MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

High Church ndugu halina tifauti na Catholic Church...Na Rozari kule tunasali vizuri....

Low Church walitaka kujifananisha na Lutherans hivyo waka-copy kila kitu kutoka Lutheran

Kama kweli wewe ni Anglican High Church nenda pale Cathedral ya St. Alban posta DSM, then angalia mandhari ya ndani ya Kanisa, kisha Nenda St. Joseph Cathedral posta ungalie uone kama utaona tofauti ....Hakuna tofauti
Mkuu hiyo rizali unaisali Anglikana? wew jamaa ni muongo sana yani anglikana anasali rozali, shame on you..

Ngoja nikwamvie iko hivi Kanisa Anglikana jimbo la Tanzania imegawanyika katika liw church na high church kulingana na Dayosisi.. Dayosisi ya Dar es salaam ni high iko chini ya Bishop Mokiwa hakuna kitu kama hicho, biblia tunatumia kama wanazotumia wapentecoste, tofaut ya high church na low church ni Namna ya uendeshaji wa ibada kwamba hawa high church wanaendesha kwa kuimba lakin liw church ni kwa kuongea, lakini litrugia ni ile ile.. acha kuudanganya umma tangu lini anglikana ikawa na rozali!!!
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Tatizo LA darasa la saba kuzuia pombe na PhD padres kuruhusu watu kunywa pombe nani mwenye uelewa zaidi??? Mfumo wa hilo dhehebu unalolitetea lipo kiutawala zaidi kuliko kiroho. Angalia mfumo wa utendaji wake, watu hawakemewi kwa dhambi zao ili mradi wapowapo tu kwenye u katoliki. Wawe wazinzi, walevi kupindukia, wanywao kidogo ila hawalewi...waendao kwa waganga na mahirizi viunoni ila bora tu waendelee kuwa wakatoliki ni saws. Jiongeze
 
Mtu hawez kwenda kwa baba ila kwa njia yangu.. Yesu anejiweka kuwa mtu wa kwanza kumuona kabla ya kufika kwa baba ni kama receptionist.. Sio koss kumuomba Mungu moja kwa moja, habari za kumtaka mtu akuombee zilikua enzi hizo ambapo makuhani hiyo ndiyo ilikua kazi yao kwamba mtu wa kawaida alikua hana uwezo wa kupiga magoti na kumuomba Mungu isipokua alipaswa kupeleka sadaka yake kwa kuhani na mahitaji yake kuhani ndio anamuombea, lakiniujio wa Yesu ulivunja vifungo vyote na ndio maana anasema Ombeni nanyi mtapewa halaf anasema ni nani ambae anaweza kumpa nyoka mwanae amuombae samaki.. maana yake ni kuwa sisi ni watoto yeye ni baba haina haja ya kupita pita sijui kwa maria au kwa nani, pray direct yupo aliyepewa jukumu la kutusaidia kuomba ambae ni Roho mtakatifu huyu hutusaidia kuomba maana peke yetu hatuwez kuomba ipasavyo....

Nahisi wewe sio Mkristo.Kama ni Mkristo basi endelea kujifunza kwa bidii neno la Mungu kwa sasbabu ni mchanga sana.
Huna hadhi ya kubishana na watu humu.Bora uwe msomaji ili ujiongezee Maarifa.

Soma vifungu vifuatavyo vikusaidie.

1.Rom.15:30-32
2.Efe.6:18-20

zote hizo zinahamasisha aombewe na wakristo.
 
Mkuu hiyo rizali unaisali Anglikana? wew jamaa ni muongo sana yani anglikana anasali rozali, shame on you..
Hahahahaha! Duuh yani wewe ni jinga kabisa....
Anglican high church wasali Rozari vizuri...Pole kama ulikuwa hujui..sasa nimekufahamisha .nijukumu lako kwenda kufanya utafiti...

Ngoja nikupe hii..

Kila tarehe 18 July Ni Siku muhimu kwa Kanisa la Anglican Uingereza maana ni siku ya "Our Lady of Walsingham"

Sherehe hii, husherejewa pamoja na Wakatoliki wote...Catholic, na Anglican huungana pamoja kuadhimisha siku hii muhimu ya B/ Maria kwa kusali Rozari na misa Takatifu....
 
