wakatoliki wengi awlipigwa marufuku kusoma Bibilia isipokuwa chuo kidogo cha sala na katekisimu, wale waliostaarabika kidogo walipewa misale ya waumini. siri hiyo ni kubwa imefunuliwa tu kwa wachache
Ila wasabato mnashida sana Hao miungu hata siwajui na wala sijawahi wafikiria mi naona wewe ndo mpenda miungu yamkini unaenda kwa waganga
 
Wangeikusanya wasingeichoma moto, Biblia ilikusanywa na Wakrtisto wa awali kabla hata wapagani wa kiroma hawajavamia kansani wakijifanya wameongoka kumbe lengo lao ni kuendeleza vita yao dhidi ya ukristo.. Ikiwa padre wako alikwambia Biblia ilikusanywa na waroma alikudanganya. Roman Catholic wamejikusanyia hiyo ya kwao wanayoiongezea vitabu kila mara. Biblia takatifu yenye vitabu 66 ilikamilishwa na waktisto wa awali kabla ya papa wenu kupewa madaraka na warumi.Upapa umeikuta Biblia na wakaongoza vita kuipiga vita ikiwemo kuwaua wote waliohifadhi nakala halisi ya Biblia.soma vizuri kisa cha waldensia waliokimbilia milina ya alps. Hawa walikimbia mateso ya papa na waliweza kuhifadhi nakala halisi ya Biblia sio hiyo waliochakachua waroma.
Postanti ndo mmechakachua lugha ya mwanzo ya biblia ni kipostant au kirumi
 
Yohane 20:21-23 ukisoma utaelewa tatizo wewe biblia husomi unamsikiliza mchungaji wako akikueleza mstari mmoja kwa masaa 6. Kuhusu kutoa sadaka

HAPANA

Hiyo mistari na mingine iliyotaja mtu kumsamehe mtu mwingine haina maana ya kuchukua nafasi ya Kristo au Mungu!!
Yesu kwenye Yohana Mtakatifu alizungumzia kutoamini kama dhambi na kwa hiyo aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kuwasamehe wapagani waliokuwa wamekubali kumpa Kristo maisha yao kwa kuamini. Msamaha hapa unasimamia kumpokea mtu kwenye ufalme wa Mungu. Kristo aliwapa wanafunzi wake hayo mamlaka lakini sio hizi zingine duh.

Wewe fikiria kama kweli Yesu alitoa mamlaka kwa binadamu kama sisi ya kusamehe, wote tunajua maisha ya mapadri, wachungaji na viongozi wote wa dini bila kujadili dhehebu wanavyoishi maisha machafu halafu hapo unampa mamlaka ya kusamehe. Hii inasikitisha kuamini kiurahisi mistari kama hii na kujipotosha kirahisi.

Muwe mnasoma Biblia kwa upana wake na kuelewa Biblia kwa maan ya Unabii wa Mungu na sio independent verses ambazo mara nyingi hupotosha. Ndio maana neno lasema, Andiko laua bali Neno lahuisha.

Yesu alikuja duniani kumpatanisha mwanadamu na Mungu na kwa hiyo hiyo huduma ya upatanisho kawaachia wanafunzi wake (Leo ni Kanisa) ili waendelee kumpatanisha mwanadamu na Mungu na kwa hiyo mwanadamu anayekubali kupatanishwa na Mungu huyo ndie mwenye sifa ya kusamehewa na yule ambaye hata baada ya kuambiwa habari za Mungu na akakataa huyo bado hajasamehewa na Yesu alikuwa akiongea kwa Context hiyo.

Ukisoma Marko 6: 11 inaelezea habari ya kukung'uta mavumbi na kuwaacha kama mtu hatawapokea na kukubali Neno la Mungu. Pia Paulo na Barnabas walifanya hivyo hivyo kule Pisidian Antioch baada ya kukataliwa waliwakungutia mavumbi na kuwaacha Matendo 13: 51
 
lembu, Hapo ndo ubishi wenu Sasa yesu si angesema vyengine ameshasema pokeeni roho mtakatifu yeyeto mtakayemsamehe dhambi amesamehewa na yeyote mtakaye mfungia dhambi amefungiwa kama unapingana na maagizo ya yesu na kazi za roho mtakatifu endelea na ufarisayo wako.
 
lembu, Hivi wewe unaweza kujua biblia zaidi ya kanisa katoliki lenye miaka 2000 wewe kama umeishi sana unamiaka 100. Sasa sijui unataka jifanya ni mkuu kuliko kanisa la bwana
 
Na ujerumani wengi ni wakatoliki yani waluther wengi wapo bongo

Baada ya Ujerumani mashariki kuungana na magharibi waprotestanti ni wengi kuliko wakatoliki. Ukiwaingiza wa austria ndio idadi ya wakatoliki ujerumani ina karibia kidogo waprotestanti. Officially wanasema 1/3 ni wakatoliki, 1/3 ni waprotestanti, 1/3 hawana dini. Lakini kiukweli waprotestanti ni wengi zaidi.
 
Taja vitu vitano wa kristo wa leo wanavipinga kutokana na kutoujua ukristo kwa historia yake......nb weka siasa pembeni
 
.
*uandishi wako unaonyesha kua huijui historia ya kanisa,,,
kwa mfano huzungumzii sala kwa bikira maria na cheo chake cha umalkia, ubatizo,,, imani, na neno..
Kwani sala ya Bikira Maria (japo umeandika jina lake kwa herufi ndogo) ina tatizo gani. Ni maneno ya kutoka kwenye Biblia toka kwa Malaika Mkuu Gabriel kama amkio na maneno ya shangazi yake Maria akiitwa Elizabeth. Labda nikukumbushe amkio ili. Salamu Maria umejaa neema umebarikiwa kuliko wanawake wote (Malkia) na yule utakayemzaa (aliyeko tumboni mwako amebarikiwa) - (“salaam Maria ewe uliyebarikiwa na Mungu! Bwana yuko nawe” Lk 1:28.)

Ona Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, “Mama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).

Habari nzima hii hapa: anzia haya ya 39 -45

39 Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,
40 akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti.
41 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
43 Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
44 Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
45 Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
Sasa wewe ni nani upinge kilichoandikwa. Wewe ni nani useme salamu ambayo Wakatoliki wanamuamkia Bikira Maria si halali wakati Malaika mkuu amemwamkia Maria na Mama yake Yohana Mbatozaji mama Elizabeth amefanya hivyo?
 
Hahaha ....unapopinga angalia usitende dhambi ....neno la Mungu ni nini? Kuna andiko kwenye Biblia ambalo si neno la Mungu? Unajua neno la Mungu ni Mungu mwenyewe? Ukisema alisema Maria si Mungu ina maana mafundisho ya mitume ni ya mitume si Mungu? Tatizo lenu mnapopinga Ukatoliki mnajisahau hadi mnavuka mstari.
Wanajitoa ufahamu wapate sadaka Kwa waumini wanaotafuta mambo ya dunia
 
Tunataka maandiko ndani ya Biblia Takatifu yaliyoandikwa mtu ukifanya dhambi ukatubu lwa binaadamu mwenzi pengine na yeye ana mizigo kukuzidi eti Maria Mtakatifu utuombee kasema nani? Utavuna ulichopanda leta maandiko acha kupotosha
Utuombee sisi wakosefu... Tatizo nyie mwajifanya watakatifu
 
Back
Top Bottom