MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Duh kaaazi kweli kweli hapo ndo mlipo mpa cheo binadamu mwenzenu awe mwombezi. mmesahau kwamba mariam na yeye ni binadamu kama niniyi na alishakufa anasubiri ufufuo siku ya mwisho.. sasa sijui nani kawadanganya kwamba maria yuko hai...... Au ni katika kitabu gani kimemtaja Mariam Kwamba yi hai ambapo anaweza kusikia maombi yenu

Mkuu we ninani hadi umpinge mtu ambaye aliweka agano na Mungu?unadhani uwepo wa bikra Mariam ni wakibahati mbaya?

soma Bible vizuri,halafu tuliza akili yako vzr,achana na mapokeo ya mafundisho ya wachungaji wako,fikiri vizuri,Wakati Mungu akimtumia ujumbe Mariam hapakuwepo na wanawake wengine,kwanini bikra Mariam?

Yaani Mungu Baba aweke agano la milele na Na Mama yule wewe useme she is noboby,ama kweli,watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa!!!!
 
Mm naona kuna haja hapa mtu atoe elimu kwanza ya uundwaji wa bibblia
Biblia ilikuwa compiled na Kanisa Katoliki(biblua ni kitabu cha kikatoliki)

na ukristu kabla ya kugawanyika .
Kulikuwa na Kanisa moja tuu, yaani Kanisa Katoliki.....Orthodox Church walijitenga na Kanisa Katoliki mwaka 1100..,,

Miaka ya 1500 huko, schism ilitokea na Luther alitengwa na Kanisa Katoliki...Hapo ndipo dhambi ya uasi ilianza kuenea kwa kasi na tukaanza kupata madhehebu kedekede

Na tujue kila maamuzi yalifanywa kwa maslahi either personal or kwa ukristu
Maamuzi gani...?
 
Wakuu mbona mnabishanana sana wakati wazungu walioleta dini/ madhehebu hayo wakila bata na kupiga hatua za maendeleo kila kukicha?, cha msingi Naona kila mtu abaki na iman yake kukosoana na kutokwa na mapovu namna hii utadhan tulikuwepo wakati biblia inaandikwa hakuna maana. Kila mmoja asidharau iman ya mingine na hakuna aliye bora kuliko mwenzake as long as wote mmeumbwa kwa mf na sura ya Mungu
 
Akusaidie wewe nani...?
Mimi nimwanadamu ninae Muhitaji Yesu lakini wewe pia unamuhitaji Yesu ili akuweke huru na upotofu wa fikra na ufia dini kana kwamba tutaenda kuhukumiwa siku ya mwisho na dini zetu au dhehebu zetu NENO ndo litakalo tuhukumu.

Hivyo nyie endeleeni kumsihi bikra maria awaombee rehema na akati aliepewa mamlaka ya kusamehe na kutuombea ni Yesu kristo peke yake na si mtume yoyote wala nani!!! ila sio mbaya mkuu nyie hata mkifa dhambini padri akija kwnye maziko yako akaomba rehema unasamehewa ila kwa sisi ukifa hakuna kutubu wala kuombewa rehema kwa mujibu wa neno.
 
Aliondoa vitabu hivyo ili ku-suit mafundisho yake....

Ni sawa Walokole leo waondoe kitabu cha (Nyaraka ya paulo kwa Wakorinto) inayokataza mwanamke kusimama madhabahuni, simply ili kuruhusu wanawake wawe ordained
Now this isn't right kwa kweli
Tujifunze kwenda na ukweli sio kuondoa sheria kwa faida binafsi

Ahsante sana napata picha tutokako na tuendako
 
offg76,
Ni kwl hata mimi siku nikiona andiko linalosema bikra maria yupo hai na anatuombea siku hiyo nitarudi kama hiyo imani ya Roma, ninae mjua yuko hai ni Kristo yesu peke yake yuko hai milele na ndio atakaekuja kunyakua kanisa na mtu haendi kwa baba bila kupitia kwake na ndio muombezi wetu.

Swala la kwanini alitumiwa kubeba mimba Roho mtakatifu au Mungu huweza kumtumia yoyote aliemuumba na ndo maana Balaki alipo mwambia mchawi balaamu awalaani wana wa israel, wakati balaamu anaenda kuwalaani wana wa israel alikuwa amepanda punda na siku hiyo Mungu alimtumia huyohuyo punda kutamka maneno kama mwanadamu.

kwahiyo hatuwez kusema punda ni mtakatifu anafaa kutuombea kisa alitumiwa na Bwana Mungu,Mungu anaweza kumtumia yoyote kwa ajili ya kazi yake maana vyote alivyoviumba viko ndani ya uwezo wake kuvitumia atakavyo,Kwhiyo mariam ni mtakatifu kwa sababu alimbeba mtakatifu na ni mbarikiwa kwa sababu alimbeba katika tumbo lake yule aliekuwa amebarikiwa hata neno linasema hata sisi tutakuwa watakatifu maana alie ndani yetu ni mtakatifu.

kwhiyo maryam kumzaa Yesu alitumiwa tu lakini haimpi mamlaka ya yeye kuwa mwombezi wenu!! hana mamlaka hayo na wala hakuna mtume wala nabii ambaye amepewa mamlaka hayo ni kristo peke yake!!

