MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Hii ni baadhi ya misingi mikuu ya imani ya Waadvenstista Wasabato, kama una swali zaidi kuhusu mismamo wa Waadvenstista Wasabato kuhusu Utatu Mtakatifu, niulize sitachoka
Misingi ya SDA siyo Utatu Mtakatifu kamwe ..ulichokiandika hapo umejichanganya sana...

SDA hamuamini Utatu Mtakatifu, mnaamini Polytheisism...
 
Kuna mtu anajiita Otorong'ong'o alikuwa anapotosha watu kuwa wasabato hawaamini Utatu Mtakatifu. hoja hii ni mahsusi kumpa ukweli ulivyo kuhusu wasabato.
Unataka nikupe uthibitisho jinsi ambavyo hamuamini ktk Utatu Mtakatifu...??

Hujui kuwa Ellen G White hakuamini utatu Mtakatifu...?

Unajua kwann mnaitwa Cult iliyofanikiwa....?
 
Misingi ya SDA siyo Utatu Mtakatifu kamwe ..ulichokiandika hapo umejichanganya sana...

SDA hamuamini Utatu Mtakatifu, mnaamini Polytheisism...

Waadventista wasabato huipokea Biblia kama kanuni yao pekee na hushika baadhi ya
misingi ya imani kuwa ndiyo mafundisho ya mabadiliko matakatifu. Imani hizi, kama
zilivyoorodheshwa hapa, hufanya welekevu wa kanisa na udhihirisho wa mafundisho ya
mabadiliko. Masahihisho ya kauli hizi yanaweza kutegemewa katika kikao cha Halmashauri
kuu wakati kanisa likiongozwa na Roho Mtakatifu kwenye ufahamu ulio kamili zaidi ya
ukweli wa Biblia au linapopata lugha iliyo bora zaidi ya kuelezea mafundisho ya Neno
Takatifu la Mungu.

1.Maandiliko Matakatifu
Maandiko Matakatifu, yaani Agano la kale na Jipya ndiyo Neno la Mungu lililoandikwa,
likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia kwa watu watakatifu walionena na kuandika kama
walivyoagizwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu
maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa
wa mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye mamlaka
wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya mungu katika historia.
(2Petro 1:20,21. 2Timotheo 3:16,17. Zaburi 119: 105. Mithal 30: 5,6. Isaya 8:20. Yoh
17:17. 1Wathe 2:13. Waeb4:12.)

2.Utatu Mtakatifu
Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele.
Mungu hapatikani na mauti, mwenye nguvu zote, ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko
daima. Yeye hana mwisho na ni zaidi ya ufahamu wa kibinadamu, hata hivyo anafahamika
kupitia kujifunua kwake binafsi. Milele zote yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa, kutumikiwa
na viumbe vyote. (kumb 6:4. Mith 28:19. 2kor 13:14. Waef 4:4-6. 1Petr 1:2 1Tim 1:17
Ufunuo 14:7)

3.Baba
Mungu Baba wa milele ndiye muumbaji, Chimbuko, Mtengenezaji, na Mfalme wa viumbe
wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, Mwingi wa rehema,, mwenye fadhili, si mwepesi wa
hasira, na mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu. Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa
ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba. (Mwanzo 1:1 Ufu 4:11.
1wakor 15:28. Yoh 3:16. 1Yoh 4:8. 1Tim 1:17. Kut 34:6,7. Yoh 14:9).

4.Mwana
Mungu Mwana wa milele alifanya mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote
viliumbwa, tabia ya mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakaribishwa na
ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu
aliye kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira
Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu
alioonyesha kwa mfano wa haki na u[endo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha
uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa hiari
msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, Alifufuliwa kutoka kwa wafu,
na akapaa kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika
utukufukwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote. (Yoh 1: 1-3,14. Wakol 1: 15-19,. Wafil 2:5-11. Yoh 10:30, 14:9 Warum 6:23. 2Wakor 5:17-19.
Yoh 5:22. 1Wakor 15:3,4. Luka 1:35. Yoh 14:1-3)

5.Roho Mtakatifu
Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji,
kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko matakatifu.
Alijaza maisha ya kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu, na wale
wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba
na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa,
huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa upatano wa maandiko uliongoza kwenye ukweli
wote. (Mwa 1,2. Luka 1:35, 4:18. Mdo 10:38. 2Petr 1:21. 2Wakor 3:18. Yoh 14:16-18,26,
15:26,27, 16:7-13)


