MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Wapo watakaoamshwa mara Yesu ajapo, lakini siyo Bikira Maria.
Kwa kifupi ni kwamba, huwezi kumlinganisha Bikira Maria na mtu yeyote awaye yote.
Hata katika mazingira ya kawaida kabisa, MAMA wa mtu maarufu huheshimiwa sana, kwa mfano MAMA wa Rais wa nchi ni lazima ataheshimiwa karibu sawa na anavyoheshimiwa Rais mwenyewe.
Je, MAMA aliyemzaa Mkombozi (Mungu ) asiheshimiwe?
 
Kama mama wa laisi gani hapa kwetu tz anae eshimiwa au naww umetoka ndotoni
 
Mm nilisha waambia ninyi wa Rc mutuletee maandiko ya kibiblia yanayo kubaliana yakwamba bikira mariamu yuko mbinguni nikipatikana andiko moja linalokili hivyo siingii tena jf
 
Huyu bikira maria munae msema baada yakumzaa yesu aliendelea na maisha yake yy namumewe naakaendela kuza nakuzaa watoto wengi tu.ndomaana biblia inawatambua nduguze yesu..ukisoma biblia utawaona nduguzake yesu ..nahuyu bikira aliishi kama wengine nakisha akafa kama wengine ..hizi habali eti alipaa mbinguni niuongo uliopindukia naupaganani ..kama munabisha leteni maandiko ya kibiblia.. Sio blaha blaha
 
Hivi martin luther wa ihave a dream na na huyu wa kanisa ni watu wawili tofauti maana sjaelewaga jamn
 
Ndugu yangu, si kila kitu lazima kiandikwe kwenye Biblia. Kuna mambo ambayo yalitokea baada ya kuandikwe Biblia, hivyo mambo hayo ndiyo yanayoitwa MAPOKEO. Hata hivyo Biblia yenyewe inakiri kwamba kuna mambo mengi aliyoyatenda Yesu ambayo hayakuandikwa kwenye Biblia. Biblia inasema kuwa kama yangeandikwa mambo yote kwenye Biblia, Dunia ingejaa vitabu.

Lakini pia ni udhaifu wa hali ya juu sana wa FIKRA kutegemea kila kitu kiandikwe kwenye Biblia.
Binadamu ana akili na utashi, hivyo basi inatarajiwa kuwa Binadamu yeyote atumie pia akili zake kuambanua mambo kuliko kusubiri tu kuandikiwa na mtu mwingine.

MAPOKEO ni muhimu pia katika maisha yetu ya kawaida. Hata hawa wazazi wetu ni MAPOKEO. Ni MAPOKEO kwa sababu wewe mwenyewe huwezi kuthibitisha kuwa yule ni mama yako kwani huwezi kujua kuwa ni kweli ulizaliwa na yule mama au la?

Naomba kuwasilisha.
 
Habali za mapokeo yesu aziliyapiga malufuku .. Naakasema mufatamapokeo yawazee wenu nakuaacha maneno yangu yakweli..yaletayo uzuma ..
 
Acheni kulaghai watu kuweni wawazi biblia ndio msingi wa wakiristo sivinginevyo wala hayo mapokeo mnayo yafata
 
Biblia haikuandikwa na Kanisa Katoliki! Iliandikwa miaka mingi sana kabla ya uwepo wa Katoliki...Bibilia ilikuwepo kabla ya ujio wa Yesu.
Martin Luther King alileta mageuzi makubwa ya kiimani,ikumbukwe enzi hizo za utawala wa Rumi ilikuwa marufuku kwa mtu wa kawaida yaani mkristo wa kawaida kusoma Biblia badala yake wali dilute Biblia na kuanzisha Mithali za waumini!...enzi hizo msamaha ulikuwa unatozwa fedha tena fedha nyingi na wakati mwingine uliweza kulipia gharama fulani na kwenda kufanya maasi
Siku moja Martin Luther King akiwa anapita kwenye kitaa huko Ujerumani akaona kutabu kikubwa chenye jalada jeusi akakinunua,wakati anakisoma ndio akaona andiko kuwa kwa kupigwa kwake tumesamehewa Bure!
Akaanza kuhoji kwa wakubwa wa Vatican kwa nini watu walipishwe wakato msamaha ni Bure?hapo ndio mgigoro ulianza na kwa wakati huo Vatican wakaogopa kumwua maana ilikuwa miaka michache tangu wamwue Galileo Galilei