Deogratius Kisandu,
kwahiyo unataka kutuambia kwamba unataka kupata legitimacy ya vitabu vya wamakabayo na akina joshua bin sira iliyoongezwa na kanisa katoliki katika Bibilia kwa ajili ya matakwa yao binafsi, badala ya 66 wao wamefanya 72
 
Mkuu hiyo rizali unaisali Anglikana? wew jamaa ni muongo sana yani anglikana anasali rozali, shame on you..

Ngoja nikwamvie iko hivi Kanisa Anglikana jimbo la Tanzania imegawanyika katika liw church na high church kulingana na Dayosisi.. Dayosisi ya Dar es salaam ni high iko chini ya Bishop Mokiwa hakuna kitu kama hicho, biblia tunatumia kama wanazotumia wapentecoste, tofaut ya high church na low church ni Namna ya uendeshaji wa ibada kwamba hawa high church wanaendesha kwa kuimba lakin liw church ni kwa kuongea, lakini litrugia ni ile ile.. acha kuudanganya umma tangu lini anglikana ikawa na rozali!!!
Soma Ufunuo uone jinsi Yohane anapata ufunuo..

"Tazama ishara ikaonekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota 12 juu ya kichwa chake"
Kwa hiyo hiyo ndiye Bikra Maria mwombezi? The Kingdom of God had got no a Queen! Only the King Jesus ndiyo mtawala wa mbingu na nchi mengine yote madoido na hadithi za kuunga unga ili kuiendeleza dini ya wenye nayo.
Na ukisoma hivyo VITABU vilivyoondolewa vingine vinafundisha uganga na ni kama hadithi tu...
 
kwahiyo unataka kutuambia kwamba unataka kupata legitimacy ya vitabu vya wamakabayo na akina joshua bin sira iliyoongezwa na kanisa katoliki katika Bibilia kwa ajili ya matakwa yao binafsi, badala ya 66 wao wamefanya 72
Aliyekuambia kanisa Katoliki limeongeza vitabu ni nani.. ?

Kumbe ulikuwa hujui Luther ndiye aliyepunguza vitabu ehhh!
 
Kwa hiyo hiyo ndiye Bikra Maria mwombezi??? The Kingdom of God had got no a Queen! Only the King Jesus ndiyo mtawala wa mbingu na nchi mengine yote madoido na hadithi za kuunga unga ili kuiendeleza dini ya wenye nayo.
Na ukisoma hivyo VITABU vilivyoondolewa vingine vinafundisha uganga na ni kama hadithi tu...
Unapingana na maandiko?
 
Lakini Wa kristo ambao siyo wakatoliki kuna swala mnanitatiza sana ivi kwanini mnakua wazito kuutambua mchango Wa mama maria katika ukombozi Wa dunia hii, ivi unawezaje kuumwabudu mwana na ukaacha kumweshimu mama , kuusu mama maria nadhani niwakati Wa maadhehebu mengine ya kikristo kujitazama na kuumpa nafasi katika maisha yao, sikia nikwambie karne zilizo pita mwana mmke alidharauliwa sana na nadhani ndiyo sababu ya madhehebu mengi kutokumpa huyu mama nafasi katika makanisa yao
Mhh kwa hiyo yesu ni mtoto wa maria na Mungu mwana aliyetumwa kuikomboa dunia, maria hawezi kuabudiwa cha ajabu zaidi hadi mnachonga sanamu kwa imani sanamu hiyo ndio Maria au yesu mwenyewe na kuzisujudu,,,..... Ngoja nijaribu kufunga mjadala kwa kusema imani yako ndio itakuponya na si knisa unaloenda kusali kila jumamosi na jumapili au ijumaa

ukatoliki ni dini iliyokuwepo hata kabla ya Yesu.
walikuwa serikali na makao makuu yao ndio leo ni makao ya kanisa
kuna siri kubwa ndani yao.