6.Uumbaji
Mungu ni muumba wa vitu vyote, na amefunua katika maandiko uhalisi wa tukio la
shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya “Mbingu na Nchi” na vitu vyote
vilivyoko hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Na hivyo
akaanzisha sabato kama kumbukumbu ya milele ya kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji.
Mwanaume na Mwanamke wa kwanza walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo wa
kazi yake ya Uumbaji, wakapewa utawala juu ya ulimwengu, na wakaagizwa kuajibika na
utunzaji wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana”
ukitangaza utukufu wa Mungu. (Mwa 1,2. Kut20:8-11. Zab 19:1-6, 33:6-9, 104. Waebr
11:3)


7.Asili ya Mwanadamu
Mwanaume na Mwanamke walifanyawa kwa mfano wa Munguwakiwa kila mmoja na nafsi
yake, uwezo na uhuru wa kufikirina kutenda. Ingawa waliumbwa viumbe huru, kila mmoja
ni umoja wa nafsi isiyogawanyika ya mwili, akili na roho, akimtegemea Mungu kwa uhai na
pumzi na mengine yote. Wakati wazazi wetu wa kwanza walipomwasi Mungu, walikana
utegemezi wao kwa Mungu na wakaanguka kutoka hadhi yao ya juuchini ya Mungu. Sura
ya Mungu iliyopo ndani yao ikaharibika na wakawa chini ya mauti. Wazao wao hushiriki
asili hii ya kuanguka na matokeo yake. Wanazaliwa wakiwa na udhaifu na mivuto ya
kuelekea kwenye uovu. Lakini Mungu katika kristo aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake,
na kwa Roho wake hurejesha ndani ya mwanadamuwatubuo sura ya muumba wao.
Wakiwa wameumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu, wanaitwa kumpenda na kupendana
wao kwa wao na kutunza mazingira yao.(Mwa 1:26-28, 2:7. Zab 8:4-8. Mdo 17:24-28. Mwa
3. Zab 51:5 War 5:12:17. 1Yoh 4:7,8,11,20. Mwa 2:15


8.Pambano kuu
Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika katika pambano kuu baina ya kristo na shetani
kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake, na utawala wake juu ya ulimwengu. Ugomvi huu
ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa uhuru wa kuchagua, katika
kujiinua akawa shetani, mpinzani wa Mungu, na kupelekea sehemu ya Malaika kwenye uasi. Akaiagiza Roho ya uasi katika ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu na Hawa
kingia dhambini. Dhambi hii ya mwanadamu ilileta matokeo ya upotoshaji ya sura ya
Mungukatika wanadamu, Uvurugaji wa ulimwengu ulioumbwa, na mwishowe kuteketea
wakati wa gharika iliyokumba ulimwengu wote. Ukitazamwa na viumbe wote ulimwengu
huu ukawa uwanja wa vita ya ulimwengu, ambao kutokana nao Mungu wa upendo
hatimaye akathibitika kuwa mwenye haki. Katika kuwasaidia watu wake katika pambano
hili, kristo anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuongoza, kulinda, na
kutegemeza katika njia ya wokovu. (Ufu 12:4-9, Isa 14:12-14, Eze 28:12-18, War 1:19-32,
5:12-21, 8:19-22, 1Wakor 4:9, Waeb 1:14)


9.Maisha, Mauti na Ufufuo wa kristo
Katika maisha ya kristo ya utii mtakatifu kwa mapenzi ya Mungu, mateso yake, mauti na
ufufuo, Mungu alitoa njia pekee ya kafara kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu, ili kwamba
wale ambao kwa imani wanapokea upatanisho huu waweza kuwa na uzima wa milele, na
ulimwengu wote uweze kuelewa vizuri upendo mtakatifu usio na kikomo wa muumba.
Kafara hii kamilifu huthibitisha haki ya sheria ya mungu na fadhili za tabia yake, kwa
sababu hufanya vyote viwili kuhukumu dhambi zetu na kutupatia msamaha. Kifo cha kristo
ni cha badala na cha kulipia, kupatanisha na chenye kubadilisha. Ufufuo wa Yesu kristo
hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu, na kwa wale wanaopokea kafara
huakikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya dhambi na mauti. Kinatangaza ukuu wa Yesu
Kristo, ambaye mbele zake kila goti mbinguni na duniani litapigwa.(Yoh3:16, Isa13:1,
1Petr 2:21, 22,1Wakor 15:3, 4, 20-22, 2Wakor 5:14, 19-21. War1:4, 3:25, 4:25, 8:3, 4,
Wafil2:6-11)