Nb soma 99 Thesis of Dr Martin Luther King
 
Biblia haikuandikwa na Kanisa Katoliki! Iliandikwa miaka mingi sana kabla ya uwepo wa Katoliki...Bibilia ilikuwepo kabla ya ujio wa Yesu.
Sijui kama unajitambua kweli wewe...?

Hata wakati wa Yesu Biblia kulikuwa hakuna...Biblia imekamilika mwaka 300 AD....Vitabu vyote vya Agano jipya vimeandikwa baada ya miaka na miongo mingi kupita toka Yesu Afufuke.. Sijui kama unalielewa hili..

Kingine Kanisa Katoliki ndio lime-compile Biblia Takatifu.....
 
Martin Luther King alileta mageuzi makubwa ya kiimani,ikumbukwe enzi hizo za utawala wa Rumi ilikuwa marufuku kwa mtu wa kawaida yaani mkristo wa kawaida kusoma Biblia badala yake wali dilute Biblia na kuanzisha Mithali za waumini!..
Biblia kipindi hiko ikikuwa ikichukuliwa kama Kitu adhimu sana ambacho mtu hatakiwa ku-temper nacho hovyo hovyo(Sacred).. Hivyo ni watu wachache waliruhusiwa kuwa na Biblia ....
 
Rejea Kitabu cha Mhubiri 7:12

Nayo mwili hurudi mavumbini ulikotoka nayo Roho kumrudia Mungu aliyeitoa .....

Roho haifi kamwe...

Soma ufunuo 5:8 uone Watakatifu wanafanya kazi gani mbinguni..
Dini ama imani, tuseme baadhi ya maeneo zina mkanganyiko wa mafundisho?
Naomba uniwekee sawa haya mambo.
Itakuwaje siku ya kiama ama siku ya mwisho?
Anapokufa mtu, roho yake huenda jehanamu ama peponi kutokana na matendo yake?
Kama yote hayo yanafanyika pindi mtu anapokufa, hiyo siku ya hukumu, yaani kiama inamaana gani kama hukumu tayari ilishatolewa?
Ama hakuna peponi wala jehanamu hadi siku ya kiama?
Haya mambo ya kiimani, ninavyoona mimi ni kama hayajawahi kuwekwa sawa katika dini ama dhehebu lolote lile, kwa kuwa kila dini ama dhehebu wanaimba ngonjera zao. Ninaomba ufafanuzi juu ya hilo ili kuniweka sawa.
 
Sijui kama unajitambua kweli wewe...?

Hata wakati wa Yesu Biblia kulikuwa hakuna...Biblia imekamilika mwaka 300 AD....Vitabu vyote vya Agano jipya vimeandikwa baada ya miaka na miongo mingi kupita toka Yesu Afufuke.. Sijui kama unalielewa hili..



Kingine Kanisa Katoliki ndio lime-compile Biblia Takatifu.....

Wewe ndio hujitambui mkuu
Biblia ilikuwepo kabla ya Kuzaliwa kwa Yesu,ni Biblia ndiyo iliyitabiri kuzaliwa kwa Yesu!
Baada ya kuzaliwa kwake ndio wanafunzi wake wakaongeza vitabu ambavyo leo vinaitwa agano jipya!
Bibilia ya kwanza iliandikwa kwa lugha ya Kiebrania!

Nenda kafanye homework ujui lini ukatoliki umeanza!

Orthodox ni kanisa la kwanza hata kabla ya Ukatoliki na walitumia Biblia!
 
Back
Top Bottom