Ngoja nikuache maana umeamua kujitoa ufahamu
 
Otorong'ong'o,
amesahau october 15 kila mwaka ni siku ya bikira maria mpalizwa mbinguni, kapewa cheo cha queen of heaven cheo alichokuwaw akishikilia samiramis mke wa nimrod katika ibada za babeli iliyokuwa ikiadhimiswa kwa huyo mungu jua siku ya kwanza ya juma, jumapili sunday worshipers.

rozari ni ibada za kipagani za miungu wa babeli ambayo imeridhishwa kizazi hata kizazi,
Mungu kasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,katika karne hizo wakatoliki wengi awlipigwa marufuku kusoma Bibilia isipokuwa chuo kidogo cha sala na katekisimu, wale waliostaarabika kidogo walipewa misale ya waumini. siri hiyo ni kubwa imefunuliwa tu kwa wachache
 
Kanisa katoliki ndilo lililoongeza hivyo vitabu kwenye biblia hapo awali yalikuwa ni mafunndisho tu ya wayahudi lakini wakatoriki waliona yanafaa kufundishia wakayaingiza kwenye orodha ya vitabu vya biblia. Na mpaka leo maaskofu wa kikatoriki wanakiri kwamba tofauti iliyopo ni kuwa hayo mafundisho hayana uvuvio wa roho mtakatifu kama vitabu vile vingine
 
Yesu ni Mungu sawa na Baba na Roho Mtakatifu...Mungu anatuombeaje sasa....??

Kuwa makini, ndio maana Waislam wanawasumbua kuwa Yesu si Mungu....
Yesu hatuombei ila maombi yetu yanapitia kwa yesu, hakuna atakayefika kwa baba yanu bila kupitia kwangu
 
KANISA KATOLIKI NDILO LILILOONGEZA HIVYO VITABU KWENYE BIBLIA HAPO AWALI YALIKUWA NI MAFUNNDISHO TU YA WAYAHUDI LAKINI WAKATORIKI WALIONA YANAFAA KUFUNDISHIA WAKAYAINGIZA KWENYE ORODHA YA VITABU VYA BIBLIA. NA MPAKA LEO MAASKOFU WA KIKATORIKI WANAKIRI KWAMBA TOFAUTI ILIYOPO NI KUWA HAYO MAFUNDISHO HAYANA UVUVIO WA ROHO MTAKATIFU KAMA VITABU VILE VINGINE
Maaskofu gani hao..? Hebu wataje..?

Biblia iliyoasisiwa/ tengenezwa na kanisa katoliki daima ilikuwa na vitabu 73/72.....
 
wewe ndiyo kichwa maji, kasome hoja 95 za luther , na historia ya Biblia na historia ya kanisa katoliki, hata kwenye mtandao vinapatikana, ndiyo uje ujenge hoja zako.
Nadhani unaweza kuchangia bila kutumia maneno makali mkuu!!!
 
Aliyekuambia kanisa Katoliki limeongeza vitabu ni nani.. ?

Kumbe ulikuwa hujui Luther ndiye aliyepunguza vitabu ehhh!
acha uvivu kumbe hata husomi historia ya kanisa lako inaonekana wewe ni mmoja wa wale waliopigwa marufuku kusoma maandiko , kasome kitabu kilicho andikwa sinodi ya africa 1990 iliyoandikwa na Karol Luangwa akisaidiana na eusebius augustus. wameifafanua vizuri sana nyogeza ya vitabu hivyo, watakuambia Bibilia ya waebrania ina vitabu 66 na watakupa sababu ya wao kuongeza hivo vingine na mamlaka ya kufanya hivyo walipata wapi watakuambia ndipo urudi hapa tuendeleze mjadala. karibu
 
Biblia Takatifu imeandikwa ni heri kuoa au kuolewa kuliko kuaka tamaaa alikuwa sahihi kabisa mijitu mnazini huko mnaiba halafu unaenda kutubu kwa binaadamu mwenzako pengine huyo unaetubu kwake ana mizigo kuliko hata uliyokuwa nayo na imeandikwa amtimae mtu kwa kumtamani huyo azini sasa kwa macho ya kibinaadamu mwanaume rijali apite binti manshallah weee wacha kabisa kawadanganyeni hao hao siku ya mwisho kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe nasema ukiijua kweli nayo kweli itakuweka huru kwelikweli.
Nimejaribu kuconnect hoja yako na niliyoyaandika sijapata connection.... Hebu isome tena mkuu halafu ucomment bila kutumia lugha kali bro. Well, kama hujawahi kutenda dhambi ya uasherati au uzinzi, hongera sana mkuu!!! Nadhani moyo wako utasema zaidi ya vidole vyako!!!
 
Back
Top Bottom