10.Uzoefu wa Wokovu
Katika upendo usio na mwisho na rehema zake Mungu alimfanya Kristo, asiyejua dhamdi
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwambakatika yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu.
Tukiongozwa na Roho mtakatifu tunatambua hitaji letu, tunakili hali yetu ya kuwa wenye
dhambi, tunatubu maasi yetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana na Kristo,
kama mbadala na kielelezo. Imani hii inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo wa
kimbingu wan a ni karama ya neema ya Mungu. Kupitia kwa kristo tunahesabiwa haki,
tunafanywa kuwa wana wa binti za Mungu, na kukomesabiwa haki kutoka katika hali ya
kuwa chini ya dhambi. Kupitia kwa Roho tunazaliwa upyana kutakaswa, Roho hufanywa
upya nia zetu, huandika sheria ya Mungu ya upendo katika mioyo yetu, na tunapewa uwezo
wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani yake tunakuwa washiriki wa asili ya uungu na
tuna hakika ya wokovu sasa na katika hukumu. (2Wakor 5:17-21, Yoh3:16, Wag1: 4, 4:4-
7, Tito3:3-7, Yoh16:8, Wag3:13,14. 1Petr 2:21,22. Warumi10:17, 3:21-26, 8:14-17, 12:2.
Warumi8:1-4,5:6-10, 2Petr 1:3,4)


11.Kukua katika kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo
wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha
mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu utupatia ushindi dhidi ya nguvu
za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapo tembea naye kwa amani, fyraha, na
uhakika wa upendo wake.Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu.
Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu tunawekwa
huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya
nguvu za uovu, ujinga, na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali,. Katika
uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea
naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake kikamilifu, tukikusanyika pamoja kwa ajili
ya ibada, na kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo
wale wanaotuzunguka na kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia
ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa uzoefu wa kiroho. (Zab.1:1,2. 23:4, 77:11,12,
Kol1:13-14, 2:6, 14-15, Luka10:17-20, Efe5:19-20, 6:12-18, 1Theo 5:23, 2Petr 2:9, 3:18.
Fil3:7-14, Math20:25-28, Yoh20:21, Gal5:22-25, Rum8: 38-39, 1Yoh4:4, Ebr10

12.Kanisa
Kanisa ni jamii ya waumini wanaomkiri Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi katika
mfululizo wa kufungamana na watu wa Mungu katika nyakati za agano la kale, tunaitwa
kutoka katika ulimwengu, na tunajiunga pamoja kwa ajili ya ibada, kwa ajili ya ushirika, kwa
ajili ya mafundisho katika neno, na kwa ajili ya maadhimisho ya meza ya bwana, kwa ajili ya
huduma kwa wanadamu wote, na kwa ajili ya tangazo la injili ulimwenguni kote, kanisa
linapata mamlaka yake kutoka kwa kristo, aliye neno lililofanyika mwili, na kutoka katika
maandiko, ambayo ndiyo neno lililoandikwa. Kanisa ni jamaa ya Mungu, waliofanywa nay
eye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi katika misingi ya agano jipya. Kanisa ni mwili
wa Kristo, jamii ya weny imani ambayo kristo mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi
ambaye kwa ajili yake kristo apate kulisafisha na kulitakasa.Wakati wa kurudi kwake kwa
ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewew kanisa lenye utukufu, waaminifu wa karne zote,
walionunuliwa kwa damu yake, lisilo na waa au kunyanzi, lakini takatifu na lisilo na
ila.(Mwa12:3, Mdo:7:38, Waef4:11-15, 3:8-11, Math28:19,20, 16:13-20, 18:18,
Waef19:22,23, 5:23-27, Wakol1:17-18).
 
Nimeweka 12 tu hapo juu, ipo misingi 28 ya imani ya wasabato. Unaweza kuona hapo kisha uendelee kuwadanganya watu.

Nitaendelea na wa 13 mpk 28
 
Nimeweka 12 tu hapo juu, ipo misingi 28 ya imani ya wasabato. Unaweza kuona hapo kisha uendelee kuwadanganya watu.

Nitaendelea na wa 13 mpk 28
Acha vichekesho wewe...