Hivi mbona neno liko wazi hizo biblia huwa mnasoma mkiwa timamu kwa kuongozwa na roho mtakatifu kwl?? au tatzo roho mtakatifu wenu huwa anakaa upande wa kulia ndo maana lakini akikaa moyoni mwako neno utalielewa vzuri sana.
 
uongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
Hahaha! unapopinga angalia usitende dhambi neno la Mungu ni nini? Kuna andiko kwenye Biblia ambalo si neno la Mungu? Unajua neno la Mungu ni Mungu mwenyewe? Ukisema alisema Maria si Mungu ina maana mafundisho ya mitume ni ya mitume si Mungu? Tatizo lenu mnapopinga Ukatoliki mnajisahau hadi mnavuka mstari.
 
Kanisa katoliki wanamuhitaji Mungu kwakwl na ndo mana wengi wanaoelewa neno huwa wanakimbia,Japo sijawahi kuwa mkatoliki lakini naskia ukifa siku ya kuzikwa padri akikuombea rehema basi unasamehewa makosa yako! Na pia mama maria ndo anawaombea wakatoliki,pia ndo dhehebu pekee ambalo pombe imehalalishwa!! Mungu atusaidie sana

Haya yote yana majibu kupitia Kanisa katoliki kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu.
Kukwepa huu mtego Martin Luther aliamua kufuta baadhi ya Vitabu vya Biblia akidhani ndio suluhisho.
 
Hahaha ....unapopinga angalia usitende dhambi ....neno la Mungu ni nini? Kuna andiko kwenye Biblia ambalo si neno la Mungu? Unajua neno la Mungu ni Mungu mwenyewe? Ukisema alisema Maria si Mungu ina maana mafundisho ya mitume ni ya mitume si Mungu? Tatizo lenu mnapopinga Ukatoliki mnajisahau hadi mnavuka mstari.
Nimemtadharisha asije kusema Paulo aliandika vile vitabu kwa matakwa yake na sio neno la Mungu....Ni hatari sana
 
Naona hujazungumzia cheo cha papa na mamlaka yake, umeshau hoja ya Marton Luther ya mamlaka milyo mpa maria kuwa muombezi wenu

Kwani wewe huwezi kumuombea mtu?
Katika sala ya bikira maria kuomba atuombee, mengi ni maneno yaliyotamkwa na Elizabeth wakati ana ujauzito wa miezi sita wa kumzaa Yohane mbatizaji. Nafikiri Bikira Maria kwa 'utakatifu alionao' (according to my faith&believe) sio kosa kuomba atuombee kama tunavyofanya kwa watakatifu wengine.
 
Mbassa jr,
Naziona fikra zako, nisawa na wale wanaosema Mungu hakuzaa, maana kwao kuzaa ni kufanya tendo la ndoa na kumpa mtu mimba, Mungu amewaumba au aliwaumba wengine kwa kusudi maalumu, kama ndivyo wewe ninani uhojie makusudi yake?
 
The Son of Man,
Biblia Takatifu imeandikwa ni heri kuoa au kuolewa kuliko kuaka tamaaa alikuwa sahihi kabisa mijitu mnazini huko mnaiba halafu unaenda kutubu kwa binaadamu mwenzako pengine huyo unaetubu kwake ana mizigo kuliko hata uliyokuwa nayo na imeandikwa amtimae mtu kwa kumtamani huyo azini sasa kwa macho ya kibinaadamu mwanaume rijali apite binti manshallah weee wacha kabisa kawadanganyeni hao hao siku ya mwisho kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe nasema ukiijua kweli nayo kweli itakuweka huru kwelikweli.
 
Alafu ili kulibeza Kanisa Katoliki Walokole wengi wanambeza sana Bikira Maria....wanasahau Yesu ni Mungu kweli na Mtu kweli ....sijui wewe utajisikiaje watu wakimkejeli mama yako .....Pale anaposema vizazi vyote wataniita mbarikiwa bila Kanisa Katoliki kwa mwenendo wa makanisa ya sasa angeitwa mbarikiwa ili hilo neno litimie?
 
Back
Top Bottom