Biblia yenu mpya (Clear Word Bible) inanesha jinsi mbavyo hamuamini katika Utatu Mtakatifu ila mnaamini ktk Polytheisism...

Hata Ellen G White hakuamini Utatu Mtakatifu..
 
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?

Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.


Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.


duuu
 
udhihirisho wa mafundisho ya
mabadiliko. Masahihisho ya kauli hizi yanaweza kutegemewa katika kikao cha Halmashauri

Ok! Sasa nimeelewa kwanini Mmeamua kufanya Editing ya Biblia na kuweka manuscript za Ellen G White...

Unaifahamu Clear Word Bible..?
 
Acha vichekesho wewe...

Biblia yenu mpya (Clear Word Bible) inanesha jinsi mbavyo hamuamini katika Utatu Mtakatifu ila mnaamini ktk Polytheisism...

Hata Ellen G White hakuamini Utatu Mtakatifu..
Naomba uielete hapa hiyo biblia hata link yake alafu uoneshe kuwa imechapwa ma wasabato
 
Ok! Sasa nimeelewa kwanini Mmeamua kufanya Editing ya Biblia na kuweka manuscript za Ellen G White...

Unaifahamu Clear Word Bible..?
Sasa Church Manual kubadilika ni dhambi acha ku quote vitu roborobo ili upotoshe? Hv kanuni za kanisa zikibadilika ni dhambi? Hiyo si ni kama katiba. Acha upotoshaji wa kijinga njoo na proof sio unawaambia watu vitu bila proof.
 
Sasa Church Manual kubadilika ni dhambi
Kumbe manuscript za Ellen G White ndio church manual zenu...?
Sasa ni kwamba hizo church Manual Zenu mmeenda kuziweka kwenye Biblia....

acha ku quote vitu roborobo ili upotoshe?
Nipotoshe kitu gani...?

Hv kanuni za kanisa zikibadilika ni dhambi?
Kama vinabadilika maana yake havikuwa divinely revelated..yalikuwa ni mawazo ya wanadamu, ndio maana mnaamua kuvibadilisha....Maana kama vingekuwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu kulikuwa hakuna haja ya kubadilisha....
Mf. Wasabato mlikuwa hamruhusu Women Ordination na ilikuwa ni kufuru kwa mwanamke kusimama madhabahuni....ila sasa GC imepitisha women Ordination...
Maana yake mafundisho ya katazo hilo awali yalikuwa ni mihemko ya Ellen White na sasa mmeamua kubadilisha kanuni...Si ndio...

Hiyo si ni kama katiba.
Ok! Kumbe mnatumia Katiba na siyo biblia..

Acha upotoshaji wa kijinga njoo na proof sio unawaambia watu vitu bila proof.
Link nimeshakuwekea na nimeku-mention
 
Mkuu kwa hili huna data.... Martine hakuwa Askofu, alikuwa Padre na miongoni mwa sababu zilizomuondoa kwenye kanisa Katoliki ni hili la Uaskofu, alipinga hairakia ya Kanisa na vyeo kama Uaskofu, Upapa na mengineyo. Sema tu mengi aliyoyapinga aliishia kuayatenda akiwa kwenye kanisa lake. Mengine ni suala la Useja, hakutaka kabisa kulisikia na alipoondoka aliondoka na Mtawa wa kike aliyeishia kuwa mkewe.

Mambo ni mengi sana na yanahitaji muda wa kutosha. Lakini niseme tu kwamba "siyo kila alilolipinga lilikuwa baya" mengine aliyapinga kihalali kabisa japo njia aliyoitumia haikuhalalisha kitendo chake!!!

Pili, Biblia za wapeotestanti na wapentekoste zina vitabu 66 wakati biblia ya Wakatoliki ina vitabu 72. Hili lilitokana na kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye vitabu hivyo (deuterokanoni) vinapingana na mafundisho yao. Sababu nyingi ni za kibinadamu tu!!! Hili lilikuwa rahisi sana kwake kwani suala zima la "Utaifa" liliingizwq kwenye huu mchakato wa Luther kujiondoa kanisa, matokeo yake kwa vile alikuwa Mjerumani, dhehebu lake likawa "dini dora" ya Ujerumani, katika hali kama hii, ni rahisi kwa uwezo wa kifedha kuchapisha Biblia zenye vitabi 66 na kuviondoa vile vingine!!!!
Hapo kwenye Biblia usitupotoshe. Vitabu vya apokrifa katika Biblia mmeviongeza wenyewe karne ya 16 baada ya baraza lenu la Trent kukaa na kuafiki. Kwa ufupi huijui historia ya Biblia
 
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?

Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.


Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.


ni suala lililo jema kuheshimu mawazo ya kila mmoja ili kujipa nafasi ya kujenga hoja mbali mbali na kusaidiana ili kupata muafaka. ninavyoelewa mimi kulingana na historia ya kanisa ni kama ifuatavyo,

- Papa Julius II akishirikiana na askofu mmoja aliyekuwa ujerumani walikuwa na mkakati wa kujenga kanisa kubwa la MTAKATIFU PETRO ambalo ndilo kanis kubwa kuliko yote duniani lililoko mjini Roma. ili kujipatia pesa za kutosha watu hao wawili waliandaa mkakati mmoja ambao ulisema kwamba, ili mtu aweze kusamehewa dhambi zake anatakiwa kutoa pesa( jambo hili lipo mpaka sasa katika kanisa katoliki likiitwa ibada ya kuwaombea marehemu) ili dhambi zake au za ndugu yake aliyefariki zifutwe mbinguni.

- papa akiwaa na askofu huyo walimwalika muhubiri mmoja aliyejulikana kw jina la Tetzel ambapo waliandaa vyeti walivyoviita vya rehema wakimaanisha kuwa mtu akinunua hata ndugu yake aliyefariki anapata ondoleo la dhambi. hili pia lilikuwa jambo mojawpo kubwa lililosababisha Martin Ruther kuolozesha makosa 95 ya kanisa katoliki mnamo tarehe 15 october 1517 .

-watu wengi sana wakiwemo maaskofu wenzake walimuunga mkono Ruther kuhusiana na mabo 95 juu ya rehema aliyoyabandika katika lango kuu la kuingilia ujerumani na jambo hili ndilo lililomfanya kutengwa japo aliitwa hata ajitetee bungeni lakini aliendelea kushikiria msimamo wke hu.

tutaendelea kuhabarishana.
 
Hapo kwenye Biblia usitupotoshe. Vitabu vya apokrifa katika Biblia mmeviongeza wenyewe karne ya 16
Unajua maana ya Apokrifa...? Au unaropoka...?


Acha kuchekesha umati....Biblia imekamilika ikiwa na Canon ya Vitabu 72/73

Tatizo kubwa hamkuwai kuambiwa ukweli huu....

Taarifa ni kuwa Bw Luther alipunguza vitabu 7 vya Agano Jipya....Na hakutosheka pia alitaka kupunguza vitabu vya Ufunuo, Yakobo na Waebrania....
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Mbona Biblia iko clear kuhusu namna ya kuomba? Hivi padre wako ndo anawafundisha hivyo? Hamjui ya kuwa sara ya maria ni copy ya upagani wa kirumi?
 
Umataka kupotosha na takataka zako hizo eti clear word. Nimekwambia njoo na statement ya kanisa ikionesha wanaikubali na ndio wachapaji wa hiyo sijui biblia

Official statement ya kanisa ni hii:

the church released the following statement:

The Clear Word Bible is not produced, nor endorsed by the Seventh-day Adventist Church, but is the private enterprise of an individual.The Adventist Church does not use the Clear Word edition, which includes passages from Ellen G. White’s writings, for its worship services and Bible studies around the world, but quotes from well known and well accepted Bible translations in the various languages. In the English language for example, the church uses the King James Version, the Revised Standard Version, the New American Bible, [sic] [recte New American Standard Bible] theNew International Version, and others

— Australasian Conference Association Limited[8]

David Newman, editor of Ministry magazine wrote a letter expressing concerns about The Clear Word (June 28, 1994), stating that "A cursory examination of the Clear Word Bible reveals the prolific addition of many ideas not found in Scripture."[9]

Others within the church, such as Phil Ward, have expressed criticism in two areas. One that the current publisher does not have a large enough footprint to get The Clear Wordout to mainstream Christian book centers, and that the paraphrase has too much extra material in it.[10]
 
Otorong'ong'o,
Hujui chochote kuhusu canon. Hujui chochote kuhusu Talmud wala synod wala septugiant. Huyu Martin Luther ni wa juzi, Biblia ni kitabu cha kale na waloongeza na kupunguza vitabu ni haohao wa kale. Shida yako unamponda Martin Luther kwa kuukosoa ukatoliki
 
Back
Top Bottom